Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Bw. Apolinary, nikiangalia mtiririko wa uzi wako, ukweli ninashindwa kujua usaidiwe vipi zaidi.
Ushauri wangu wa haraka haraka, jaribu kumuona Mtaalamu wa Mifugo wa Kata yako. Pamoja na mengine mengi anayotakiwa kukushauri, umuombe akuunganishe na Wajasiriamali ambao ni Wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa kama wewe katika Kata yenu ili ukajifunze kwao (Shamba Darasa) ili uelewe ni vipi wao wanakabiliana na changamoto kama za kwako. Usiku mwema!

Huu ushauri ni mzuri pia
 
Kama unataka kutengeneza sailage MAJANI HAYATAKIWI YAKOMAE SAANA.....Chukua muda jifunze namna ya kutengeneza sailage/ hay....hutaishia kulalamika hata kidogo....usifuge kama mababu zetu walivyokuwa wanafuga.....unatakiwa uwe tofauti......mie nina ngombe 34 ndani ya robo heka na sina shida ya chakula kwa mwaka mzima.......

Mkuu hapa umeongea pwenti nzito sana mkuu..

Hebu funguka mkuu, hao ng'ombe 34 kwa robo heka ni wa maziwa au hawa wa kawaida??
 
Mimi sio mfugaji wa ng'ombe ila najifunza ili nianzie na mbuzi, ninakuwekea maelezo haya uyafanyie kazi: Akiba ya malisho
Majani ya miti husaidia wakati kuna uhaba wa malisho hasa wakati wa kiangazi. Ulishaji wa virutubisho mbadala vinavyotokana na Calliandra, Leucaena diversifolia, Gliricidia sepium, na vinginevyo huongeza uzalishaji na ubora wa maziwa kwa wanyama wa maziwa, na pia hupunguza gharama ya chakula kwa ajili ya ng’ombe wa maziwa. Lisha kiasi cha asilimia 30 ya majani kutoka kwenye miti ya malisho. Wakulima wanashauriwa kulima malisho ya mifugo kama njia ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa malisho wakati wa ukame, pia kujiongezea kipato kwani malisho hayo yanaweza kuvunwa kuhifadhiwa na baadaye kuuzwa kwa wafugaji wengine wasiyo na maeneo kwa ajili ya kilimo cha nyasi.
Wafugaji wanashauriwa kupanda malisho mchanganyiko ambayo ni nyasi kama vile rhodes grass, African fox tail, na majani aina ya mikunde kama vile desmodium spp. Mbegu za malisho hupatikana katika maeneo yafuatayo; Chuo cha Mifugo Tengeru, na Vikuge wilaya Kibaha. Nakuwekea hii doc uisome ni wafugaji wa Moshi huko. Kifupi ni kuwa majani ya mahindi sidahni kama yatakidhi mahitaji ya protein, huwa inatakiwa waongezwe protein concentrates za kununua, kusaidia hilo ndio walifundishwa kulima hii mikunde in protein nyingi, ukisoma hii doc utaona matumizi yake. Lakini mtafute Prodigal Son alisema atakuelekeza vizuri zaidi

Safi sana Mama Joe , leo umenipa kitu cha maana sana hapa jamvini.
 
Kuna makala ya hydroponic fodder kenya wamenufaika nayo sana nadhani ni nzuri kuliko silage kwani mifugo wanapata majani mabichi kila siku na pia inaongeza mazao kwa maana ya uzalishaji wa maziwa na nyama kwa kuku nguruwe na mifugo wengine. Waweza ku google mimi nashindwa kuweka hiyo link hapa jukwaani. Ni hydroponic kenya. Waweza pata majaniabichi katika eneo dogo hata kama upo mjini kwani huchukia nafasi ndogo kuzalisha chakula kingi.
 
SHukrani sana mkuu kwa taarifa hizi

Ngoja nifuatilie google
 
Habari wapendwa wana Jf !!!!!!!!!!!!!! Mimi nina ng'ombe wangu wawili aina ya freshian ni wanunua pale ubungo
lakini wanatoa maziwa kidogo sana 3 litres per day kwa ng'ombe mmoja. Hawa ng'ombe wanapatiwa chakula bora na suppliments mbalimbali. je hawa ng'ombe wana matitizo gani!!!!!!!!!!!!!!! Tafadhali nisaidieni Mm nipo makondeko kama unaelekea kibamba Photo0135.jpg Photo0134.jpg
 
Habari wapendwa wana Jf !!!!!!!!!!!!!! Mimi nina ng'ombe wangu wawili aina ya freshian lakini wanatoa maziwa kidogo sana 3 litres per day kwa ng'ombe mmoja. Hawa ng'ombe wanapatiwa chakula bora na suppliments mbalimbali. je hawa ng'ombe wana matitizo gani!!!!!!!!!!!!!!! Tafadhali nisaidieni Mm nipo makondeko kama unaelekea kibamba

Hakikisha Ng,ombe wako wanapata maji ya kutosha;
Aina ya ng,ombe ulionao ni Ng,ombe ambao rekodi ya Uzalishaji wake haijawai kuvunjwa tangu Karne ya 19 na 20/
Angalia vile vile labda vijana au mfanyakazi wako anauza maziwa kwa wizi huku akiacha hizo litre (3)
Kama ukitaka kujua zaid andaa siku moja ushinde hapo kwenye mifugo yako,na uhakikishe wanapata kila kitu,Mwisho wa siku ndio uwakamue ili kujiridhisha.
 
Mkuu tafuta habari za huyu FLECKVIEH huyu ni balaa anatoa hadi lita 40 akifikisha uzao wa 3
 
Mkuu nimesikia habari kuhusu FLECKVIEH wanastahimili mazingira ya EAst africa , lakini makao makuu yao yapo Kenya sasa sifahamu utawapataje hao ng,ombe na cost zake zipoje. Please give more Information hata namba zako za simu mkuu!!!!! Je kuna mtu yeyote anaewafuga Tanzaniaatupe datails zao
 
Shukrani mkuu!!!!!!!! Hivyo vyote ulivyosema nilisha fanya na wala sikuona any changes. labda hii breed yake sio freshian halisia maana ni 2years sasa toka niwanunue pale Ubungo. yaani mkuu imefika wakati nataka niwabadilishe na nianze upya! ishu inakuja nitawapata wapi cattle diary ambao ni wazuri na watakaotoa high yield ya maziwa.feed za hao ng'ombe kipo in large amount. Msaada toka kwako
 
Mkuu nimesikia habari kuhusu FLECKVIEH wanastahimili mazingira ya EAst africa , lakini makao makuu yao yapo Kenya sasa sifahamu utawapataje hao ng,ombe na cost zake zipoje. Please give more Information hata namba zako za simu mkuu!!!!! Je kuna mtu yeyote anaewafuga Tanzaniaatupe datails zao

Mkuu kuna namna mbili za kupata hawa Ngo'ombe
1. Ni wewe kuomba kibali cha kuwaagiza kutoka Kenya, wizara hutoa hivyo vibari.hapa itakugharimu sana make ni lazima uwasafirishe kutoka Kenya hadi hapo ulipo

2. Ni kuagiza/kuchukua mbegu zake na uje upandikize mwenyewe, hii ndo rahisi sana, hawa Ng'ombe nilifanikiwa kuwaona kwa macho ni wazuri sana ukiwa nao kadhaa unaaga umasikini.
 
Bei yao ikoje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom