Mradi wa Ziwa Victoria wapata hasara ya zaidi ya Sh500milioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mradi wa Ziwa Victoria wapata hasara ya zaidi ya Sh500milioni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by paesulta, Oct 27, 2009.

 1. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Date::10/26/2009
  Mradi wa Ziwa Victoria wapata hasara ya zaidi ya Sh500milioni
  Na Zulfa Mfinanga, Shinyanga

  MRADI mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria kwenda miji ya Kahama na Shinyanga umepata hasara ya zaidi ya Sh500 milioni tangu ufunguliwe na Rais Jakaya Kikwete.

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Kahama na Shinyanga (Kashwasha), Mhandisi Clement Kivegalo aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake juzi kuwa hasara hiyo inatokana na uharibifu wa bomba kuu unaofanywa na watu wasio waaminifu.

  Mhandisi Kivegalo alisema mradi huo, ambao uligharimu Sh252 bilioni , ulifunguliwa Mei 30 mwaka huu na tangu wakati huo valvu 22 zimeshaharibiwa na watu wasio waaminifu kwa nyakati tofauti.

  "Wiki iliyopita kulifanyika uharibifu wa miundombinu ya maji na kusababisha kukosekana kwa huduma ya maji katika miji ya Kahama na Shinyanga kwa takriban siku sita mfululizo... hii pia ni hasara mojawapo," alisema mhandisi huyo.

  Alisema kutokana na uharibifu huo, mamlaka yake ilipata hasara ya Sh420 milioni kutokana na kushindwa kuziuzia maji mamlaka za miji ya Kahama na Shinyanga.

  Alisema hasara nyingine inatokana na uharibifu wa valvu unaohusishwa na wanakijiji wasio waaminifu. Alisema kila valvu mmoja huigharimu mamlaka hiyo zaidi ya Sh1 milioni.

  Mhandisi Kivegalo aliyataja maeneo yanayoongoza kwa vitendo vya hujuma na uharibifu wa miundombinu ya maji kuwa ni kata za Iselamagazi na Solwa ambazo kwa pamoja ziliharibu valvy tisa kwa siku moja.

  Inadaiwa kuwa baadhi ya wananchi katika kata hizo wamekuwa wakiharibu miundo mbinu ya maji kutokana na kukosa huduma ya maji ya kunywa wao na mifungo yao.

  Bomba kuu la mradi huo linapita katika vijiji 54 vya wilaya za Misungwi mkoani Mwanza na Shinyanga na Kahama mkoani Shinyanga.
   
 2. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  pamoja na kuwa ningependa kuwalaumu wananchi wanaofanya uhalifu huu lakini pia hii inatokana na kuanzisha miradi bila kufiria ni kwa kiasi gani wakzi wa maeneo ambayo miradi hii inapita watafaidika.....
   
Loading...