Mrejesho: Hatimaye Hajir wangu anaolewa

Mrejesho: Hatimaye Hajir wangu anaolewa

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,403
Reaction score
2,550
Ni matumaini yangu mmeamka salama kama Mimi. Mlioamka vibaya, Mungu awasimamie siku yenu iwe nzuri.Bila kupoteza wakati naanza kutiririka yaliyomo moyoni mwangu.

Siku chache zilizopita nilileta Uzi humu nikielezea jinsi nilivyomkumbuka X wangu Hajir ambae tuliachana kisa linimzaba kofi moja la kikurya baada ya kumkuta anachati na jamaa. Nashukuru watu wengi walinishauri niongee nae ikiwezekana tuyajenge ili hali yetu irudi kama zamani. Kwa kuwa nampenda Hajir, niliamua kumtafuta hadi kwenda kwao ili niweze kuyajenga nirudishe furaha yangu. Yaliyonikuta huko kwao mpaka kesho sitasahau...kumbe wanawake ni ny*k* kiasi hicho!

Huyu mjinga si amechumbiwa na ndoa yake mwezi wa kumi. Yaani nilipoambiwa hivyo na brother wake Ali nilijihisi kama vile nimefungiwa mzigo mzito mdomoni. Sikuwa na la kuzungumza zaidi ya kuchuruzikwa na machozi ya hasira. Mbaya zaidi nasikia anaolewa na Kei.

Kei ndo wa kunifanyia hivyo Mimi? Kei mshikaji wangu nimepiga naye O level. Na ndiye aliyekuwa ananambia kuwa Hajir ni kama vile hajatulia. Ndo Kei huyu huyu mtoto wa mama Kei. Ambaye nilikuwa na msaidia kwenye masomo. Dah, watu hawanashukurani hata kidogo!!

Sasa nimeamua kumove on na maisha yangu. Nahisi kwa sasa nahitaji mtoto tu; sitaki kuishi na kiumbe anayeitwa mwanamke. Maana nikiishi na mwanamke yeyote ntakuwa najidanganya tu maana Hajir peke yake ndiye mwanamke ninaempenda japokuwa kanitenda. Anyway, kwenye ndoa yake nimepanga kumpelekea zawadi kupitia kwa rafiki yake Aisha. Naamini akiipata hiyo zawadi, atajua Mimi pekee ndiye ninae mpenda kuliko hata mama yake anavyompenda.

Asanteni muwe na Siku njema.
 
Ubongo wako unakudanganya. Embu jiulize, akishajua unampenda kuliko mama yake then what? Awe anamtoroka mumewe aje? Kama unataka kufanya jambo fanya kabla hajafunga ndoa. Ila pia haya mapenzi ya kiwango hiki huwa mnayapatia wapi? Ushawahi jiuliza kwanini unampenda mtu kwa kiwango unachompenda? Sababu huwa inakuwa ni nini? Au ni ubongo wako tu unacheza na mwili wako?
 
Ubongo wako unakudanganya. Embu jiulize, akishajua unampenda kuliko mama yake then what? Awe anamtoroka mumewe aje? Kama unataka kufanya jambo fanya kabla hajafunga ndoa. Ila pia haya mapenzi ya kiwango hiki huwa mnayapatia wapi? Ushawahi jiuliza kwanini unampenda mtu kwa kiwango unachompenda? Sababu huwa inakuwa ni nini? Au ni ubongo wako tu unacheza na mwili wako?
Kama kutangaza nilimpenda kosa, acha nifungwe
 
Hivi....
Hizi nguvu za kuwaza mapenzi asubuhi namna hii tena mida ya kazi, huwa mnazipata wapi...!!??
Anyway, awamu hii huyu baba ajipange sana ili kutokomeza umasikini kwenye hiki kizazi cha akina Kei
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama kutangaza nilimpenda kosa, acha nifungwe
Kuna Mtu alishawahi sema "kupenda sanaaa mpaka unashindwa kukumbuka kuwa zawadi ya kuishi si ya milele kupoteza mda ukimuwaza mwanamke/mme tu ni kilema kama ukipofu, ukiziwi au ukiwete". Mm naamini wewe si kilema.
 
Kwa hiyo Kei ameamua kumchukua demu wako?
Halafu wakati Kei anajipanga kwenda kuoa hakukwambia kwamba anaoa?
Hapa inaonesha Kei hakuwa mshikaji wako ila wewe ulitaka zaidi kuwa mshikaji wake.
Anyway mtu anayekupiga ngwala ili kukudondosha ni yule aliyekaribu yako.

So just Move On, Maisha ndio haya haya.
 
Unategemea angeendelea kukusubiri mpaka ujisikie kumrudia? Wengi yanawatokea haya. Mtu anakurupuka na kumsema mwenzake kwa maneno mabaya ya kejeli na kumtukana, anamuacha akidhani amemkomoa kumbe umejikomoa mwenyewe. Unarudi unalia heeee.... hata mimi nisingekusubiri, ukinitema natemeka.
 
Kama wewe umempiga kofi mwenzio anampiga ndoa.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
IMG_20190916_081515.jpeg
IMG_20190916_081515.jpeg
IMG_20190916_081515.jpeg
 
Back
Top Bottom