Mr president ahadi ni deni-1

Katika ziara mkoani Kilimanjaro rais alihaidi Computers kwa kila shule ...Kama picha inavyoeleza wadogo zetu WAMEKAA wana subiri.


dawati.jpg

Shule jijini Dar es Salaam

Hii si afadhali mkuu,kuna sehemu hapa nchini watoto wanasomea chini ya miti,na darasani wanaishi walimu kwa kugawa darasa kama hanga la jeshi/polisi.
 
Rais amewateua watendaji wake kama vile mawaziri wamsaidie kazi. Na pia kuna wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa elimu. Hawa wanafanya nini katika maeneo yao? Mwalimu mkuu alishawahi kuishirikisha kamati ya shule na kuwaita wazazi kuona hali halisi shuleni kwake ili wachukue hatua? Watanzania wenzagu kila mmoja atimize wajibu wake naamini mambo yatakuwa mazuri.
 
Katika ziara mkoani Kilimanjaro rais alihaidi Computers kwa kila shule ...Kama picha inavyoeleza wadogo zetu WAMEKAA wana subiri.


dawati.jpg

Shule jijini Dar es Salaam

Afadhali huko Dar es Salaam wengine wamekaa kwenye madawati, vijijini wote wanakaa chini, akirudi jioni unaona alivyochafuka.
 
What is more expensive? Dawati or Computer? Kama jibu unalo awape kwanza kilicho cheap.
...Mkuu si suala la kitu gani ni rahisi au kipi ni aghali..Tatizo la ****** haelewi hata vipaumbele vya watu wake. Haingii akilini raisi wa nchi unajuwa wazi wanafunzi wako bado wanakaa sakafuni hakuna madawati unawapa ahadi ya kuwapatia computer si bure kuna tatizo mahali mtu mzima kuwa hivyo...:pound::pound::pound:
 
Watoto waliokaa chini wanaandika utafikiri wanasujudu vile....ama kweli kua uyaone. Na hizo laptop zakuwekwa sakafusini kwenye vumbi na zisizotumia umeme zimebuniwa lini ? maana shule nyingi hazina hata umeme...ama kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya JK.
 
Back
Top Bottom