Halafu Mangi inawezekana tunajadili kitu ambacho hakipo! Hebu chungulia heading "Ng,ombe wangu wamenishinda nahitaji ushauri wako" hapo kwenye red ndo nini mkuu
heheeeeeeeee nimecheka kweli comment zako we sio Mpare unatafuta kesi ya kuku wewe? joking
Mimi sio mfugaji wa ng'ombe ila najifunza ili nianzie na mbuzi, ninakuwekea maelezo haya uyafanyie kazi: Akiba ya malisho
Majani ya miti husaidia wakati kuna uhaba wa malisho hasa wakati wa kiangazi. Ulishaji wa virutubisho mbadala vinavyotokana na Calliandra, Leucaena diversifolia, Gliricidia sepium, na vinginevyo huongeza uzalishaji na ubora wa maziwa kwa wanyama wa maziwa, na pia hupunguza gharama ya chakula kwa ajili ya ng'ombe wa maziwa. Lisha kiasi cha asilimia 30 ya majani kutoka kwenye miti ya malisho. Wakulima wanashauriwa kulima malisho ya mifugo kama njia ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa malisho wakati wa ukame, pia kujiongezea kipato kwani malisho hayo yanaweza kuvunwa kuhifadhiwa na baadaye kuuzwa kwa wafugaji wengine wasiyo na maeneo kwa ajili ya kilimo cha nyasi.
Wafugaji wanashauriwa kupanda malisho mchanganyiko ambayo ni nyasi kama vile rhodes grass, African fox tail, na majani aina ya mikunde kama vile desmodium spp. Mbegu za malisho hupatikana katika maeneo yafuatayo; Chuo cha Mifugo Tengeru, na Vikuge wilaya Kibaha. Nakuwekea hii doc uisome ni wafugaji wa Moshi huko. Kifupi ni kuwa majani ya mahindi sidahni kama yatakidhi mahitaji ya protein, huwa inatakiwa waongezwe protein concentrates za kununua, kusaidia hilo ndio walifundishwa kulima hii mikunde in protein nyingi, ukisoma hii doc utaona matumizi yake. Lakini mtafute Prodigal Son alisema atakuelekeza vizuri zaidi
nimejifunza, nimeelewa
mimi ni mfugaji wa asiliNa wewe pia ni mfugaji?au ndio unaanzaa.
Sidhani kama unahaki ya kulalamika........tunaishi huku duniani ili tuitawale hii dunia na sio dunia ikutawale wewe.......namaanisha nini.....kama unajua unachokifanya sidhani hata kidogo chakula kinaweza kikawa chngamoto...
nikulize swali...unafuga kibiashara??????
Ushauri wa BURE.......kama umehamua kuwa mfugaji....usichoke kujifunza....unatakiwa uelewe kwa siku ngombe moja anakula majani/chakula cha kiasi gani inaweza ikawa unapima kwa kilo na maji kwa siku anatakiwa anjwe lita ngapi................ukishajua hilo fanya hivi........kipindi chamvua/masika hakikisha unakusanya majani ya kutosha(kumbuka unatakiwa uwe na stoo ya kuhifadhi) kulingana na idadi ya ngombe unaahakikisha unakusanya chakula cha kutosha kuwalisha ngombe wako miezi 12 au hata miezi 24
Unafanyaje..............kama unakiu ya kujifunza....soma namna ya kutengeneza .....sailage......ukikusanya majani ( kumbuka sio kila majani kwa moshi kuna majani fulani yanaitwa ya tembo yanafaa saana...unaweza yaotesha..au kuwashawishi majirani zako wakuoteshee..kipindi cha mvua unaweza vuna kila baada ya wiki tatu kama umeyatunza vizuri........kama hiyo itakuwa ngumu unaweza tafuta karatasi ngumu yanapatikana Balton chimba shimo kusanya maji ya kutosha kipindi cha mvua unaweza otesha hayo majani kwa kumwagilkia
Muda wa kulalama mabadiliko ya tabia nchi sidhani kama una nafasi hapa......nchi kama Norway na sweden ukienda kaskazini kuna maeneo wanaliona jua kwa miezi 4tu kwa mwaka lakini hawalii lii hata kidogo......chukulia hayo mazingira kama changamoto.......kama unavyojiwekea chakula cha kutosha cha familia na ngombe wanatakiwa ufanyie hivyo
Ukitaka maelezo zaidi unaweza ni ibox kila la kheri
mimi ni mfugaji wa asili
Msukuma/Mmaasai/MbarbaiqMfigaji wa asili kivipi mkuu.
Msukuma/Mmaasai/Mbarbaiq
ufugaji wa asili nimesemaNi kweli lakini hapa tanzania hakuna asiyekuwa na asili.
ufugaji wa asili nimesema
wape magamba ,Hapa hapakufai nenda jukwAA la siasa,
Vizurl lakin tiyar nimewekeza katika ufugaji,ingekua vizur kama ungeonyesha njia nzuri ya kuwafu
Vizurl lakin tiyar nimewekeza katika ufugaji,ingekua vizur kama ungeonyesha njia nzuri ya kuwafu
Mkuu samahani nilkua sijakupata vizuri,kuusu namna kupata chakula hua inategemea na wee mwenyewe na sehemu uliopo, kwa uzoefu wangu maeneo ya tanga na kilimanjaro chakula kikuu ni nyasi(majani):Labda ungeeleza chakula gani ndo hakipatikani,na wee upo mazingiara gani...tuanzie hapo
[QUOTE=St.Apolinary;Shida ya nyasi hutokea pale wakulima wanapoandaa mashamba kwa ajili ya msimu
Habar JF Mimi ni fugaji mkoani Kilimanjaro,nina ng,ombe (4) wote ni jike,tatizo ni chakula chao kinapatikana kwa shida,
Sasa hapo nishakupata,hua kuna mbinu moja ivi ya kutunza nyasi hasa kikaribia kipindi ukame au kusafisha mashamba
Mbinu hii ni ya kutunza majani kwenye maghala,baada ya hapo ni kunchanganya nyasi zile za kwenye ghala na zingine mbichi huku ukiwapa maji ya kutosha pamoja na jiwe flani hivi la madini ya chuma(nimelisahau jina)