Mrejesho: Mama mkwe amevunja ndoa yangu

mpenda siri

Member
Dec 30, 2015
79
40
Ndugu wapendwa wana jukwaa,

Awali ya yote niwashukuru wote waliotoa mawazo yao kipindi cha mwanzo nilipoleta thread inayosema Mama mkwe amevunja ndoa yangu

MREJESHO:…

Kutokana na mambo yaliyonipata kwenye ndoa hii iliyojaa visa na vitimbi vingi, wazazi wangu waliingia aibu kuu ya mwaka kwani ndugu na jamaa walidai kurudishiwa michango yao na walichekwa sana pamoja na kuwasihi wakwe zangu Ili waende wakamtibishe apone haraka na sherehe ifanyike bado waligoma na kusema mpaka binti yao apone.

Nililazimika kuwasaidia wazazi kulipa hiyo michango pamoja kwamba walishatumia kwenye vikao vya maandalizi ya hiyo reception na kulipia ukumbi jumla ya deni ilikuwa kama 3.m. ( Mahari ya harusi nilitoa mimi mwenyewe kama 2.1m pamoja na 1.m kwenye kamati ya harusi ) niliwahurumia wazazi wangu kwasababu mimi ndie niliyesababisha aibu hiyo kwani nilioa mtu asiejitambua na alikuwa na dharau nyingi kwani alidiri kusema ningewasikiliza wazazi na kuacha kumwoa yeye kwani wazazi walinionya nisioe mnyarwanda.

Itaendelea…
 
aiseee!!!!! pole mkuu,,,, ila ndoa ya aina gan? kama kikristo tafuta suluhu nasio kubomoa,,,,,,,.
 
Ndugu wapendwa wana jukwaa,

Awali ya yote niwashukuru wote waliotoa mawazo yao kipindi cha mwanzo nilipoleta thread inayosema “ MAMA MKWE AMEVUNJA NDOA YANGU”

MREJESHO:………………

Kutokana na mambo yaliyonipata kwenye ndoa hii iliyojaa visa na vitimbi vingi, wazazi wangu waliingia aibu kuu ya mwaka kwani ndugu na jamaa walidai kurudishiwa michango yao na walichekwa sana pamoja na kuwasihi wakwe zangu Ili waende wakamtibishe apone haraka na sherehe ifanyike bado waligoma na kusema mpaka binti yao apone.

Nililazimika kuwasaidia wazazi kulipa hiyo michango pamoja kwamba walishatumia kwenye vikao vya maandalizi ya hiyo reception na kulipia ukumbi jumla ya deni ilikuwa kama 3.m. ( Mahari ya harusi nilitoa mimi mwenyewe kama 2.1m pamoja na 1.m kwenye kamati ya harusi ) niliwahurumia wazazi wangu kwasababu mimi ndie niliyesababisha aibu hiyo kwani nilioa mtu asiejitambua na alikuwa na dharau nyingi kwani alidiri kusema ningewasikiliza wazazi na kuacha kumwoa yeye kwani wazazi walinionya nisioe mnyarwanda.

inaendelea...

Baada ya kujifungua nilijipa muda kumsoma nione labda ilikuwa ni wenge la ujauzito lakini wapi, mwanzoni alianza kutuma meseji za kuomba msamaha na kelele nyingi za kutaka turudiane ila kwasababu ya visa na vitimbi alivyofanya kipindi cha ujauzito cha kufikia hatua ya kutaka vitu vyake vyote vya ndani tulivyopewa kwenye harusi ambavyo nilimrudishia bila kubakiza hata kijiko, matusi mengi na dharau kwangu na kwa wazazi wangu,kunipeleka polisi zaidi ya mara moja akishirikiana na mwalimu mwenzake wa kiume.

Mshahara wangu ni 450,000 kwa mwezi baada ya makato ya mkopo benki , hapo bado sijalipa deni nililosababisha kwa wazazi wangu , visa vvake viliendelea kwenye meseji kwani aliendelea kunitukana kwenye meseji na mimi nilikuwa namjibu kwani alizidi kuniudhi makusudi kwa kisingizio kuwa ni mjamzito,mimi nilimwambia ujauzito sio ugonjwa na aache matusi yake.

Nilivumilia yote nikaendelea kutuma matumizi kidogo kidogo huku yeye akiwa kwao kama 50,000 mpaka 110,000 kila mwezi nje ya vitu vya mtoto kama nguo poda, mafuta na nepi,nk. Ambavyo alivikataa kwa madai ni screpa hivyo nitoe pesa juu ya 200,000 kila mwezi.

Kimsingi hiyo gharama ningetoa kama tungekuwa bado tunaishi kama mke na mume pamoja, ila kwasababu yeye yupo mkoa tofauti na mimi,hivyo siwezi kutoa hiyo kwani na yeye ni mtumishi wa serikali hivyo tusaidiane kulea mtoto pamoja hilo niliongea na afisa elimu na akakubali kutusaidia uhamisho bila hata senti ya rushwa, kitu cha ajabu huyu mke aligoma kabisa kuhama huko alikopangiwa kazi.

Kama ambavyo watu wengi walivyosema hapa nimeanza kusumbuliwa na huyu mke kuhusu matumizi ya mtoto akidai bili ya maziwa ni eltu tisini kwa mwezi wakati mtoto bado hajafika hata miezi sita,hapo bado anadai hela ya matunzo yake na kodi ya nyumba na anadia nikikaidi nitazitoa kwa lazima kituoni.

itaendelea..
 
  • Thanks
Reactions: MC7
mwisho...

Nimefikia hatua ya kuona kwamba nilifanya makosa kuoa nchi jirani hasa pande hizo kwani kwa research yangu ndogo niliyofanya nimegundua kwamba wanawezana wao kwa wao na hivyo vijana wenzangu wa bongo angalizo ninalowapa usijaribu, tena kama uko mbioni kuoa huko au ndugu yako anataka kuoa huko mwambie atapata misukosuko mingi sana na mwisho wa siku atakimbiwa kama mimi

Yapo mambo mengi sana ila sijaweka hapa kwani ningewachosha wasomaji wa hiki kisa. Wanawake wa kutoka kwa rais mrefu kuliko kweli ni wazuri wa sura na maumbo na wengi wao na wanafaa kwa matumizi ya binadamu, ila kama unalengo la kuoa kihalali na kisheria nikupe angalizokwenye tabia zao ni zero. Hivyo kuwa makini japo mwanzo atajifanya kuwa na malengo na ndoa na hata ukiwa ni mtu wa matumizi atajidai kukupa ushauri mzuri wa pesa zako ila ukishaweka ndani ndo utajua kama maharage ni mboga au futari.take care guys. Kwani lazima atazaa na mtu wa kwao ila mimi sijapima D.N.A.

Naomba ushauri wa kuvunja ndoa hii ya kikristo tena kanisani kabisa ,Je nifuate hatua zipi kuanzia mwanzo mpaka mahakamani ?,Gharama za D.N.A zikoje? Je gharama za matunzo kwa mtoto kwa mwezi ni shilingi ngapi kisheria hapa bongo?

NB; Usinishauri kuendelea na ndoa hii kwani haiwezekani kuishi nae tena, hata maandiko yanasema chumvi ikiharibika haifai tena kwa matumizi hata itiwe nini. Karibuni….
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Aisee usifuate biblia utajitia hatiani mwenyewe kwa hapo ulipofikia achana nae tu usihangaike na mambo ya kanisani mpe talaka ya kawaida tu then make sure unapiga chini ki kweli usiwe na kigeu geu kama zeru zeru baadae.
 
Ndugu pole sana kwa yaliokusibu,huyo mkeo hamuwezi kuendelea nae maana huko kutaka kukurudia ni kwa sababu amezaa na wale wote waliokua wanamdanganya wamemuacha ila jua kwamba mtoto akikua ataendeleza tabia zake.Kwa ushauri wangu kwa wanajukwaa si wanyarwanda wote wana tabia hizo ni isolated cases kama zile tunazosema kuhusu wamachame though inakua ngumu kumtambua nani ni mwaminifu na nani sie.Kama unataka kumuoa na ndugu wakakukatalia kaa chini na ufikirie mara mbili
 
mwisho...

Nimefikia hatua ya kuona kwamba nilifanya makosa kuoa nchi jirani hasa pande hizo kwani kwa research yangu ndogo niliyofanya nimegundua kwamba wanawezana wao kwa wao na hivyo vijana wenzangu wa bongo angalizo ninalowapa usijaribu, tena kama uko mbioni kuoa huko au ndugu yako anataka kuoa huko mwambie atapata misukosuko mingi sana na mwisho wa siku atakimbiwa kama mimi

Yapo mambo mengi sana ila sijaweka hapa kwani ningewachosha wasomaji wa hiki kisa. Wanawake wa kutoka kwa rais mrefu kuliko kweli ni wazuri wa sura na maumbo na wengi wao na wanafaa kwa matumizi ya binadamu, ila kama unalengo la kuoa kihalali na kisheria nikupe angalizokwenye tabia zao ni zero. Hivyo kuwa makini japo mwanzo atajifanya kuwa na malengo na ndoa na hata ukiwa ni mtu wa matumizi atajidai kukupa ushauri mzuri wa pesa zako ila ukishaweka ndani ndo utajua kama maharage ni mboga au futari.take care guys. Kwani lazima atazaa na mtu wa kwao ila mimi sijapima D.N.A.

Naomba ushauri wa kuvunja ndoa hii ya kikristo tena kanisani kabisa ,Je nifuate hatua zipi kuanzia mwanzo mpaka mahakamani ?,Gharama za D.N.A zikoje? Je gharama za matunzo kwa mtoto kwa mwezi ni shilingi ngapi kisheria hapa bongo?

NB; Usinishauri kuendelea na ndoa hii kwani haiwezekani kuishi nae tena, hata maandiko yanasema chumvi ikiharibika haifai tena kwa matumizi hata itiwe nini. Karibuni….
Ndoa za kanisani zinahangaisha sn kutengana mpaka pawe mambo mazito na ya muda yanayohatarusha uhai wa mtu,mm on mehangaika sn lkn nimepata njia na sasa nnaenda mahakamani,yapo makabila na nchi wanafaa kuoana wao kwa wao,kwa bongo wanyakyu na wanyira wanapaswa kuoana wenyewe,ni majipu ukioa huko,hao wa nchi hyo na wale wa ndombolo ya solo nao wanafaa waoane wenyewe maana ni vichwa ngumu,
Pole
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Mkuu pole sana,,,,,mimi nina demu mwenye asili Ya huko Rwandan ni mzur sana nataka niwe serious nae mpaka ndoa vip hapo mkuu? Kwan wakwako alitoka kabisa Rwanda au amezaliwa tz wazaz ndio huko
 
Aisee usifuate biblia utajitia hatiani mwenyewe kwa hapo ulipofikia achana nae tu usihangaike na mambo ya kanisani mpe talaka ya kawaida tu then make sure unapiga chini ki kweli usiwe na kigeu geu kama zeru zeru baadae.

Kwani talaka inaandikwaje?
Samahani kama una sample /template / draft naomba unisaidie kuiweka hapa
 
Unaandika hivi:
Mimi fulani bin fulani
Yah:Talaka
Nimeamua kumuacha fulani bin fulani kwa sababu hizi....
Then aina ya talaka unayompa
Finish hayo mambo ya witness wawepo
No problem.
 
pole ila usitumie neno watu wa eneo fulani hawafai kuna watu wameoana ukoo na kabila moja ila wamefanyiana vitimbi ya kwako cha mtoto.

hizo ni changamoto zinakukomaza tu kindoa tuliza akili.
 
mwisho...

Nimefikia hatua ya kuona kwamba nilifanya makosa kuoa nchi jirani hasa pande hizo kwani kwa research yangu ndogo niliyofanya nimegundua kwamba wanawezana wao kwa wao na hivyo vijana wenzangu wa bongo angalizo ninalowapa usijaribu, tena kama uko mbioni kuoa huko au ndugu yako anataka kuoa huko mwambie atapata misukosuko mingi sana na mwisho wa siku atakimbiwa kama mimi

Yapo mambo mengi sana ila sijaweka hapa kwani ningewachosha wasomaji wa hiki kisa. Wanawake wa kutoka kwa rais mrefu kuliko kweli ni wazuri wa sura na maumbo na wengi wao na wanafaa kwa matumizi ya binadamu, ila kama unalengo la kuoa kihalali na kisheria nikupe angalizokwenye tabia zao ni zero. Hivyo kuwa makini japo mwanzo atajifanya kuwa na malengo na ndoa na hata ukiwa ni mtu wa matumizi atajidai kukupa ushauri mzuri wa pesa zako ila ukishaweka ndani ndo utajua kama maharage ni mboga au futari.take care guys. Kwani lazima atazaa na mtu wa kwao ila mimi sijapima D.N.A.

Naomba ushauri wa kuvunja ndoa hii ya kikristo tena kanisani kabisa ,Je nifuate hatua zipi kuanzia mwanzo mpaka mahakamani ?,Gharama za D.N.A zikoje? Je gharama za matunzo kwa mtoto kwa mwezi ni shilingi ngapi kisheria hapa bongo?

NB; Usinishauri kuendelea na ndoa hii kwani haiwezekani kuishi nae tena, hata maandiko yanasema chumvi ikiharibika haifai tena kwa matumizi hata itiwe nini. Karibuni….
Kusanya ushahidi. Mahakamani watataka ushahidi kuthibitisha kuwa ndoa imevunjika irreparably! achana na mambo ya kanisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom