Mrejesho: Je, kwa ili nililoanza kulifanya kwa huyu mpenzi wangu linaweza kuleta athari kwangu?

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,929
Habarini za siku ndugu zangu, poleni na majukumu ya hapa na pale,

Baada ya kuleta uzi kuusiana na maswahiba ya mpenzi wangu kubadilika ghafla, na kwa upande wangu kujaribu kujua kinachomtatiza ila yeye ananiambia yupo sawa tu wakati kihualisia namuona amebadilika kabisa kabisa.

Baada ya kusoma michango yenu ikanibidi nimtafute huyu mpenzi wangu wa kike, kwa nia ya kutaka kujua tu nini kipo nyuma ya pazia cha kumfanya awe katika hali ile, nilimbana sana mwishoni aliongea sentence hii " kuna shida sehemu ila nipe muda siwezi kukuambia leo, niache nipe muda kwanza"--hapa ndipo nilipozidi kumbana ili nijue shida ipo wapi, ila ndugu zangu sikufanikiwa maana alisimamia kauli yake hiyo hiyo kuwa atakuja kuniambia mbeleni, nimekaa nae miaka 4 sikumzoea hivyo alivyo sasa, amebadilika ghafla

Baada ya kuona amekataa sana kunieleza nilimuambia kauli mbili

1. Nilimuambia kama anashindwa kuniambia tatizo nini mimi kama mpenzi wake, basi sitoweza kuwa na amani na haya mahusiano.
2. Nilimuambia ombi lake la kutaka nimpe muda nimelikubali, " nakuacha uende, siku ukiona unaweza niambia utanitafuta, ukiona hauwezi niambia nakutakia kila la kheri huko uendako"

Baada ya kauli hiyo nimefuta mawasiliano yake kila sehemu.

Ni siku ya tano leo "hajanitafuta kabisa, baada ya kumuambia hivyo"

Nilipanga nimuoe mwakani, ila ndio ndege ameshapeperuka, nilimpenda na ninampenda kutoka moyoni hata hapa naumia ila sitarudi nyuma kwenye haya maamuzi

Asanteni kwa mawazo yenu, Mungu awabariki sana
 
Mi mwenzenu moyo na mwanamke Sina kabisa. Huyo kapata mwingine aliyemrubuni kwa vitu vidogo sana. Ngoja akatest booster huko akiona mambo yako kombo na alichokitegemea jua atarudi na 260km/h kwako.
 
Pole sana
Hawa wanawake sio wa kuwaamini, mwanamke akikwambia nipe mda jua ushaachwa kijanja hapo.
 
Mi mwenzenu moyo na mwanamke Sina kabisa..
Huyo kapata mwingine aliyemrubuni kwa vitu vidogo sana...
Ngoja akatest booster huko akiona mambo yako kombo na alichokitegemea jua atarudi na 260km/h kwako.
ndio ivyo kuu, ngoja maisha mengine yaendelee
 
Duh aya mambo ya kupenda penda huku ngoja nitafute kwanza maisha. Lakini mkuu ungekua na mtu wa pembeni kidogo nadhani ingekua relief kwako usingekua na mawazo au maumivu. Mimi na mpenzi wangu ambae nadhani nitamuoa nimekaa nae au tumejuana since niko form four miaka 8 imepita huko lakini always najua hawa wanawake ni selfish wanarubunika kiwepesi (kuna mtu humu alileta mada kuhusu wanawake).

Najua endapo ikitokea akiondoka siwezi Kua na maumivu kihivyo japo mwanzoni utamkumbuka kwa sababu ni mtu ambaye kila siku mlikua mnaongea nae, lakini kumbuka kitu kimoja Mungu ametuumba kwa mtindo wa kusahau ndio maana wazazi wetu wanafariki au ndugu zetu lakini tunaumia but tunasahau tunaishi normal tu. Kwa kukushauri jipe mda fanya mambo yako jioni au asubuhi kimbia fanya mazoezi week moja au mbili mbeleni utabaki kujishangaa kwanini ulikua una mng'an'gania.

Lakini ukiruhusu mawazo yakutawale labda unawaza yuko na msela anakazwaa utaumia, utakonda utawaza mpaka mama yako atakuuliza tatizo nini mwanangu unamjibu ""wewe mama tulia bado mdogo haya mambo huyajui ""

TAFUTA MAISHA NDUGU
 
๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ Mwenzio huko kashukuru kweli kweli umerahisisha mambo sasa huku anagegedwa kwa raha zake.
 
kaka najua ni chungu, najua inachoma na kuumiza pia lakini piga moyo konde yataisha na utasahau kila kitu uyo sio wako kutoka kwa mungu subiri wako anakuja mungu akipanga hakuna ambae ataweza kutengua nakutakia maisha mapya๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Duh aya mambo ya kupenda penda huku ngoja nitafute kwanza maisha. Lakini mkuu ungekua na mtu wa pembeni kidogo nadhani ingekua relief kwako usingekua na mawazo au maumivu. Mimi na mpenzi wangu ambae nadhani nitamuoa nimekaa nae au tumejuana since niko form four miaka 8 imepita huko lakini always najua hawa wanawake ni selfish wanarubunika kiwepesi (kuna mtu humu alileta mada kuhusu wanawake)...
""wewe mama tulia bado mdogo haya mambo huyajui "" ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ you made my day ndugu.
 
kaka najua ni chungu, najua inachoma na kuumiza pia lakini piga moyo konde yataisha na utasahau kila kitu uyo sio wako kutoka kwa mungu subiri wako anakuja mungu akipanga hakuna ambae ataweza kutengua nakutakia maisha mapya๐Ÿ™๐Ÿ™
shukrani sana mkuu, ubarikiwe sana ndugu yangu
 
""wewe mama tulia bado mdogo haya mambo huyajui "" ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ you made my day ndugu.
Ni kweli ndugu Mimi niko kwenye mahusiano ambayo sijui yanahusiana na nini ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Simama Eneo Lako
Unachoamua Kiamini Halafu, Mwache Aende Zake Salama. Akishindwa Huko Hakuna Kurudi Kwako
 
Back
Top Bottom