Mradi wa panya (APOPO) wa SUA ndani ya BBC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mradi wa panya (APOPO) wa SUA ndani ya BBC

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ITEGAMATWI, Sep 13, 2012.

 1. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
 2. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,038
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Haswaa. Hila tuache ufisadi
   
 3. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hawa panya wa APOPO, at a very early stages wanaweza kunusa jasho na kohozi la mtu wakagundua ana TB au lah! Very interesting.
   
 4. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Huu Mradi kama sikosei ulianzishwa na unasimamiwa na wa Belgium, watanzania tulivyo na visa na kupenda ufisadi hao panya wangekuwa wameshakufa kwa njaa, kuuzwa, ama kusafirishwa nje ya nchi, maana tuna viongozi weziwezi wasioamini kama tunaweza kusimamia lolote ila wana nidhamu kwa wazungu, na hata mradi ukishakuwa na wazungu ndani yake unaona unafanikiwa...
  Mifano;-
  1.Mashamba ya NAFCO yenye kila aina ya zana kama tractors, combine Harvesters, na Harrow yote yamekufa na yalikufa baada tuu ya watanzania kukabidhiwa, pale Morogoro ilibidi wawape wakorea sasa ndo wanaendesha uzalisahji wa mbegu, mashine ya kukoboa mpunga na kuu grade iliuliwa sasa imeuzwa kwa bei ya kutupwa kwa waarabu

  2.Mradi wa mabomba ya serikali, majosho ya mifugo,visima na mifereji ya umwagiliaji iliyoanzishwa na wafadhili kipindi cha Nyerere yote kwishnei

  3.Viwanda vya Ngozi, Moshi, Arusha, Morogoro vimebaki historia
  4.Kiwanda na nyumba za Urafiki wote mnaona kinachofanyika
  5.General Tyre ishajifia zamani
  6. Reli imebaki historia si ya kati, kusini mashariki wala magharibi
  7.Vyura wa kihansi
  8. Faru toka South
  9. Twiga, swala na digidigi wa Maige


  Sisi tunaweza nini zaidi ya kulalamika, kuiba, kuzini na wake za watu, kufungua bar na gest house kila mtaa...
  Shame sana kwa mimi, wewe na wote tunaoitwa watanzania, maana wezi ama ni ndugu zetu, rafiki zetu, adui zetu
  Tumekaa kimya kama maiti wakati yote haya tunaweza yarekebisha na kuwaadabisha hawa nguchiro waliotufikisha hapa
   
 5. m

  makeda JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  The hunter kwenye hiyo like naomba uongeze namba mbele kadiri upendavyo.kweli itabaki kuwa kweli.
   
 6. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280  Mkuu kwa nilivyokuelewa hapo lawama zako umezielekeza kwa serikali yetu ambayo hata mimi nipo pamoja na wewe,lakini turudi kwenye point ya msingi niliyotaka kuiweka kwenye hii post kuwa serikali pia iweke msisitizo kwenye udhamini wa tafiti mbalimbali kuleta tija kwenye sekta mbalimbali na hilo tunaliweza maana huo mradi wa APOPO wasimamizi wake ni wataalamu wa hapahapa Tanzania sema usimamizi upo mathubuti wa wabelgiji,sasa serikali ifanye hivyo pia kwenye tafiti itakazo dhamini tuone mafanikio yake itakuwaje! Maana kama wasomi na wataalamu tunao wa kutosha kufanya lolote lile.
   
 7. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145

  Chief.. sisi hatuwezi, sisi ni wezi na wabinafsi.... kizazi cha kesho hatukifikirii wala miradi ya aina yoyote hatuijali.. tunajali dili za hapo kwa hapo.. tunajali zawadi kama suti na visafari hata vinavyohusu uzazi wa mpango.. Sisi ni wepesi kulaumu wakoloni walioondoka nchini miaka 45 nyuma kama wao ndo waasisi wa umaskini wetu toka kufikiri hata kutenda.
  Jiulize miradi mingapi tumeanzisha ama kwa pesa zetu wenyewe ama za wafadhili ambayo bado ipo? Unakumbuka Kilimo kwanza kilivyoanza kwa mbwembwe... yale mapower tiller ya kichina situlinunua wenyewe? hatukuyaona kama mengi ni mabovu but sababu sisi ni watu wa dili kwani tulijali?
  Mradi wa kusambaza dawa, mbolea na mbegu kwa wakulima kwa njia ya vocha .. bado upo na umefanikiwa? si ni sisi wenyewe tuliosimamia zoezi zima? bt nini matokeo yake,..? najua unaelewa sana kilichotokea?
  Vyakula vya misaada kama mahindi vinapotolewa unajua huwa tunafanya nini? tunaiba na kuficha kwenye maghala yetu huku jirani ambao wako hatua ishirini na unapoishi wakifa njaa, nani anajali bana..
  Unakumbuka Machinga Complex.? nenda tafiti kama kuna machinga yoyote... wale unawaona pale ni ndugu wa vizito waliotolewa mikoani kuja kusimamia frem za vigogo hao..
  Vipi Kigamboni mpya..? umeona jina la mkaazi wa tandika,tandale, vijibweni, au temeke... yote si ni ya wamasaki, upanga, kimara?
  Sisi hatuhitaji cha baba yake mradi wala bibi yake mradi,... sisi tuvute mkwanja wa research tuandike sana ikibidi tucopy na kupaste.. mwisho wa siku tujaze makabati...
   
 8. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280


  Mkuu wangu nadhani bado hatuelewani,sasa kwanini mradi wa APOPO umefanikiwa chini ya uongozi wa wataalamu wa kitanzania na usimamizi wa wabelgiji?Is it kwamba Tanzania hakuna wataalamu au usimamizi wa serikali si wa makini? Miradi yote uliyoitaja inapitia kwa vihiyo tu wa halmashauri na serikali kuu vipi miradi ikisimamiwa na wataalamu wa vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za utafiti?Mwaka jana serikali ilitenga bajeti kwa tafiti mbalimbali kutoa matokeo ya tafiti hizo ni mapema lakini naimani matunda yake yanaweza patikana.Mkuu mradi wa kilimo kwanza unasimamiwa na diwani wa darasa la saba na wanasiasa mafanikio yatapatikana wapi?
   
Loading...