MREJESHO: Kinachoendelea Mpaka sasa

Mfalme Daudi

Senior Member
Dec 23, 2011
110
245
Nimeona Niwape Mwendelezo Wa Kile kilichoendelea na maamuzi niliyofikia mpaka sasa Tangu last time nimepost kueleza kile kinachoendelea kwenye mahusiano yangu and so far na maamuzi niliyochukua mpaka sasa! Nimejitoa kwa mpenzi wangu nimegundua haya. Je, nifanyeje?

Baada ya kupost uzi ule siku ile ya jumanne mchana 12/1 nakumbuka niliamua kuondoka Jioni yake kuelekea Dar bila kutoa taarifa yoyote kwa mama mtoto wangu! niliondoka Arusha Baada ya kutoka ofisini na kukamilisha taratibu za ruhusa mnamo saa 10 Jioni kuelekea Dar. Nikasafiri usiku kucha kwa private nikiwa na lengo la kufika Dar kabla hakujapambazuka kwa ajili ya kutimiza lengo la ambush!

Safari ilikua Poa Na Mungu Ila Baada Ya Kupita Bagamoyo Mwendo Kama Wa Saa 11 Alfajiri Tulipata Changamoto Kidogo kwenye Gari ambayo ilitubidi tuchelewe kidogo kwenye kuitatuta mpaka kunaanza kupambazuka mwendo wa saa 12 kasoro tukawa tumefanikiwa kutatua tatizo. Tukamalizia Safari ambapo mpaka saa 12 na nusu asubuhi nilikua nishafika Eneo La tukio.

Cha Kwanza Wakati nafika sikuingia ndani ya Geti moja kwa moja ikabidi nipite mpaka nyuma ya dirisha kuhakiki kama kuna chochote nitapata. Nilipoona kimya kwa kuwa Geti lilikuwa wazi kwa mda huo nadhani kwa sababu watu walikua washaanza kutoka kuelekea makazini nikaingia Ndani Moja Kwa Moja!

Nikaenda Moja Kwa Moja Mpaka Kwenye Mlango Nikastuka baada ya kuona malapa ya kiume mlangoni! Niilipogeuka kuangalia kwenye kamba nikaona kuna shati la kiume limefuliwa na kuanikwa sambamba na vest white. Moyo Ukaanza Kunienda Mbio Nikahisi Naanza Kukosa Nguvu. Nikapiga Moyo Konde Nikagonga Mlango,Mara ya kwanza,ya pili,ya tatu nikasikia kuna mtu kama Kagusa kitasa cha katoka chumbani na mlango kwa hisia za mbali kama ulifunguliwa akatoka mtu akatulia sebleni pale kwa mda kukawa kimya. Nikagonga tena kama mara 3,Kimya.

Nikapata idea baada ya kuona moja ya dirisha upande wa chumbani (Madirisha ya alminium ya kuslide) Liko wazi Nikaenda mpaka pale kwenye dirisha nikaingiza mkono kusogeza pazia ili niweze kuona ndani chumbani.

Baada ya pazia kunipisha nikawaona watu wawili ndani (Mwanamke wangu na Jamaa) Wameshikwa na kama bumbuwazi wakiwa kama wanajadili wafungue mlango ama lah! Baada ya kuniona jamaa panic ikazidi nikaanza kumshurutisha afungue mlango niingie,jamaa nae akawa ameanza kama kumsihi ''Nenda Tu Kamfungulie''.

Baada Ya argument za mda mchache alikuja mpaka sebuleni na kunifungulia mlango nikaingia moja kwa moja mpaka ndani na kuanza kugomba huku nikiwashurutisha watoke. Nilipandwa na hasira na niliumia sana ila nilimwomba Mungu anipe uvumilivu nisije fanya kitu chenye majuto mda huo. Nikafanikiwa kuwashurutisha wakatoka bila kutokea kwa ugomvi mkubwa zaidi. Baada ya kutoka nikakaa Sebuleni kwa mda kama wa lisaa lizima nikiwaza cha kufanya. Baadae nikaamua nitafunga nyumba na kurudi zangu Arusha.

Nikapumzika siku nzima ndani nikiwa na mawazo na nikiwa nimeumia na kuugua kuliko kawaida, nilichokumbuka ni kupiga magoti kuomba na kumshukuru Mungu kwa yote yaliyotokea. Baadae jioni nikatafuta fundi wa kuchomelea grill akanisaidia kutengeneza mlango wa nje uliokuwa umechomoka,Nikanunua Kofuli la lile grill,Asubuh na mapema siku inayofuata Nikafunga Nyumba nikapanda Basi Kurudi Arusha.

Mpaka Sasa niko Arusha Sijawahi kumpigia simu wala kuwasiliana nae kwa chochote Tangu Nitoke Huko Last Wednesday,Ila Siku ya Alhamisi last week nilipokea simu toka kituo kimoja cha police Dar wakaniambia kuna mwanamke ameenda kupeleka malalamiko kwamba amepigwa na anataka kufungua mashtaka. Kulingana na maelezo Afande anasema baada ya kumhoji maswali kwa kugundua kwamba ni kesi za kimahusiano ambayo walimshauri aende kwenye dawati la jinsia kujielezea.Baadae wanasema alibadili msimamo na akasema hatati tena kunifungulia kesi anachotaka ni kuchukua vitu vyake na mimi nichukue nyangu tumalizane.

Baada ya pale akaniambia na yeye amenipigia simu kunisikiliza na kuchukua maelezo kwangu pia. Basi nami nikamweleza whole situation ilivyokuwa jamaa nikamwambia yote niliyomwelezea amuulize then atagundua ukweli. Baada ya hapo Akanipa pole kwa yote na kunipatia ushauri personal ni kipi cha kufanya nikaupokea akaahidi atampigia simu kumuita kwa ajili ya maelezo zaidi na kumaliza huu utata.

kesho yake nikampigia Afande simu kumuuliza walipofikia akaniambia alimcheki lakini hakumpata hewani akamuachia ujumbe wa kurudi kituoni na akaahidi chochote kitakachoendelea atanijulisha.

Tangu Siku hiyo mpaka Leo hamna feedback yoyote nimepata toka kwao. Kikubwa nimekua mtu wa maombi sana na kumwomba MUNGU wangu anivushe kwenye hili na kuruhusu amani yake pekee ndio iamue nafsini mwangu.Na Nauhakika kwenye Hili atanipigania na nitalivuka kwa ushindi mkubwa. Nimewaza nimrudishie tu funguo na nikae kimya kusubiri Mungu aamue! Na Siwezi kuwa wa kwanza kushika simu kumtafuta. Naomba Ushauri wa ziada kama upo juu ya hili linaloendelea sasa!!...
 
Ni ukweli Mkuu na anapokuwa na wakati mgumu wa kufanya maamuzi ndiyo anazidi kuumia.

Mpaka hapo alisharahisisha mambo, maana nyumba ameshaweza kuichukua.

Ampe vitu vyake kiusalama tu, amwache aendelee na mishe zake. Asigombane naye zaidi maana wana mtoto tayari, huwezi jua ya mbeleni.

Akabidhi nyumba fasta, maana dada anaweza kurudi akabomoa akachukua vitu vyake halafu akavidai.
 
Mbona huna maamuzi? Umeshindwa ku'move on? Basi rudiana nae kama vipi maana hata hujui upande wako wa kusimamia.
Nimewaza nimrudishie tu funguo na nikae kimya kusubiri Mungu aamue
Ilipaswa umtolee vitu vinavyomuhusu kabla hujageuka kurudi uliporudi....Kama una huruma sana mpe funguo aendelee kuishi hapo na wewe ufanye yako. Nina imani hukulipa kodi ya mwaka mzima, itamuishia tu
 
Polee sana mkuu, hawa viumbe tuliambiwa tuishi nao kwa akili, Kuna mda inabidi uwe mkatili ukiwa mpolee sana watakusumbua,

Hivyoo vitu vyake ungevitoa njee ufunge mlango wako Kodi ikiisha tafuta watu wenye uhitaji hivyoo vitu vyako vitoe MSAADA utaishi kwa amani kulipo kuendelea kubaki navyoo.
 
Uamuzi uliochukua wa kuishinda hiyo vita bila kupigana wala kufanya chochote huo ndio uamuzi wa kiume,mtu asije kukudanganya kwamba, sijui ungemla-witi mgoni,sijui ungewapiga sana. Hakuna chochote ambacho wewe ungekipata zaidi ungekuwa jera sasa. Hongera sana kwa hilo. Mimi mwenyewe ningefanya hivyo. Kwa sasa fanya mpango kampatie vitu vyake vyote,ksbb kaenda kureport polisi ukifika nenda moja kwa moja hapo polisi,waambie nataka aje achukue vitu vyake na polisi awepo. Vitu vyako ikiwezekana ondoka navyo ksbb upo arusha kikazi funga nenda navyo. Ni rahisi tu namna ya kusafirisha. Unasafirisha kwa malori yapo kariakoo ni bei rahisi sana. Hata mabox ya kufungia mizigo yapo kariakoo. Ukihamishia vitu vyako uliko itakufanya usahau yote ya dar kwa haraka. Huyo ni mke au mpenzi au mchumba?. Nahisi nimedandia tren kwa mbele,kama kuna tred nyingine ilikuwepo,ila mimi nimejibu hii
 
Halafu kwa sasa hivi akili yako haipo sawa kabisa. Kwa sasa moyo ndio unaokuongoza. Nadhani kila ukifumba macho unamuona anavyovutia na umbo lake akiwa uchi, unayaona makalio yake yanavyovutia, kisha unapiga picha kuna jamaa mwingine anapendwa kuliko wewe na anayashika hayo makalio kadri anavyojisikia, ...hicho ndio kinakuumiza jomba. Okay fanya hivi jikaze kama miezi miwili hivi bila kumtafuta. Nina uhakika yeye na huyo jamaa hawezi kudumu zaidi ya miezi miwili, wataachana tu. Baada ya miezi miwili mtafute kupima upepo, ukikuta bado yupo na jamaa basi jiambie nafsini mwako kuwa huyo sio wako tena, na uweke nadhiri ya kuachana naye. Ila ukimkuta washamwagana na jamaa basi mrudie ili usiendelee kuumia. Huyo demu unampenda mpaka basi hivyo wewe ufuate moyo wako baada ya hiyo miezi 2 provided hayuko na jamaa.
 
Halafu kwa sasa hivi akili yako haipo sawa kabisa. Kwa sasa moyo ndio unaokuongoza. Nadhani kila ukifumba macho unamuona anavyovutia na umbo lake akiwa uchi, unayaona makalio yake yanavyovutia, kisha unapiga picha kuna jamaa mwingine anapendwa kuliko wewe na anayashika hayo makalio kadri anavyojisikia, ...hicho ndio kinakuumiza jomba. Okay fanya hivi jikaze kama miezi miwili hivi bila kumtafuta. Nina uhakika yeye na huyo jamaa hawezi kudumu zaidi ya miezi miwili, wataachana tu. Baada ya miezi miwili mtafute kupima upepo, ukikuta bado yupo na jamaa basi jiambie nafsini mwako kuwa huyo sio wako tena, na uweke nadhiri ya kuachana naye. Ila ukimkuta washamwagana na jamaa basi mrudie ili usiendelee kuumia. Huyo demu unampenda mpaka basi hivyo wewe ufuate moyo wako baada ya hiyo miezi 2 provided hayuko na jamaa.
Sio ushauri mzuri huu kwa kweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom