Mradi wa Mabasi BRT na nauli kwa watumiaji

Tiba

JF-Expert Member
Jul 15, 2008
4,604
3,163
Leo wakati napitia gazeti la Mwananchi, nimekutana na habari ya changamoto wanazokutana nazo waliopewa jukumu la kuhakikisha mradi unaanza kazi by tarehe 12 January 2016. Wamekiri kwamba bado hawajamaliza kujenga vituo kama 12 na bado hawajatengeneza parking ya magari kwa abiria watakao kuwa wanakuja na magari yao vituoni ili kutumia mabasi hayo. Wamekiri pia kwamba hawajamaliza kukokotoa nauli itakuwa shilingi ngapi. Hapa kwenye nauli ndipo hoja yangu ilipolalia.

Mmoja wa watumiaji wa daladala anayeishi Mbezi Malamba Mawili amesema yeye kwa sasa analipa Tshs. 500 (Sijui kama nauli hii imepangwa na Sumatra kwani Mbezi Malamba Mawili mpaka mbezi mwisho ni kariibu mno na nauli haipashwi kuzidi shs. 200) mpaka Mbezi Mwisho. Kutoka Mbezi mwisho anapanda daladala ya kwenda posta kwa nauli ya Shs. 600. Kwa sasa ukipanda daladala kutoka Mbezi Mwisho mpaka Kimara mwisho nauli ni Shs. 400. Tuseme kwa sasa anatumia nauli ya Tshs. 1,100 kufika mjini kati, Posta.

Tunatarajia mradi huu ukianza basi mtumiaji huyu asilipe nauli inayozidi anayoitumia kwa sasa vinginevyo yatakuwa maumivu kwa watumiaji. Sumatra zingatia ukweli huu.

La ziada nililogundua leo ni kwamba mradi huu utaendeshwa kwa pamoja kati ya wenye daladala na UDA, kwa maana hiyo mradi utaendeshwa na watu binafsi, si UDA iliishabinafsishwa kwa kina Kapuya? Nini nafasi ya Serikali katika mradi huu? Ina maana serikali imegharimia ujenzi wa barabara ili kina Kapuya na Mzee wa Masaburi wapige hela? Anayejua zaidi asaidie kutufafanulia hapa.

Naomba kutoa hoja.

Tiba
 
Back
Top Bottom