Kwanza natoa shukrani za dhati kwa wote waliochangia mawazo yao katika mkasa ulionitokea kazini, pia niwatoe wasiwasi wliofikiri kua ni simulizi tu. Nirudi kwenye mada. Baada ya kuwaza sana huku nafsi yangu ikinituma jamaa nimchome sindano ya sumu, nimuoverdose au nimnyonge kabisa niliamua kutekeleza wajibu wa kazi yangu.
Niliandika barua ya kusitisha rikizo yangu ambayo ingeanza siku mbili baadae ili nishiriki kikamilifu katika kuhakikisha anapona huku mke wake ambae ni binti mdogo tu, ndugu jamaa na marafiki wakisistiza tuwape uhakika kama mgonjw wao atapona au waruhusiwe kumpeleka nje ya nchi .
Siku ya Jumatatu tarehe 26 mwezi wa tano alipata nafuu na kuhamishwa kutoka chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU). Kipindi chote nmekua karibu nae nikijaribu kumdadisi. Nafikiria kumwambia pamoja na kuokoa maisha yake lakini alimuua rafiki yangu roho inasita, nataka nilipeleke swala hili katika vyombo vya usalama ili sheria ifuate mkondo wake ila pia naona huenda ukakosekana ushahidi wa kutosha kumtia hatiani.
Kinachoniuma ni kua pamoja na kua ni miaka imepita tangu rafiki yangu auawe kuna uhasama mkubwa kati ya familia yetu na familia ya marehemu rafiki yangu nikihusishwa na kifo chake, pia maisha duni inayoishi familia ya Marehemu kwani yeye ndiye kijana aliyetegemewa asome ili aikomboe familia yao na kinachoniuma zaidi ni misukosuko mingi niliyopitia baada ya kifo cha rafiki yangu hadi leo. Yani Dr. MO nimechanganikiwa.
HADITHI INAANZIA HAPA