Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,954
- 4,327
Mradi wa JNPP ulianza tarehe 26 July 2019 na ulitarajiwa kukamilika na kuanza kuzalisha umeme mwezi June 2022.
Sasa kama ni kweli kwamba hadi kufika February 2021 mradi ulikuwa nyuma siku 477, maana yake ulikuwa aidha haujaanza kutekelezwa au ndiyo ulikuwa unaanza. Hii ni kwa mjibu wa hesabu nyepesi nyepesi za kutoa na kujumlisha.
Waziri wetu kadanganywa hivyo na wahandisi wa JNHPP na yeye bila kukokotoa hesabu hizo akaamini wanasema kweli. Anapaswa kuwaadabisha waongo hao. Kwa nini wadanganye hivyo?
Haiwezekani ukawa nyuma siku 477. Sote tulikuwa tunaona angalao kwenye luninga jinsi kazi zilivyokuwa zikifanyika kwenye mradi huo. Au hizo handover notes za mtangulizi wake ziliandikwa kimakosa na yeye kazisoma bila kuzitafakali?