Mrejesho: Atafia mikononi mwangu

Mrejesho: Atafia mikononi mwangu

Dr.

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2014
Posts
217
Reaction score
193
Kwanza natoa shukrani za dhati kwa wote waliochangia mawazo yao katika mkasa ulionitokea kazini, pia niwatoe wasiwasi wliofikiri kua ni simulizi tu. Nirudi kwenye mada. Baada ya kuwaza sana huku nafsi yangu ikinituma jamaa nimchome sindano ya sumu, nimuoverdose au nimnyonge kabisa niliamua kutekeleza wajibu wa kazi yangu.

Niliandika barua ya kusitisha rikizo yangu ambayo ingeanza siku mbili baadae ili nishiriki kikamilifu katika kuhakikisha anapona huku mke wake ambae ni binti mdogo tu, ndugu jamaa na marafiki wakisistiza tuwape uhakika kama mgonjw wao atapona au waruhusiwe kumpeleka nje ya nchi .

Siku ya Jumatatu tarehe 26 mwezi wa tano alipata nafuu na kuhamishwa kutoka chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU). Kipindi chote nmekua karibu nae nikijaribu kumdadisi. Nafikiria kumwambia pamoja na kuokoa maisha yake lakini alimuua rafiki yangu roho inasita, nataka nilipeleke swala hili katika vyombo vya usalama ili sheria ifuate mkondo wake ila pia naona huenda ukakosekana ushahidi wa kutosha kumtia hatiani.

Kinachoniuma ni kua pamoja na kua ni miaka imepita tangu rafiki yangu auawe kuna uhasama mkubwa kati ya familia yetu na familia ya marehemu rafiki yangu nikihusishwa na kifo chake, pia maisha duni inayoishi familia ya Marehemu kwani yeye ndiye kijana aliyetegemewa asome ili aikomboe familia yao na kinachoniuma zaidi ni misukosuko mingi niliyopitia baada ya kifo cha rafiki yangu hadi leo. Yani Dr. MO nimechanganikiwa.

HADITHI INAANZIA HAPA
 
Sikuona simulizi la mwanzo...too bad
 
Ungeweka link ya simulizi ya awali ili wengine ambao hatukuona tupate mtiririko mzuri wa story.
 
pole umefanya vyema sana kutimiza wajibu wako. Mungu atakutetea kwa namna nyingine iko siku mambo yatakaa sawa, kama umeamua kusamehe hayo mengine achana nayo!
 
Mkuu nakupongeza kwa kuishinda nafsi najua haikuwa kazi rahisi .Napia kwa mtazamo wangu ni vyema ukaongea na huyo mgonjwa friendly muulize anamjua rafiki yako mtajie jina.
Akisema anamjua au hamjui ndipo utapata pakuanzia kuflow ifike mahali ajue kuwa maovu aliyo yafanya kuna watu wanayajua.
 
Mkumbushe matukio ambayo rafiki yako alikuwa anayafanya (kazi).
Mpe taarifa kuwa kifo cha yule kaka kimetibua hali ya hewa kati ya family yako na jamaa yako na pia kasababisha family ya jamaa iishi kwa shida sana maana jamaa alikuwa tegemeo.Kama amebakiwa na utu hii habari itamuumiza kama hana utu haita msumbua kichwa.
 
Nimekumbuka, post ya mwanzo. Kwa kweli huu ulikuwa mtihani sana na bado ni mtihani. Huyo jamaa ingawa ni mgonjwa, ila roho ya ukatili bado iko palepale, hivyo huyo mtu pamoja na wema uliomfanyia, bado anaweza kukupoteza pia baada ya kujua unajua siri yake. Mwachie Mungu.
 
mbona kama mtu ame recover kutoka dengue fever?
 
Ebu tupia link ya bandiko la mwanzo ile twende sawa
Hivi itakuwa nusu nusu
 
Umeidhulumu nafsi yako, ungepiga tu sindano ya sumu

Hakuna kuwa fair kwa dunia hii mbovu na chafu

Unless utake kutangazwa mtakatifu
 
Kwanza natoa shukrani za dhati kwa wote waliochangia mawazo yao katika mkasa ulionitokea kazini, pia niwatoe wasiwasi wliofikiri kua ni simulizi tu. Nirudi kwenye mada. Baada ya kuwaza sana huku nafsi yangu ikinituma jamaa nimchome sindano ya sumu, nimuoverdose au nimnyonge kabisa niliamua kutekeleza wajibu wa kazi yangu.

Niliandika barua ya kusitisha rikizo yangu ambayo ingeanza siku mbili baadae ili nishiriki kikamilifu katika kuhakikisha anapona huku mke wake ambae ni binti mdogo tu, ndugu jamaa na marafiki wakisistiza tuwape uhakika kama mgonjw wao atapona au waruhusiwe kumpeleka nje ya nchi .

Siku ya Jumatatu tarehe 26 mwezi wa tano alipata nafuu na kuhamishwa kutoka chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU). Kipindi chote nmekua karibu nae nikijaribu kumdadisi. Nafikiria kumwambia pamoja na kuokoa maisha yake lakini alimuua rafiki yangu roho inasita, nataka nilipeleke swala hili katika vyombo vya usalama ili sheria ifuate mkondo wake ila pia naona huenda ukakosekana ushahidi wa kutosha kumtia hatiani.

Kinachoniuma ni kua pamoja na kua ni miaka imepita tangu rafiki yangu auawe kuna uhasama mkubwa kati ya familia yetu na familia ya marehemu rafiki yangu nikihusishwa na kifo chake, pia maisha duni inayoishi familia ya Marehemu kwani yeye ndiye kijana aliyetegemewa asome ili aikomboe familia yao na kinachoniuma zaidi ni misukosuko mingi niliyopitia baada ya kifo cha rafiki yangu hadi leo. Yani Dr. MO nimechanganikiwa.

Akigundua unajua mkasa mzima utapigwa risasi na wewe
 
Hongera sana kwa kuishinda nafsi na endelea kuishinda nafsi tena na tena,kama nilivyosema awali kisasi si kazi

yako mwachie Mungu kazi yake,ili uwe huru na upate wepesi wa moyo zungumza naye kirafiki tu mwambie yote

aliyofanya na kisha mwambie NIMEKUSAMEHE na sina kinyongo chochote nawe.Mungu akubariki,akuongoze na akulinde na

mabaya yote siku zote za maisha yako.
 
Acha kelele unganisha na bandiko la kale hapa tusome kwanza
 
Back
Top Bottom