Mr. President, your response to doctors' strike is tepid!

Mr. President, your response to doctors' strike is tepid!

MM, our president isn't known to be a kind of a person who'd sit down and read such a very long article; whilst, the Kurugenzi ya Habari at the state house would never tell him what has been wrote, wanamgwaya.
 
Hakuwa na uwezo na kazi aliyopewa

Hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake ipasavyo

Hawezi kutatua au kufanya maamuzi yoyote ambayo yana maslahi kwa walio wengi,haijawahi kutokea na siamini kama inaweza kutokea mpaka atakapomaliza muda wake uliobaki
 
Kuna watu wanasema; Muhimbili kama madaktari wamegoma, wagonjwa si waende kwa Kairuki?? (Kama hakuna mkate, si wale keki?)
 
Nilikuambia alichokifanya Pinda kama ulidhani ni Pinda then you are wrong!. Rais Kikwete unamfahamu fika, ubabe jeuri na kiburi chake kinafahamika usitegemee otherwise this time eti kwa vile ni madakitari.

Kwa hiyo kiburi cha Mh.Rais ni kwa faida ya nani? kuwakomoa wananchi wake? Hivi Pasco umeshaona wananchi walio wengi wanavyoside na Madaktari,ukiwa unaangalia taarifa za habari kwenye TV's hasa ITV na hata wanaochangia kupitia redioni utaona wote wanakubaliana na hoja za Madaktari,ok tunakubali Rais anakiburi lakini kwa hili basi atumie busara ya wengi wape ambao ni wananchi wanaotaka Madaktari wapewe haki zao ili na wao wapate huduma.Sasa akiendelea na kiburi hiki ni mpaka watu wangapi wafe ndio atoe maamuzi ya kunusuru hali hii?
 
Safari Hii sijui hatakutania wapi na wazee wa Dsm Kuzungumzia hili la Madaktari.Bottom line katika hili Busara na Hekima vinatakiwa Ubabe na Vitisho havina nafasi.
 
Mheshimiwa Raisi,

Niungane na barua ya Mwanakijiji na nyingine nyingi utazozipata mbelini kwenye swala hili la mgomo wa madaktari.

Mgomo huu ulipoanza nilidhani kabisa vyombo husika vitasimamia swala hili – labda kwa kuwa bado na imani na mfumo wa Serikali za Kiraia kutoa dira ya haki za msingi kwa wananchi wake. Na ni kweli, tumeona juhudi za Serikali kupitia Waziri Mkuu na Waziri wa afya lakini zilizoshidwa kumaliza mgomo badala yake kutumia nguvu za dola na mabavu. Nguvu ambazo hazikuwa za lazima. Viongozi wako wangekuwa wasikivu na wafuatiliaji wa madai ya madaktari - madai haya si mageni zaidi wataalamu wanasema mfumo wa afya katika sekta ya umma ni mbovu, vitendea kazi ni hafifu na maslahi duni - vyote vikiadhiri huduma inayotolewa. Sasa kuna ubaya gani mfanyakazi wako kukwambia ukweli?

Mheshimiwa Raisi,

Kiburi cha madaraka ni kibaya sana, hasa kwa viongozi wasiojua ama kwa makusudi kudharau nguvu ya Serikali inayojengwa na watu – na sio mitutu na bunduki - tulipiga kura za hiari. Serikali yako imeziba masikio juu ya madai ya madaktari, kazi yake imekuwa ni kutoa amri na vitisho. Eti warejee kazini ama ajira hamna. Haikuishia hapo tu mara mbwembwe ya madaktari wa jeshi ikaja! Ni mtu tu asiye na utambuzi kamili atayedhani hali tuliyonayo ni ya hatari na kujaribu kutumia nguvu ya dola na wataalamu wa jeshi kwa mgomo ambao ungeweza kuongeleka. Hii, ni dhahiri tunashidwa kutambua tofauti ya serikali ya kidemokrasia na jeshi.

Mheshimiwa Raisi,

Hii nchi haiongozwi na jeshi wala polisi. Tanzania inaongozwa na Raisi tuliyempigia kura, ingawa mimi sikukupa yangu, ila nakuheshimu kwani wewe ndio Raisi wa Tanzania. Hii ni nchi ya kidemokrasia, tena huru ambapo watu wanahaki ya kueleza kyero zao bila woga. Serikali ilipaswa kusikiliza na kuongea na madaktari. Sio kutuletea suluhu za mabavu zisizo za lazima. Ni ufinyu wa mawazo kudhani tuko vitani kutumia hazina ya madaktari wetu wa jeshi kuwa suluhu ya mgomo – tena kutumia kiongozi mkuu kama Waziri Mkuu na Waziri wa afya – kutishia watu kuachishwa kazi na kuleta madaktari wa jeshi. Chakushangaza zaidi, ni viongozi wetu kushidwa kutambua hata hao madaktari wa jeshi ni wachache kulinganisha mahitaji ya wagonjwa. Ni juha tu, anayeweza kucheza mchezo huu wa kuigiza.

Mheshimiwa Raisi,

Hii ni nchi ya utawala wa demokrasia na unajukumu la kuongoza nchi hii. Mimi labda nipishane na wenzangu, sitoi wito wa kusema ujiuzulu ama uachie madaraka, kwani hicho ni kiini macho na ni jambo ambalo huwezi kufanya, wewe kama mtu binafsi na hulka za viongozi wengi ambao wameshakuwa madarakani. Kuacha kuwa Raisi sio rahisi – na sina ndoto kwamba utafanya hivyo. Kwahiyo rai yangu mimi ni kukutaka ubebe majukumu yako ya kutuongoza kwani ni wajibu wako kutuongoza hasa pale ambapo hali ya wananchi inapokuwa tete. Nadhani tunapaswa kuweka kipengele katika utendaji kazi pale ambapo Raisi na serikali yake inaposhidwa kutimiza wajibu wake ndani ya muda stahili ifanywe nini. Maana inaanza kuwa mazoea sasa kwa serikali kukosea wananchi wake na wafanyakazi wake bila kuli uvunjaji wa haki za wananchi wala amani yao. Kama ni haki kumshtumu mwanachi kuvunja amani, na hivyo tutaifanya kosa la jinai kwa Serikali kuvunja imani. Tunaanza kufikiria hilo.

Mheshimiwa Raisi,

Nimesikia uko safari, lakini hali yetu ilipofia unapaswa kurudi nyumbani. Usianze kufanya mazoe kwamba watananzania watapiga kelele halafu watanyamaza. Yawezekana ilikuwa hivyo jana, ya leo hayatabiriki hasa kufuatia maamuzi yako juu ya kuboresha maslahi ya wabunge huku waatalamu wengine wakiendelea kukandamizwa. Kwa hadithi za redioni ama tunapoangalia kwenye luninga, haiwezekani kabisa kuelewa kwanini posho za wabunge zinaongezwa kwenye kipindi kama hiki – ambacho kinachochea vurugu kwa wananchi. Nashidwa kujilazimishwa kuamini kwamba alama hizi za fukuto huzioni – ama unaziona lakini umedharau. Hapa utakuwa umekosea sana tu.

Mheshimiwa Raisi,

Mimi kama mwananchi ambaye familia yangu imebahatika kutibiwa na hospital za umma. Hasa, siku za hivi karibuni, ninakila sababu ya kusema Serikali hawezi kuepuka kutatua mgogoro huu na madaktari. Ni dhahiri, tuna hospital binanfsi, lakini lazima tujiulize ni kwanini hospital za umma ndizo zinazofurika wagonjwa – wakiwemo wale wanaotoka wilayani na hata wale wa kutoka hospital binafsi. Hospital kuu za serikali sio tu kimbilio la watu waliochini lakini ndio sehemu yenye wataalamu waliobobea.

Mheshimiwa Raisi,

Unawajibu wa kujibu hoja za madaktari, kutuhakikishia huduma za afya sisi wananchi, na kuwajibisha watendaji wako. Lakini, la muhimu zaidi unawajibu wakutuhakikishia sisi wananchi unatuongoza katika vipindi vyenye mwamko wa kitaifa kama huu. Hayo sio maombi ni wajibu wako. Unaweza kuamua kujibu kisiasa ama kuangalia uhalisia na kutatua tatizo la sekta ya afya. Hapa tunaongelea mfumo wa sekta ya afya, ambao unawekeza zaidi katika hospital kuu, huku zahanati na wilaya zikiwa hali duni, na kufanya hospitali kuu kulemewa.

Mheshimiwa Raisi,

Ongeza taifa letu.
 
Tufike mahala SERIKALI iwepo au ionekane kuwepo. Tusitake serikali iwepo wakati wa mafuriko tu. Pinda alikuwa amejiandaa kuwapa karibu kila kitu walichooomba MaDaktari hawa Jumapili iliyopita. Wakakaidi. Wakatoa visingizio visivyo na mashiko. Sitawaunga mkono maDaktari wetu hadi wapunguze kiburi, kujiona, majigambo na mambo kama hayo.
Vinginevyo wapanue madai yao yawe kwa fani na taaluma zote nchini.
 
Does anyone in the currently dying CCM government really care about all these public plights anyway?
 
What is even more obnoxious is the fact he has approved the luxurious and lavish allowance to MPs at this very critical moment. How will they convince anybody that they don't have money to meet doctors' demands? Only on this part of the world.

Again, I ask the question, do they listen? And if they do, do they care at all?

Though nilkuwa siugo mgomo katika current formhiii kuudhinisha haya malipo ya wanasisa umenichefua tena yameidhinishwa nje ya mwaka wa bajeti.
Hivi nchi yetu do we have a financial discpline. Kwa nn mwalimu akiomba kuongezewa aambiwe asubiri next bajeti lakini kwa mbunge ni anytime........

Au mimi jamani ndio sijui hizi posho z awabunge zinazonngezwa znachotwa kutoka kwenye fuko gani. Au ndio ile chenji ya rada...... wanajipogeza
 
DO NOT drag Presidential powers over matters which the law has already assigned to other organs. Briefly, doctors’ strike is ILLEGAL. The strike has no support in law. Medical doctors should now see the importance of joining trade unions like TUCTA. I’m surprised that medical doctors do not know that there are procedures under Labour Laws for them to carry out strikes. Medical doctors are not late. They should go to the ESSENTIAL SERVICES COMMITTEE, COMMISSION FOR MEDIATION AND ARBITRATION instead of breaking the law.
 
What is even more obnoxious is the fact he has approved the luxurious and lavish allowance to MPs at this very critical moment. How will they convince anybody that they don't have money to meet doctors' demands? Only on this part of the world.

Again, I ask the question, do they listen? And if they do, do they care at all?

They listen and understand everything but the problem they are detached from citizen needs. They are there to serve themselves not to serve the people.

 
Tunisians,Egyptians and Libyans did it,Zanzibarees in 1964 did it too.WE HAVE ALL REASONS IF WE ALL CARE ABOUT THE FUTURE OF OUR SONS& DAUGHTERS TO DO IT NOW.
 
I don't think if he cares anything at all. Tanzania is not poor. JK is not a leader rather a RULER. Shame on him and his govt.:lol:
 
MM, One single voice is important than none. Let us call for the Tanzanian government to resettle her people back to their home. We need to remain united in this. I support you.
 
Watanzania tupige kelele; unajua hata kama mtu hatoamka kutoka usingizingi anaweza kujisogeza kidogo na kuzuia mbu kumuuma
 
Back
Top Bottom