Mradi wa JNHPP ulianza 26 July 2019 na ungalikamilika June 2022. Kama ni kweli Feb 2021 ulikuwa nyuma siku 477 ina maana ulikuwa haujaanza kutekelezwa

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,952
4,324
Mradi wa JNPP ulianza tarehe 26 July 2019 na ulitarajiwa kukamilika na kuanza kuzalisha umeme mwezi June 2022.

Sasa kama ni kweli kwamba hadi kufika February 2021 mradi ulikuwa nyuma siku 477, maana yake ulikuwa aidha haujaanza kutekelezwa au ndiyo ulikuwa unaanza. Hii ni kwa mjibu wa hesabu nyepesi nyepesi za kutoa na kujumlisha.

Waziri wetu kadanganywa hivyo na wahandisi wa JNHPP na yeye bila kukokotoa hesabu hizo akaamini wanasema kweli. Anapaswa kuwaadabisha waongo hao. Kwa nini wadanganye hivyo?

Haiwezekani ukawa nyuma siku 477. Sote tulikuwa tunaona angalao kwenye luninga jinsi kazi zilivyokuwa zikifanyika kwenye mradi huo. Au hizo handover notes za mtangulizi wake ziliandikwa kimakosa na yeye kazisoma bila kuzitafakali?
 
Kuchelewa kwa siku 477 haina maana kuchelewa kuanza inamaana kazi ambayo labda ingetakiwa kufanywa kwa siku 10 inafanywa kwa siku 70 kutokana na kusuasua kwa malipo na hela za vifaa. So watu wapo site lakini progress ni ndogo
 
Kwani Marope ni wa NCCR?? ccm wajinga sana nyie
Maendeleo hayana chama. Huu mradi utafaidisha sana watanzania wote. Hata kama NCCR au CHADEMA ingalichukua madaraka, watanzania wangaiibana ikamilishe mradi huo na mingine kama ya SGR, tanzanite bridge, daraja la magufuli la Kigongo-Busisi huko Mwanza nk.
 
Kuchelewa kwa siku 477 haina maana kuchelewa kuanza inamaana kazi ambayo labda ingetakiwa kufanywa kwa siku 10 inafanywa kwa siku 70 kutokana na kusuasua kwa malipo na hela za vifaa. So watu wapo site lakini progress ni ndogo
Ni hisabati tu Mzee zinagoma. Chukulia mradi tangu uaenze hadi leo una siku 400. Halafu mtu aje akuambie mradi tangia uanze uko nyuma siku 500 wewe utamwelewaje? Utakuwa umechelewa kuanza au kitu gani?
 
Mradi wa JNPP ulianza tarehe 26 July 2019 na ulitarajiwa kukamilika na kuanza kuzalisha umeme mwezi June 2022.

Sasa kama ni kweli kwamba hadi kufika February 2021 mradi ulikuwa nyuma siku 477, maana yake ulikuwa aidha haujaanza kutekelezwa au ndiyo ulikuwa unaanza. Hii ni kwa mjibu wa hesabu nyepesi nyepesi za kutoa na kujumlisha.

Waziri wetu kadanganywa hivyo na wahandisi wa JNHPP na yeye bila kukokotoa hesabu hizo akaamini wanasema kweli. Anapaswa kuwaadabisha waongo hao. Kwa nini wadanganye hivyo?

Haiwezekani ukawa nyuma siku 477. Sote tulikuwa tunaona angalao kwenye luninga jinsi kazi zilivyokuwa zikifanyika kwenye mradi huo. Au hizo handover notes za mtangulizi wake ziliandikwa kimakosa na yeye kazisoma bila kuzitafakali?
Huyu Chamuriho ndiyo alikuwa Waziri Wizara ya Ujenzi, Karemani alikuwa Waziri Nishati, Kareman ilikuwa kila mwezi lazima aende Hapo site.

Chamuriho ndiyo mtaalamu wa majadiliano alieshiriki katika miradi yote kuongozo timu ya majadiriano kwenye mapatano kati yetu na wakandarasi, mradi Nyerere Hydroelectric Power aliongoza timu ya majadiliano, mradi wa SGR yeye ndiyo aliongoza majadiliano, mradi wa ununuzi wa Ndege ndiye aliengoza timu ya majadiliano ata kule Bagamoyo ni yeye na timu yake ndio waliona mradi ule unawabana sana Watanzania, ikukbukwe Dr. Leonard Chamuriho ni Engineer sasa ukija kusikia mradi wa Bagamoyo unapigiwa kelele huko mbele ujue timu ya majadiliano ilikuwa ya wanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hisabati tu Mzee zinagoma. Chukulia mradi tangu uaenze hadi leo una siku 400. Halafu mtu aje akuambie mradi tangia uanze uko nyuma siku 500 wewe utamwelewaje? Utakuwa umechelewa kuanza au kitu gani?
Mkuu ulisoma hesabu kidogo?? Kuna kitu kinaitwa PROJECT. Kwa mfano mpaka kufika siku 30 unatakiwa ulime hekari 10, lakini mpka siku ya 15 ww umelima hekari 2, hapo kimahesabu upo nyuma kwa siku ngapi?? Vivyo hivyo Jamaa amekuelewesha hapo kuwa kama kazi za ufumaji wa zile nondo ulipaswa kufanyika ndani ya siku 7 lkn ukafanyika ndani ya siku 15 maana yake wamechelewa kwa siku 8, hali hii hupekea pia vitu ambavyo vilipaswa kuanza mara baada ya kukamilika kwa hizo nondo nazo kuchelewa kuanza hali inayopelekea vitu vingine kuchelewa. Kabla ya kupost kitu kaa kwanza chini uelewe kile unachopinga, nahisi hukumuelewa Makamba.
 
Jiwe na genge lake walikuwa waongo sana. Makamba anasema ukweli anaonekana anadanganywa
Dah.. Kusingeuwa na serikali wewe wangeshakumaliza hapo ulipo.

Akili za mtopeni kabisa hizi.

Mleta uzi katoa nondo hadi namba ..wewe imeleta ushenzi na ushuzi tupu.
 
ule mradi ungekamilika kwa wakati Kama ilivyokuwa imepangwa.inshu kubwa kwa Sasa ambayo huenda ikamfanya huu mradi uende hata 2025,ni pesa plus vifaa.sijui mzimu gani umeingia pale naona Kasi imepungua,tofauti na mwanzo,sikuhizi hatuonyeshwi kwenye runinga Kama zamani kazi ilipofikia.lakini hili la mradi kuwa nyuma kwa siku 477 daah sijui limekaaje
 
Mkuu ulisoma hesabu kidogo?? Kuna kitu kinaitwa PROJECT. Kwa mfano mpaka kufika siku 30 unatakiwa ulime hekari 10, lakini mpka siku ya 15 ww umelima hekari 2, hapo kimahesabu upo nyuma kwa siku ngapi?? Vivyo hivyo Jamaa amekuelewesha hapo kuwa kama kazi za ufumaji wa zile nondo ulipaswa kufanyika ndani ya siku 7 lkn ukafanyika ndani ya siku 15 maana yake wamechelewa kwa siku 8, hali hii hupekea pia vitu ambavyo vilipaswa kuanza mara baada ya kukamilika kwa hizo nondo nazo kuchelewa kuanza hali inayopelekea vitu vingine kuchelewa. Kabla ya kupost kitu kaa kwanza chini uelewe kile unachopinga, nahisi hukumuelewa Makamba.
Duh! Kumbe hizo ndizo aina ya hesabu mlizokuwa mnamdanganya Mr Makamba na yeye akadanganyika. Eti Project Mathematics! Mapenguin bwana kwa maneno ni hodari sana.

Hapa tunaongelea mradi kuwa nyuma ya muda fulani (scale) uliokuwa umepangwa. Ni hesabu ya motion (kinetics) kwenye scale iliyopangwa zinazohusisha speed ya utekelezaji. Tunachoangalia ni speedometer reading ambayo ndiyo scale yetu. Haiwezekani speedometer ikasoma negative speed. Ni aidha zero au kwenda mbele. Haiendagi nyuma.

Kwenye mfano wako wa kwanza wa kulima heka 10 kwa siku 30, scale yetu ya speedometer ni 0 hadi 30. Wewe siku ya 15 ulikuwa umelima hekta 3 tu wakati ulitakiwa uwe umelima hekta 5 (speed ilitakiwa kuwa hekta 1/3 kwa siku ili ukamilishe hizo hekta 10 siku ya 30). Hizo hekta 3 ulizolima zilitakiwa kuwa zimelimwa siku ya 9. Hivyo scale yetu siku ya 15 itasoma uko nyuma kwa siku 6. Itasoma mradi uko nyuma siku 6. Na ili uweze ku catchup inabidi speed iongezwe kuwa zaidi ya iliyopangwa. Mfano wako wa pili hau apply hapa kwani mradi wetu haujamaliza muda wake uliopangwa kukamilika ambao ni June 2022. Mfano wako huu wa pili hatusemi uko nyuma kiasi gani bali tunasema umechelewa kukamilika kwa muda gani na mkandarasi anaanza kukatwa malipo ya ucheleweshaji kuanzia tarehe ambayo mradi ulikuwa umepangwa kukamilika (end of the scale).
 
Mradi wa JNPP ulianza tarehe 26 July 2019 na ulitarajiwa kukamilika na kuanza kuzalisha umeme mwezi June 2022.

Sasa kama ni kweli kwamba hadi kufika February 2021 mradi ulikuwa nyuma siku 477, maana yake ulikuwa aidha haujaanza kutekelezwa au ndiyo ulikuwa unaanza. Hii ni kwa mjibu wa hesabu nyepesi nyepesi za kutoa na kujumlisha.

Waziri wetu kadanganywa hivyo na wahandisi wa JNHPP na yeye bila kukokotoa hesabu hizo akaamini wanasema kweli. Anapaswa kuwaadabisha waongo hao. Kwa nini wadanganye hivyo?

Haiwezekani ukawa nyuma siku 477. Sote tulikuwa tunaona angalao kwenye luninga jinsi kazi zilivyokuwa zikifanyika kwenye mradi huo. Au hizo handover notes za mtangulizi wake ziliandikwa kimakosa na yeye kazisoma bila kuzitafakali?
Kazi ya miaka mitatu iko nyuma kwa karibu mwaka na nusu hizo ni kauli za kuwarudisheni nyuma hiyo miaka na issue hapa ni upigaji unaandaliwa kaeni mkao wa kupigwa na mtapigwa ile mbaya na siyo hapo
 
Yaani kazi imefanyika mwaka mmoja na nusu tu lakini tukaikuta iko nyuma kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu!!! Hapo lazima tufanye matambiko. Tuwakodi wazeze wale wa Kwamsisi kwa shilingi angalao trillion moja. La sivyo hatutafika po pote.
 
Back
Top Bottom