Mradi wa "sitaki-jojo" nauona ni kama time bomb linalosubiri kulipuka huko mbeleni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Wadau, mradi huu kwa muda sasa umekuwa ukiibua maswali mengi yasiyo na majibu, na kushindwa kutolewa kwa majibu sahihi, ni kiashirika cha awali kuwa kuna mambo hayako sahihi kuhusu huu mradi.

Pia,uzoefu unaonyesha kuwa ukiona wapinzani wanahoji ama kupinga jambo kwa nguvu na hata kufikia hatua ya kuongea na vyombo vya habari,basi ujue kuna uwezekana mkubwa tu teyari wameshapewa "tip" ya kinachoendelea na wao huongea kama whistle blower na mara nyingi tumeona muda ukiwa upande wao hivyo hata katika mradi huu wa sitaki-jojo kuna siku muda utakuja kuthibitisha mashaka yao na ndio maana nauona ni kama time bomb.

Mfano mzuri wa hiki ninachokisema, ni mashaka waliokuwa nayo wapinzani wakati ule kuhusu mradi wa gesi na ambao hata Bungeni walipinga vikali sana muswaada ule wa sheria kwani ni wazi walishajua ni nini kinaendelea na muda leo hii umethibitisha walichokuwa wanapinga maana kwa sasa habari ya uchumi wa gesi ni kama imekuifa kifo cha mende.

Hivyo,na kwenye huu mradi wa sitaki-jojo,kama tulivyoona kwenye gesi,matatizo yanaweza kuja kujitokeza kabla ya kukamilika kwake au baada ya kukamilika(iwapo utakamilika) nikimanisha utakopaanza kutumika hasa pale utakopokwenda kinyume na maelezo au ahadi za wakubwa wanazozitoa leo na kuwapa wadanganyika matumaini makubwa.

Tuombe uzima.
 
Back
Top Bottom