Mrejesho 2: Barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

HustlerOG

Senior Member
Dec 27, 2022
143
183
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kheri ya Mwaka Mpya Ndugu zangu!

Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa kuniruhusu kuuona mwaka 2023. Kama nilivyowaambia mwaka jana mwishoni...Mimi ndiye yule Kijana niliyekua naomba kuonana na Mhe. Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN ili niweze kusikia Mwongozo wake, busara zake na Utashi wake kabla sijafanya uamuzi wa kujitoa uhai wangu.

Kwa bahati nzuri,..niliweza kuichukua picha yake na kuanza kuitizama sana huku nikitokwa na machozi...nikiomba anisaidie.Nilifanya kitendo hiki usiku na nikapitiwa na usingizi. Na hapo ndipo nilipoota naongea na Mhe. Rais , akiniambia...atanisaidia kunipa pesa kupitia Mama yangu MZAZI, na tena nisilie, atanisaidia. Ilipofika Asubuhi, nikashangaa Mama yangu MZAZI ananipigia simu...tukaongea pale na kisha akanitumia sh. Laki Moja.

Kiukweli nilishangaa kitendo hiki, imekuaje hiyo connection, na kwa kuwa bado nilikua nina uhitaji wa pesa zaidi ya hiyo....nikasubiri tena usiku uingie...nikafanya kitendo kile kile cha kumuomba Mhe. Rais msaada kupitia picha...this time hakunitokea kwenye ndoto. Nikasema sio case.

Sasa jana mchana , nilikua mpweke sana...macho muda wote yalikua yanatoka machozi kwa mbali...hata kwa kuniangalia tu..lazima ungeweza kujua nina mistress mingi. Nikaichukua tena picha ya Mhe. Rais , nikamwambia kama tunapiga story tu vile...Mama Nimekwama..ninahitaji shilingi laki tatu...then nikapitiwa na usingizi. Nikaona kwenye ndoto ya mchana , Mhe. Rais kaja na kuniambia nitakusaidia ombi lako kupitia mtu jioni hii. Usijali mwanangu.

Kweli Bwana, kufika jioni..mida ya saa Moja hivi..nikashangaa napigiwa simu na mtu ambae tulipotezana kitambo sana....oya vipi wewe? Mbona sauti yako ipo kinyonge sana....shwari mtu wangu? Unatesekea pande zipi mkali wangu? Maswali yake yakawa hivyo ..then mwisho wa maongezi akaniambia sikilizia muamala hapo na wewe uifurahie sikukuu....

Mara triii laki tatu ikaingia....aloooo wee!!!

"Ndugu Mteja
Umepokea kiasi cha TZS 300,000 katika akaunti yako nambari: 01525*****00
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0714197700"

Sasa basi, napenda kuchukua nafasi hii , kukushukuru sana Mhe. Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN kwa kunisaidia hitaji langu.

Nakuahidi 2025 nitakupa kura yangu. Nakushukuru sana Mama yangu. Nakutakia Heri ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2023.


Nakushukuru sana sana Mama ( Tears of joy) . Kweli nimekukubali Mama , Hakika unaupiga mwingi!

Ng'ara SAMIA Ng'ara!!!!!

WhatsApp%2BImage%2B2021-03-23%2Bat%2B3.57.24%2BPM.jpg
 
Hakika washirikina hawataingia peponi.
Ushirikina umeingiaje hapo Ndugu? Kama huna MAARIFA ya kuhusu Picha ya RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA..Kaa kimya!

Seems nyie ndo wale ambao , mnazini maofisini na kuomba RUSHWA mbele ya picha ya Mhe. Rais...na hapo hapo mnataka mpandishwe madaraja au muongezewe mishahara...., Mkidhanj hawaoni mnayotenda! Shame upon you!!!!
 
Hauna tofauti na muabudu sanamu
Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza Bob, na unalolijua ni kama usiku wa Manani.

Think before haujacomment....

Kuna mambo mengine , sio kujudge tu ....kama hauna original idea ( precept) ya kuhusu PICHA YA RAIS , kausha!
 
Amelaaniwa amtegemeaye binadamu..badala umuombe Mungu wako mwenye hekima iliyo ya juu kupita maelezo
Mungu ndiye aliyeiweka JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA , yeye ndiye aliyeiunda SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA na pia yeye ndiye aliyewaweka WANANCHI katika SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA....na akatoa Amri tuitii pasipo shuruti... You hear Me!

Na yeye kupitia hao WANANCHI ndio akatengeneza KATIBA, SHERIA , KANUNI , TARATIBU , MWONGOZO, BUSARA na UTASHI.

" Don't you know that you are all gods..and that your bodies are the temple of God"

Kulielewa hilo fumbo ....inahitaji uwe na AKILI, na kamwe usiwe na UCHIZI, WEHU au UKICHAA wa aina yeyote!
 
And incase you didn't know.....

Tunaweka picha za wazazi wetu au za familia zetu Kwenye kuta za sebule zetu kwà lengo la kuwa Honor ( Kuwaheshimisha)...

Na tunaweka picha ya Kiongozi wetu wa Serikali, I mean picha ya MKUU WA NCHI,..katika ofisi zetu au sehemu za shughuli zetu kwà lengo la KUMTII ....na kwà kufanya hivyo ..tunajiongezea kipato.

So Picha ya RAIS inaouwezo wa kuita watu wa TRA waje wakukamate hapo dukani au ofisini kwako kama wewe ni mkwepa kodi. Na usije singizia eti kuna mtu kakuchomesha!
 
Ndugu Mteja
Umepokea kiasi cha TZS 300,000 katika akaunti yako nambari: 01525*****00
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0714197700"
:::::::::::::::::::::::::::::::::%%%
Kipande hiki ndicho kilichothibitisha wewe ni muongo konki.
CRDB bank hiyo bro
 
Acha u
Hujatosheka kuabudu sanamu.

Umeamua kuabudu picha ya samia.

Poor you.
Kama kuangalia picha ni kuabudu? Vipi na kuhusu kuangalia Jua?

Anyways ...ninachokijua Mimi ..tumeumbiwa Umoja...furaha ya Mungu ni kutuona tukiwa katika hali ya Umoja, Mshikamano na Upendo.

This requires Connection, Chemistry, Intimacy and Bond.

Kama kweli una mpenda mtu , lazima Muungane katika vitu hivyo vinne nilivyotaja.

Mfano:- Mimi Mama yangu alikua anauwezo wa kutuambia...Baba yenu atangia hapa nyumbani ndani ya dakika tano zijazo....na kweli ikawa inakua hivyo. Sasa je Mama alikua anamuabudu Baba?

Ebanaee ...Oya..sikia....NASEMAJE... " MAMA SAMIA SULUHU HASSAN , RAIS WA NCHI anaupiga mwingi sana"
 
Mhe. Rais Dkt . SAMIA SULUHU HASSAN,

Rais wa wanyonge! Asante sana Mama yangu. Umeifanya siku yangu kuwa ya furaha sana leo.

Asante sana Mama
 
Ndugu Mteja
Umepokea kiasi cha TZS 300,000 katika akaunti yako nambari: 01525*****00
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0714197700"
:::::::::::::::::::::::::::::::::%%%
Kipande hiki ndicho kilichothibitisha wewe ni muongo konki.
Hahahahahaha huyu anataka kuchukua nafasi ya yule jamaa wa kutwa lucas nani sijui.
 
Haka kajamaa kanajikuta kachawa kanadhani mama samia atapitia hii thread ili katafutwe kapewe mchongo...pambana kiume acha kulia lia kama una kipaji kiseme dunia itakiona we unadhani wakina mbape au kina diamond walisaidiwa na maraisi zao mwanzoni mwa hustle zao
 
Back
Top Bottom