Mrejesho baada ya selection TCU

Mrejesho baada ya selection TCU

Crystal field theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2014
Posts
951
Reaction score
412
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
imeongeza muda wa udahili wa
wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo
vikuu mwaka wa masomo 2016/2017 ili
kuwapa fursa waombaji ambao wana sifa
lakini hawakupata vyuo kutokana na
ushindani wa vyuo na kozi
walizozichagua.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu
Mtendaji wa TCU Prof. Eleuther Mwageni
alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari juu ya mwenendo mzima wa
udahili kwa mwaka wa masomo
2016/2017, leo Jijini, Dar es Salaam.
“ Tume imekamilisha awamu ya kwanza
ya udahili kwa waombaji wenye sifa ya
kidato cha 6, ambapo jumla ya waombaji
wote ilikuwa 55,347, waombaji wenye sifa
ni 47,203 sawa na asilimia 85.3 ya
waombaji wote. Katika waombaji hao
wenye sifa waliopata vyuo ni 30,731
sawa na asilimia 65 na waombaji 16,472
ambao wana sifa sawa na asilimia 35
hawajapata vyuo hadi sasa, waombaji
waliokosa sifa ni 8,144,” alifafanua Prof.
Mwageni.
Amesema kuwa Tume imeamua
kuongeza muda wa udahili kuanzia
Septemba 12 mpaka Septemba 23, 2016
ili kuwapa nafasi waombaji wenye sifa,
fursa ya kuomba tena vyuo na kozi zenye
nafasi kutokana na wengi wao kuomba
vyuo na kozi za aina moja.
Prof. Mwageni alivitaja vyuo ambavyo
vimeombwa na waombaji wengi na tayari
vimeshajaa kuwa ni Chuo cha Ardhi, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu
cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi
Shirikishi, Chuo Kikuu cha Kikristo cha
Tiba Kilimanjaro(KCMUCo) na Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.
Pia alizitaja kozi ambazo zimechaguliwa
na waombaji wengi kuliko nafasi zilizopo
kuwa ni kozi ya Ualimu, Udaktari wa
Binadamu, Ufamasia, Uhandisi, Sayansi
ya Uthamini wa Ardhi na Sheria. Alitoa
mfano wa kozi ya Ualimu Chuo Kikuu
Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam
ilikuwa na waombaji 15,803 wakati nafasi
ni 1,000.
Hivyo amewashauri waombaji waliokosa
nafasi kuomba vyuo na kozi zisizo na
ushindani ili waweze kupata nafasi kwa
awamu hii ya pili.
Aidha Tume hiyo imepunguza viwango
vya udahili kwa waombaji wenye sifa ya
stashahada kutoka GPA 3.5 mpaka 3.0.
Hivyo wamewataka waombaji wenye
vigezo hivyo kuomba vyuo na kwa wale
waliomba awamu ya kwanza
hawatatakiwa kuomba tena bali kusubiri
matokeo ya waombaji wenye sifa ya
stashahada
 
Ndugu zangu bado sijailewa taarifa iliyotolewa
Mwanzoni kasema waliokosa ni 16 elf na ushee ambao Wana sifa Baadae kasema ambao wamekosa vyuo na ambao Wana sifa ni 24 elf na ushee
Je Kuna majina ambao vyuo wamewakataa au?
Nielewesheni ndugu
 
Ndugu zangu bado sijailewa taarifa iliyotolewa
Mwanzoni kasema waliokosa ni 16 elf na ushee ambao Wana sifa Baadae kasema ambao wamekosa vyuo na ambao Wana sifa ni 24 elf na ushee
Je Kuna majina ambao vyuo wamewakataa au?
Nielewesheni ndugu
COMPETITION NI KUBWA MNO COZ WENG WAMEAPPLY VYUO VYA SERIKALI NA KUVIACHA VYA PRIVATE
NA PRIVATE NAFASI ZIPO ZA KUTOSHA ILA APPLICANTS NI WACHACHE SO WAKIFANYA MASIHALA PASIPO BADILI GIA LAZIMA WAACHWE NA KUCHUKULIWA BAADHI KAT YAO ILI UPATE CHANGANYA MACHAGUO PRIVATE NA GOVT
 
Jamani nina CEES form six yaani div.3 ya 13 je naweza apply upya chuo au.maana nilisha maliza lakini nataka kusoma degree mpya
 
Don't lose hope
Mimi niko selected but hyo taarifa iliyotolewa sijailewa kabisa
Kama mlimskia vizuri amesema Mwanzoni waliokosa ni 16 elf na ushee na Baadae akasema wamekosa 24 elf
Sijailewa ndugu zangu
Au pamoja na kambwa tumechaguliwa tunaweza kutemwa na vyuo?
 
Jamani nina CEES form six yaani div.3 ya 13 je naweza apply upya chuo au.maana nilisha maliza lakini nataka kusoma degree mpya
pole viwango vimebadilika at least 2D.....,PRINCIPAL NI D
 
Ndugu zangu bado sijailewa taarifa iliyotolewa
Mwanzoni kasema waliokosa ni 16 elf na ushee ambao Wana sifa Baadae kasema ambao wamekosa vyuo na ambao Wana sifa ni 24 elf na ushee
Je Kuna majina ambao vyuo wamewakataa au?
Nielewesheni ndugu
Hiyo 24 mbona sijaiona
 
Back
Top Bottom