Mrejesho: Mama kaniletea mke bila ridhaa yangu

Mrejesho: Mama kaniletea mke bila ridhaa yangu

baptiste

Member
Joined
Aug 17, 2015
Posts
92
Reaction score
158
Ndugu wana nzengo nawasalim,

Wiki mbili au zaidi zilizopita, niliwaeleza kuhusu binti ambae mama alikuja nae kwenye uzi huu: Mama kaniletea mke kutoka kijijini bila ridhaa yangu, nifanyeje?

Kwa ufupi ni hivi, mama kaniletea mke from village na kumuacha kwangu kwamba anaenda kwa kaka kusalimia kumbe akaenda kupanda basi na kurudi, na baadae akiwa huko kijijini akapiga simu na kudai huyo aliemuacha ni mke wangu, wameniolea.

Mrejesho;

Kwa kweli nimekua na ugomvi mkubwa na msichana wangu Florence tangu amkute huyu binti kwangu, nilijaribu kumdanganya kuwa ni cousin yangu, baadae nikadai ni mke wa ndugu yangu kaja kwa matibabu, nikabadilisha na kusema ni mchepuko wa kaka umekuja kutoka mkoani ndio nausitiri, baada ya mvutano wa karibu 2 week finally ndipo nika admit kuwa ni mke nimelazimishwa na wazazi kumuoa.

Kwa zaidi ya siku nne nyuma akawa hapokei simu zangu, jana nikaona niende alikopanga, wanawake ni watu wa ovyo sana, nashanga kufika pale nakuta kuna jitu lingine lina boxer tu limejilaza kenye kochi huku mpenzi wangu akisonga ugali pembeni jikoni, nilishikwa na hasira kali nikaanzisha vagi pale kabla ya wapangaji wengine kuja kutuamua.

Hivi inawezekanaje mtu tumetofautiana wiki moja mbili halafu haraka hivi umepata jitu lingine? Au alikua nalo siku nyingi?

Mimi sio kwamba nilimkubali moja kwa moja yule mke wa mama, nilikua bado namchunguza matendo ndipo niamue, kwanza nashangaa binti wa kijijini anakata mauno hadi siamini macho yangu, amenifanyia vitu vizito mno hadi nikaogopa, kwa kweli nahitaji kuijua historia yake ndipo tuendelee.

Ndio maana nilitaka nimbakishe Florence around, sasa na yeye ndo kanifanyia ushenzi, hovyo sana huyu binti.

Najua cha kufanya.
 
mm sio kwamba nilimkubali moja kwa moja yule mke wa mama nilikua bado namchunguza matendo ndipo niamue
Kana akili sana ka florence, kaambie nimekapenda mnoo. Sijui na yeye alikuwa na spare tyre au ndo kavuta kitu kipya hahhaha

Wewe upo humo ndani na mkeo wa kuletewa mnafanya tu yenu afu useme etu nilikuwa bado namchunguza. Kwa hiyo ulitaka Florence akae asubiri maamuzi yako while wewe upo na mtu mwingine ndani? What if ungeamua kuendelea na huyo mkeo wa kijijini, kwanza ushasema kakukoleza na Viuno. Basi wewe endelea kukolezeka huku muache Florence na yeye akolezwe huko. Mwizi akiibiwa weee mtakoma
 
We ushakubali mke tulia umtunze kama umeshakubali 'ufundi' wake basi ushapenda yakhe. Na huyo bibie mwingine achana nae maana inaonekana hicho kijeba ni cha mda mrefu mlikuwa mnashare
 
Aisee!
Any idle resources must be utilized effectively and timely
Yeye naye mtu Chief anauhitaji sana mkia maana ndo utamu wenyewe wa dunia! Pole lakini.
 
Kwisha kabisaa...no new episode wala mrejesho.
Ilishatoka hiyo kaka.huwez kukaa na mtu ndan week afu ujidai humtaki.
Sitegemei kuona mrejesho wako hapa.otherwise uje na mrejesho unatumwa ndimi..limao...vitu vichachu chachu gengeni
 
sasa ulitaka florence adode nayo? ndiyo hivyo ulikuwa spare Tyre .. we endelea na mke ulioletewa na mama tu aisee ....... flora naye kafanya yake
 
Kwisha kabisaa...no new episode wala mrejesho.
Ilishatoka hiyo kaka.huwez kukaa na mtu ndan week afu ujidai humtaki.
Sitegemei kuona mrejesho wako hapa.otherwise uje na mrejesho unatumwa ndimi..limao...vitu vichachu chachu gengeni
Ha ha ha. Umeua aisee! Na hicho ndio kitakachofuata! Binti wa kijijini katumwa huyo na keshajipanga, ana kazi moja tu - ya kuwa MKE!
 
Flerence amekunyoosha mkuu!.ukisema chanini Mzee wa boxer alikuwa pending kachukua nafasi..
 
Tulia na binti kutoka kijijini ......Florence mwachie jamaa
 
mkuu huna maana hujui unalosema. kama kweli ulikuwa wampenda florence usisex na huyo wa kijijini hadi mwenyewe angejiondokea, ila uliamua kumhamishia kwako ili ufaidi alafu sasa waleta vurugu ya nini
 
Eti anakata mauno... Tamaa ilimponza bwana afya wa porini. Kilicho baki komaa na Zubeda, huyo born town mwachie mzee wa boxer.
Mwambie mama mamsapu yupo gudi wafanye mipango ya komoni, chimpumu, ulanzi ili upewe jiko rasmi uendelee kupika familia.
 
Afu mi huwa sipendi watu wa dizaini hii kushindwa kuhandle situation ndogo tu hii na kukimbilia huku jf kwa ushauri kama demu! Mapenzi ya kitoto hayo kupanick upuuzi! Ndio kwanza ujifunze kupenda naona
 
Florence ana akili sn, maana kumbe wew n mshenzi. Ulitaka umfanye yeye wa akiba, sasa kakuwahi roho imekuuma sn endelea na huyo mkata viuno acha kumpotezea muda Dada wa watu maana maisha yako kwnz hujielew akili umeshikiwa na watu.
 
Back
Top Bottom