Mr handsome, hadithi ya kusisimua

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2022
17,796
32,148
HANDSOME BOYS...

SONGA NAYO...........

"Maisha yangu yamekuwa ya mapito mateso na furaha pia, vyote vimekuwa vikichukua nafasi katika maisha yangu na kunifanya niwe imara na kuwa na furaha za kuwa mpambanaji Zaidi katika maisha yangu, ukiwageni umeishi maisha ya vipindi tofauti tofauti yaani Leo uzuni kesho furaha hayo tunasema Ni maisha.

Kwa majina naitwa Edna nyerere mtoto wa pekee kabisa kwa mama yangu na baba yangu, Mungu aliwajaalia mtoto mmoja tu, lakini pia akatupatia maisha ya kawaida mno sio matajili, lakini pia alitufungulia njia ya kipato kidogo ambacho kilikuwa kikikidhi maitaji yetu madogo madogo, nakumbuka wimbo mkubwa kwa mama yangu ilikuwa Ni Edna soma sana hauna urithi, nimekuwa na malezi ya upande mmoja baada ya baba yangu kufariki nikiwa darasa la nne, lakini hiyo haikuwa sababu ya mama kukata tamaa kwasababu aliamini kuwa Mimi Niko upande wake, lakini pia hakuitaji Tena kuolewa au kuanzisha mahusiano mengine mama alikuwa allimpenda Sana baba angu.

Nakumbuka ilikuwa 2019 matokea ya kidoto Cha sita yalipotoka, nilikuwa jikoni nikipika mama akaja na kunikumbatia kwa nyuma uku machozi yakimtoka sana niliogopa niliwaza mama amepatwa na nini, niligeuka haraka na kumuuliza

"Kuna Nini mbona unanitisha ..??"

"Silii kwa uzuni nalia kwa furaha Edna hiko kichwa Ni Cha baba yako kabisa ingawa alifariki na elimu yake bila kupata kazi lakini naimani wewe utashika Hadi nafasi zake, hongera sana mwanangu umefauru kwenda chuo kikuu Tena kwa ufahuru mzuri kabisa "

Nyie nilikuwa na akili flani hivi ya kijinga yaani akili yangu ilikuwa Moto Sana sikumkumbatia mama Wala Nini nilitoka nje nikiwa napiga kelele Kama nimechangayikiwa, mbele ya nyumba yetu Kuna kiwanja kikubwa tu kina michanga ya kutosha SI unajua Tena jiji la dar kwa michanga, nilitoka nje na kuanza kuruka ruka nikipiga kelele nikalala chini na kugalagala uku na uku sikujali ya kuwa nachafuka au laah! Nilikuwa na furaha ambayo aielezeki, uswazi Ni uswazi tu watu walijaa na kuanza kunishangaa nikigalagala kila mtu aliongea lake

"Au amepandisha mashetani maana huyu mtoto nae"

"Amechanganyikiwa au??"

Kila mtu alisema analolijua sikuwa nikiwasikiliza mie nikabaki kushangilia ushindi wangu.

Mama akatoka ndani haraka akaona Sasa nataka kuwa chizi maana sio kwa ushangiliaji ule

"Haya inatosha amka hapo"

Nilistuka hatari na kuinuka, nilipokuwa nagalagala pale chini sikuwa nikiwaona vizuri Nyie nilipoinuka walikuwa wengi niliona aibu ya hatari nikainuka na kurudi ndani haraka, nikaingia bafuni na kuoga, Kisha kurudi jikoni.

Siku ziliendelea kusonga huku nikiqgaikia Mambo ya mikopo kwaajili ya chuo, na kwakuwa nilisoma ST. KAYUMBA kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato Cha sita ilinisaidia sana kupata mkopo, na nilifanikiwa kuchaguliwa kwenye chup kikuu Cha dar es salaam yaani UDSM furaha ikangezeka nilikuwa nakitaka Sana hiko chuo nilikuwa na wenge la kuanza chuo tu.

Mama alikuwa ameifadhi pesa zake akanipatia nikafanye shopping ya nguo Kama mjuavyo kile chuo kwa mavazi kama wako kwenye mashindano, nikafanya shopping yangu uchwara pale ya kawaida kwani haikuwa pesa kubwa Sana hivyo nyingi zilikuwa za mtumba, nilichojali kuwa Ni nguo mpya na pesa nimepewa na mama yangu.

Siku ya kuanza chuo iliwadia ilikuwa ni siku ya usajili kila mtu alikuwa mwenyewe isipokuwa Mimi ambaye nilikuja na mama yangu maana mama alitoa ahadi kuwa siku yangu ya kwanza chuoni lazima atanipeleka, mwanzo wanafunzi wengine walijua kuwa mama Ni mwanafunzi SI unajua elimu aina mwisho, lakini walipokuja kujua kuwa Ni mama yangu amenileta walicheka sana na kisema kuwa Mimi Ni mtoto wa mama, nilijisikia vibaya lakini mama alikuwa pale na kunifanya nione kuwa ni Mambo ya kawaida Sana niwaache waongee tu.

Usajili ulikamilika na kulikuwa na wiki Moja ya orientation, baada ya wiki hiyo kuisha rasmi tukaingia kwenye masomo, kwakuwa nilikuwa nikijua darada langu Ni lipi haikunipa shida Moja kwa Moja nikaingia kwenye darasa langu, nilikutana na watu tofauti tofauti wamependeza na wengi walionekana kuwa na maisha mazuri, niliingia nakukaa
 
zangu mbele kabisa Kama nilivyozoea, kila mwalimu alikuwa akiingia na kutaja topic zake za somo na kutoa kazi ya kufanya na kuondoka akisema tukipime kabla masomo ayajaanza rasmi, hapo ndo nilianza kujua uongo wa waliokuwa wakisema kuwa chuo Ni bata.

Nilipata shida Sana kuelewa Mambo ya chuo nilikuwa mpole Sana kila mtu alikuwa na rafiki yake isipokuwa Mimi nilikuwa pekee yangu muda mwingi nilionekana mnyonge Sana lakini sikujali simu yangu ilikuwa rafiki yangu ukizingatia na free WiFi iliyopo chuoni kila kitu Ni bambam.

Nikiwa nimekaa kantini nakula alikujq msichana mzuri tu alikuwa mweupe Sana mwili wake simple, ufupi alivutia Sana

"Samahani naweza kukaa hapa....??"

Aliniuliza msichana huyo ambapo ilikuwa ndo Mara ya kwanza Kuonana

"Yaaah karibu "

Nilimkaribisha akakaa kwenye kiti kilichopo mbele yangu

"Am theresia sijui unaitwa Nani ??"

Alijitambulisha

"Niite Edna"

Nilijibu na kuendelea na msosi

"Aaah me nimwanafunzi mpya kwenye darasa lenu nimechelewa kuanza chuo lakini nimekukalili ulikaa mbele kabisa "

"Oooh kumbe na wewe unasomea Sheria ??"

"Ndio"

Basi tulipiga story nyingi sana nami nikapata rafiki wa kuwa nae karibu.

Nakumbuka ilikuwa siku ya ijumaa nilikuwa na kipindi Cha mchana, nilifika kwa kuchelewa na lecture alikuwa ameshaanza kufundisha, niliingia na kuomba samahani kasheshee likaja nilipokuwa nikikaa kila siku nilikuta mkaka amekaa niliinama na kumnong'oneza

"Samahani uwa nakaa hapa naomba unipishe mbali sioni"

Aliinuka bila kuongea chochote.

Lecture ilipoisha rafiki yangu theresia akanifuata

"Unajuana na hawa mapacha wapya wa darasa letu....??'

" Mapacha gani nawe??"

"Si yule alikuwa amekaa kwenye kiti chako "

"Eeeh unafikili nilimuangalia usoni basi kwanza ndo najua Sasa hivi kwamba Kuna wanafunzi wapya "

"Hao waone jamani wazuri cheki wanavyofanana "

Nikageuza shingo yangu kuwaangalia hao wakaka wazuri uwiii walikuwa wazuri hatari midomo ya pink Kama wamepaka kitu vile, weupe wao, mavazi ya bei, nywele zao ndo usiseme kiukweli Kuna watu wazuri jamani niliganda nikiwaangalia tu.

Theresia ndo alichanganyikiwa kabisa akasogea karibu na kuwasalimia

"Mambo zenu??"

Walimuangalia Kisha wakajibu kwa sauti ya chini sana niliishia kuona midomo ikicheza lakini sikusikia sauti , Kisha wakampita na kuondoka , nikainuka kwenye dawati na kumfata theresia

"We nawe ndo shobo za aina gani hizo....??"

Nilimuuliza maana niliona Kama amejishusha sana

Lakini muda huo huo alirudi mmoja Kati ya wale wakaka na kunyoosha mkono akimpagoa theresia

"Am clevo........"

Theresia haraka akanyosha mkono na kujitambulisha

"Am sorry nimeambiwa nikufuate wewe kwaajili ya kazi za group no 7 "

"Ooooh kumbe upo group Moja na sisi anyway naomba namba zako nikuunge kwa group taarifa zote utakuwa ukizipata uko "

"Thanks......"

Alijibu na kutaka kuondoka, lakini gafla akarudi nyuma na kuniangalia Sana kisha akasema

" Ni yupo charming tu sio kwamba anajipendekeza "

Nilishangaa kumbe amesikia nilipokuwa nikimchamba theresia , nikabaki nikimuangalia Hadi alipokua akikata Kona gafla Nika.........

Nilishangaa kumn amesikia nilipokuwa nimimchamba theresiq nikabaki nikimuangalia Hadi alipokua akiiata Kona gafla nikashtushwa na theresia akisema tuondoke, Bado akili yangu ikimuwazia yule mkaka alivyonichana makavu nikajisemea kimoyo moyo

"Hunijui vizuri wewe nitakunyoosha "

Hao kila Mtu akashika njia yake na kuondoka, nilifika nyumbani na kumkuta mama akiwa anachambua mboga kwaajili ya chakula Cha jioni nilimsalimia na kuelekea chumbani kwangu.

Siku iliyofuata nilijiandaa na kwenda chuoni siku hiyo nilinyukw hatari yaani nilipendeza mpaka nilijijua kabisa nilipendeza, nilivunja kabati Kama naenda on date kumbe masomoni nilifika Tena kwa kuchelewa na Kama kawaida nilimkuta mmoja Kati ya wale wakaka mapacha akiwa amekaa kwenye siti yangu

"Samahani unaweza kunipisha....??'

"Umechanganyikiwa au ? "
 
Aliniuliza nikamtolea macho ya hasira hatari,.lakini haikusaidia kitu kwani hakutoka lecture alituangalia tunavyofanya fujo mwisho akasema

" Tokeni nje "

Niliitika haraka

"Nani Mimi ??"

"Wewe na mwenzio..."

Nikasema huu msala Sasa, nikagauka na kutoka nje, Kisha kijana yule akafatia nyuma sikujua kwamba ni clevo au mwenzie maana walifanana kila kitu nailikua sio rahisi kuwatofautisha aswaa sisi ambao ndio kwanza tumeonana, tulipofika nje akanifuata

"Kulikuwa na hajw gani ya drama zote zile ??"

Aliniuliza, nikimuangalia nakumjibu

"Umekaa sehemu yangu halafu unasema naanzisha drama "

"Nikukumbushe tu hapa Ni University na sio shule ya msingi au secondary kwamba Kama ni sehemu Ni yako mpaka unamaliza mwaka sawa, I didn't like that at all"

Hapo sura ilinishuka maana aliongea ukweli kabisa, Kisha akaondoka na kuniacha nikimuangalia tukaenda kukaa vimbwetani kila mtu alikaa kimbweta chake lakini tulikuwa tukionana, alionekana kuwa Ni kijana mtaratibu Sana na hapo nilijua kabisa huyu sio clevo Ni pacha wa clevo, baada ya muda mfupi clevo slikuja

"Na umekubali kutoka nje we una Nini atw kujitetea umeshindwa, kwanza Yuko wapi yule msichana ??"

Niliposikia ananitafuta nikaingia chini ya kimbweta ili asinione lakini yule yule pacha aliniona na akabaki akicheka, nikiwa chini ya kimbweta nimejificha, nikaunganisha mikoni yangu kwa kuomba msamaha na kumuonesha ishara asiseme kuwa Niko hapo chini alibaki akicheka tu

"Ebu nyamaza yaani baada unisaidie iumtafuta huyu msichana unacheka kama umetekenywa, anyway twende tukale "

Wakainuka na kuondoka hapo niliinuka kwa pupa na kujikuta nikijigonga, niliumia nikabaki nikiangalia uku na uku Kama Kuna mtu ameniona, nikatoka eneo ilo nikiwa na wenge Sana nikimtafuta theresia, nikiwa naangalia uku na uku ilikuja gari kwa Kasi Sana na kutua miguuni kwangu ikiwa inapoga honi nikaanguka chini, watu wakajaa wakiangalia niliinuka haraka kwa kuwa sikuwa nimeumia na kwenda kwenye kioo Cha Gari hiyo upande wa dereva

"Unaendesha gari kama uko kwenye mashindano ungenigonga hapo na ulivyokuwa na dharau hata kushuka umeshindwa SI ndio?? Sijui watu matajili mnashida gani "

Muda huo huo kioo kilishushwa kwanza nilipata mshtuko wa Hali ya juu jamani alikuwa mkaka mmoja hivi mzuri mwili ukionekana kabisa Ni wa gym akuwa mweupe Sana ila Ni mweupe alikuwa mzuri Sana nikabaki nikimuangalia

"Lakini sijakugonga na haujaumia "

Alijibu kwa utaratibu na sauti yake nzito kabisa nilihisi kuzimia, nikabaki nikiwa nimemkodolea macho tu

"Infact unatakiwa uwe muangalifu unatembea kama unamiliki hi barabara na ulivyokuwa hauna aibu unapata na nguvu ya kunifokea, whatch out girl"

Alizungumza hivyo kisha akafunga kioo Cha gari yake na kuondoka, kila mtu alibaki akiniangalia Mimi niliona aibu ya hatari maana maneno nishapewa na mtu kaondoka nimebaki Kama sanamu pale watu wakinicheka tu.

Niliona kuwa Ni siku mbaya Sana kwangu , niliwasha data na kuingia mdatandaoni Kisha nikatuma ujumbe kwa group kuwa siko sawa hivyo sitakuwepo kwenye group discussion, siku hiyo niliondoka nyumbani mapema Sana Wala sikutaka kupoteza muda chuoni, nilifika nyumbani hata mama alishangaa lakini alipouliza nilimwambia kuwa sijisikii vizuri

Nilishinda ndani siku nzima nikichezea simu yangu kwa kusoma simulizi ya MZIMU WA HUSINA.

Siku iliyofuata kwakuwa ilikuwa weekend hivyo sikuwa na haja ya kwenda chuoni niliamua kubaki nyumbani tu, muda huo huo nilipokea ujumbe kutoka kwa theresia kuwa wanagroup wanataka kuja nyumbani kuniona na kufanya discussion kwakuwa sikushiriki siku iliyopita, sikuwa na hiyana niliwakaribisha na kumpa taarifa mama

Nikaandaa chakula na kufanya usafi vizuri Sana sikutaka aibu maana kwetu hatuna pesa tuna makochi ya kizamani lakini muda wote kulikuwa vizuri tv yetu ilikuwa ya chogo, sikuwaza vyote hivyo nilichokuwa nikijali Ni wao kufika nyumbani kwetu tu.

Baada ya muda, lilipaki Noah Moja nzuri Sana nje ya nyumba yetu, nilibaki nikishangaa tu kupitia dirishani nilitoka nje haraka baadaya kuona theresia ndio alikuwa dereva wa Gari hiyo

"Waooooo, waooooh na kuendesha gari unajua"
 
zangu mbele kabisa Kama nilivyozoea, kila mwalimu alikuwa akiingia na kutaja topic zake za somo na kutoa kazi ya kufanya na kuondoka akisema tukipime kabla masomo ayajaanza rasmi, hapo ndo nilianza kujua uongo wa waliokuwa wakisema kuwa chuo Ni bata.

Nilipata shida Sana kuelewa Mambo ya chuo nilikuwa mpole Sana kila mtu alikuwa na rafiki yake isipokuwa Mimi nilikuwa pekee yangu muda mwingi nilionekana mnyonge Sana lakini sikujali simu yangu ilikuwa rafiki yangu ukizingatia na free WiFi iliyopo chuoni kila kitu Ni bambam.

Nikiwa nimekaa kantini nakula alikujq msichana mzuri tu alikuwa mweupe Sana mwili wake simple, ufupi alivutia Sana

"Samahani naweza kukaa hapa....??"

Aliniuliza msichana huyo ambapo ilikuwa ndo Mara ya kwanza Kuonana

"Yaaah karibu "

Nilimkaribisha akakaa kwenye kiti kilichopo mbele yangu

"Am theresia sijui unaitwa Nani ??"

Alijitambulisha

"Niite Edna"

Nilijibu na kuendelea na msosi

"Aaah me nimwanafunzi mpya kwenye darasa lenu nimechelewa kuanza chuo lakini nimekukalili ulikaa mbele kabisa "

"Oooh kumbe na wewe unasomea Sheria ??"

"Ndio"

Basi tulipiga story nyingi sana nami nikapata rafiki wa kuwa nae karibu.

Nakumbuka ilikuwa siku ya ijumaa nilikuwa na kipindi Cha mchana, nilifika kwa kuchelewa na lecture alikuwa ameshaanza kufundisha, niliingia na kuomba samahani kasheshee likaja nilipokuwa nikikaa kila siku nilikuta mkaka amekaa niliinama na kumnong'oneza

"Samahani uwa nakaa hapa naomba unipishe mbali sioni"

Aliinuka bila kuongea chochote.

Lecture ilipoisha rafiki yangu theresia akanifuata

"Unajuana na hawa mapacha wapya wa darasa letu....??'

" Mapacha gani nawe??"

"Si yule alikuwa amekaa kwenye kiti chako "

"Eeeh unafikili nilimuangalia usoni basi kwanza ndo najua Sasa hivi kwamba Kuna wanafunzi wapya "

"Hao waone jamani wazuri cheki wanavyofanana "

Nikageuza shingo yangu kuwaangalia hao wakaka wazuri uwiii walikuwa wazuri hatari midomo ya pink Kama wamepaka kitu vile, weupe wao, mavazi ya bei, nywele zao ndo usiseme kiukweli Kuna watu wazuri jamani niliganda nikiwaangalia tu.

Theresia ndo alichanganyikiwa kabisa akasogea karibu na kuwasalimia

"Mambo zenu??"

Walimuangalia Kisha wakajibu kwa sauti ya chini sana niliishia kuona midomo ikicheza lakini sikusikia sauti , Kisha wakampita na kuondoka , nikainuka kwenye dawati na kumfata theresia

"We nawe ndo shobo za aina gani hizo....??"

Nilimuuliza maana niliona Kama amejishusha sana

Lakini muda huo huo alirudi mmoja Kati ya wale wakaka na kunyoosha mkono akimpagoa theresia

"Am clevo........"

Theresia haraka akanyosha mkono na kujitambulisha

"Am sorry nimeambiwa nikufuate wewe kwaajili ya kazi za group no 7 "

"Ooooh kumbe upo group Moja na sisi anyway naomba namba zako nikuunge kwa group taarifa zote utakuwa ukizipata uko "

"Thanks......"

Alijibu na kutaka kuondoka, lakini gafla akarudi nyuma na kuniangalia Sana kisha akasema

" Ni yupo charming tu sio kwamba anajipendekeza "

Nilishangaa kumbe amesikia nilipokuwa nikimchamba theresia , nikabaki nikimuangalia Hadi alipokua akikata Kona gafla Nika.........

Nilishangaa kumn amesikia nilipokuwa nimimchamba theresiq nikabaki nikimuangalia Hadi alipokua akiiata Kona gafla nikashtushwa na theresia akisema tuondoke, Bado akili yangu ikimuwazia yule mkaka alivyonichana makavu nikajisemea kimoyo moyo

"Hunijui vizuri wewe nitakunyoosha "

Hao kila Mtu akashika njia yake na kuondoka, nilifika nyumbani na kumkuta mama akiwa anachambua mboga kwaajili ya chakula Cha jioni nilimsalimia na kuelekea chumbani kwangu.

Siku iliyofuata nilijiandaa na kwenda chuoni siku hiyo nilinyukw hatari yaani nilipendeza mpaka nilijijua kabisa nilipendeza, nilivunja kabati Kama naenda on date kumbe masomoni nilifika Tena kwa kuchelewa na Kama kawaida nilimkuta mmoja Kati ya wale wakaka mapacha akiwa amekaa kwenye siti yangu

"Samahani unaweza kunipisha....??'

"Umechanganyikiwa au ? "
Will b back
 
Nilizungumza hivyo tu baada ya kutoka nje

"Utatukaribisha au utaanza kuzungumzia kuhusu magari ??"

"Nikawakaribisha na wengine wakaanza kushuka kwenye gari, nilistuka baada ya kumuona clevo anashuka kwenye gari, aliningalia tu lakini hakusema chochote

"Karibuni Sana jisikieni mko nyumbani "

Moja kwa moja niliwapeleka sebleni kwani niliwaandalia sehemu nzuri tu nilitengeneza kwaajili yao, ila uwepo wa clevo ulinifanya niwe na wasiwasi sana, basi baada ya muda niliwapatia juice ambayo nilitengeneza na kuwapa chakula, kila mtu alikula isipokuwa clevo ambaye Alisema kuwa juice inamtosha.

Baada ya muda tukaanza discussion kwa utambulisho kila mtu alitaja jina lake na miaka yake na shule aliyomaliza, yaani katika wote wale Mimi na kijana aliyekuwa akijulikana Kama Ismail ndio tulikuwa tunatoka shule za ST. KAYUMBA ila clevo ndio alikuwa ametoka shule Moja nzuri Sana hapa dar es salaam na shule yenye ada ya juu shule yenyewe kwanza hawakuwa wakivaa nguo za shule walikuwa wanavaa kawaida kabisa yaani mavazi yoyote.

Tulimaliza kazi zetu Kisha tukakaa tukiangalia movie ambayo niliiweka ikienda kwa jina na the rising ilikuwa Ni favorite movie.

Baada ya muda simu ya clevo iliita kwakuwa tuliweka sauti kubwa ya TV akatoka nje kwaajili ya kuzungumza nami nikamfuata nje.

Alipomaliza kuzungumza na simu nikamuomba tuongee

"Najua hatuna ukaribu kihivyo ata Kama tuko group moja, nikuombe tusahau yaliyopita maana nasikia Jana ulikuwa ukinitafuta kwa hasira sana, muda huo huo ilikuja gari Moja nzuri Kali hatari kushinda ile ambayo alikuja nayo theresia, vioo vikashushwa Kisha pacha wa clevo akatoa kichwa nje

"Yoooh ma niggah tuon.........."

Kabla ajamaliza akashtuka kuniona Niko na clevo akashuka haraka na kuja kunipa mkono akiwa na furaha Sana mpaka nikashangaa

"Miss ma drama uku tena na kaka angu mnafanya Nini ? Clevo SI ulisema unaenda group discussion.?"

Aliongea maneno mengi kwa wakati mmoja akiwa amenishika Mkono

"Unafikili nafanya Nini huku, anyway Ni hivi nilipewa taarifa kuwa tunafanya discussion kwa kina Edna but I didn't know that she's the one "

Wakabaki akichekeana nilipata muda wa kuwaangalia yani walifanana kila kitu Hadi tabasamu zao nilichokigundua clevo alikua na dimpo upande mmoja lakini yule mwingine alikuwanayo pande zote mbili yaani niliganda kabisa kuwaangalia nikiwa nimeachia mdomo.

Muda huo huo theresia akatoka nje akiwa anaongea

"Wenzetu mnafanya Nini mpaka mmetutelekeza uku ndani"

Baada ya theresia kutoka nje niliona Gari ile nyingine ikifunguliwa na mtu akaita theresia , sikuamini kumuona mkaka ambaye alitaka kunigonga chuoni akishuka kwenye gari ya kina clevo nilihisi kuchaganyikiwa tu nilibaki nimeganda

"Oooh Skyler, my God tumeonana Tena ??"

Alizungumza theresia na kumsogelea mkaka huyo ambaye nilipata kujua kuwa Anaitwa Skyler na wakakumbatiana, nilimsikia clevo akisema

"Waooooh celvin this is amazing wapige picha "

Hapo nikajua kumbe pacha wa clevo anaitwa Calvin......

ITAENDELEA....

HANDSOME BOYS....
SEHEMU YA: 03

SONGA NAYO............

Theresia na mkaka huyo ambaye nilitokea kumuogopa Sana aliyekuwa akiitwa Skyler waliendelea kukumbatiana uku Calvin akiwapiga picha , mwisho wakaachiana na kuanza kujuliana hali, nilisimama pembeni nikiwa naangalia tu nilikuwa mwenyeji lakini Mimi ndio nilionekana kama mgeni vile.

"Mnajuanana huyu....??"

Aliuliza clevo

"Ywaah nilikutana nae wiki mbili nyuma alinisaidia taili Moja la gari "

Alijibu Skyler nilibaki nilishangaa tu walikuwa wamekutana watu wenye pesa tu maana Mimi hata baiskel sikuwai kumiliki

"Basi mkaribie ndani jamani "

Niliona niwakaribishe ndani kuliko kuwaacha nje wakiwa wamesimama, Skyler alimuangalia Calvin ambaye alinigeukia na kunijibu

"No it's okay kwakuwa mmemaliza kila kitu tunaondoka tulimpitia huyu kijana tu uwe na jioni njema"

Kisha wakapanda Gari lao na kuondoka, theresia alionekana kuvutiwa Sana na wale watu yaani

" Ila nyie Hawa wazuri jamani uwiiii"

Alizungumza theresia na kunifanya nicheke tu, nikauliza

"Kwani Hawa Ni ndugu ??
 
" Shoga angu acha tu nimewajua muda mfupi Sana lakini hatari na nusu subili tuagane na hao wazungu watu nikupe mchongo mzima"

Baada ya muda wote waliondoka nikabaki na theresia tukakaa ndani ya gari yake na kuanza kupeana umbea

" Yule ambaye nilikuwa nimekumbatiana nae anaitwa Skyler , ndo Kaka yao mkubwa kabisa, me nimejua juzi tu baada ya Skyler kuwaweka status nikamuuliza akasema Ni wadogo zake "

Nikabaki nikijisemea kimoyo moyo tu

"Kuna watu wamebarikiwa Sana jamani "

Masomo yaliendelea, na nilikuwa bize Sana na masomo yangu kidogo kidogo nilianza kuzoeana na Calvin ambaye ndio alikuwa Mdogo Kati ya wote, Skyler alikuwa akisoma chuo hiko hiko course ya udaktari lakini ilikuwa sio rahisi kuonana nae na alikuwa mwaka wa pili na wadogo zake walikuwa mwaka wa kwanza course ya Sheria kama Mimi

"So Edna una plan gani weekend hi baada ya kumaliza test....??

Aliniuliza Calvin

"Sina plan yoyote Zaidi nitakuwa nyumbani na mama yangu "

"Huwa haupendi kutoka na marafiki mkainjoy uko ??"

"Noooh napenda napia mama amekuwa akinisisitiza Sana niwe natoka lakini nimeshindwa sio kuwa sitaki lakini matumizi ya pesa yanakuwa makubwa ukizingatia mama ndio baba kwangu hivyo kila kitu Ni juu yake namuonea huruma "

"Oooh naelewa how about this nikufuate uje nyumbani tutakuwa na birthday party ya mama, hautatumia hata 100 nitakurudisha pia "

Muda huo huo nilitokea Gari na kusimama mbele yetu kioo kikashushwa na hakuwa mwingine Bali Ni Skyler

"Can we go...??"

Alimuuliza Calvin ambaye aliniaga na kuondoka lakini sky aliniangalia kwa jicho la hasira sana.

Siku ya jumamos ilipowadia majila ya saa 12 jioni nilijiandaa na Calvin alikuwa nyumbani Kisha tukaondoka, tulifika kweny jumba kubwa na Kali kabisa la kifahari picha linaanza alifungua geti kwa remote ndogo aliyokuwa nayo, tulipoingia nilikutana na bustani nzuri sana ya maua, SEHEMU nzuri ya kupaki magari lakini pia kulikuwa na swimming pool kubwa na nzuri Sana nilibaki nikishangaa tu uku na uku, Calvin aligundua kuwa nimevutiwa na mazingira hayo akaniambia

" Shuka uyatizame kwa karibu "

Nikajichekesha tu mwisho nikashuka na kuanza kuangalia uku nauku

"Aiseee Ni pazuri Sana Mungu wa ajabu Sana hongereni mno "

Ingawa kulikua na party yakukua na kelele yoyote ile ya mziki au watu kusikika ikanibidi niulizie

"Mbona Kama hamna mtu ??"

" Oooh wapo wanajisubili Mimi tu "

Basi Moja kwa Moja tukaingia ndani kulikuwa na seble Moja matata nzuri iliyojitosheleza ilinukia vizuri sana, Skyler baada ya kuniona akaja mbele yangu lakini Calvin pia akaja mbele yangu akinikingia kifua

"Hi ni party ya familia kwanini huyu Yuko hapa....??"

"Unafikili Kuna hajaya Mimi kukujibu ? Huyu Ni rafiki yangu hivyo Ni Kama familia "

"Calvin......."

Alifoka Skyler alionekana kuwa na hasira Sana, nikaona huu msala Bora niondoke kumbe Ni family party

"Calvin tutaonana jumatatu chuoni"

Nikageuka na kutaka kuondoka lakini ilisikika sauti ya mwanamke ikisema

" Karibu mgeni "

Niligeuka na kuangalia nyuma nilimuona mama mtu mzima tu akishuka ngazi akiwa amependeza Sana Moja kwa Moja nikajua kuwa huyu Ni mama yao niliogopa Sana nikabaki nikitetemeka Kama Kuna kosa nimefanya

"Calvin unaiponza "

Niliongea kipolepole Calvin alicheka sana, Skyler akiondoka na kupanda ngazi kwa hasira Sana nikajisemea kimoyo moyo

"We mjinga wewe siku yako ipo kumbe umjui Edna Ni Nani eeh nitakunyoosha mbuzi wewe "

Hapo nilikuwa na hasira Sana yaani sema sikuweza kuzionesha mbele za watu, kiukweli mama yao alionekana kuwa mwanamke mmoja mcheshi Sana yaani ambaye anajali utu, tulisalimiana Kisha akanikaribisha kwa furaha zote.

Muda wa kukata keki ulifika tukaata keki jan alionekana kumpenda Sana mama yao, nae aliishi nao Kama rafiki zake aliwapenda Sana niliona upendo kati yao na mama yao hata wao walipendana Sana sema Ni mikwaruzano ya kawaida ambayo uwa inatokea katika familia.

Wakawa bize kupiga picha nami nikapata wasaa wa kuangalia nyumba kwa makini, na mama yao ndio alikuwa akinitembeza kila Kona alinipeleka vyumbani kwao walahi Kuna watu wanalala pazuri jamani kulikuwa panavutia Sana
 
"Kama unavyoona kila mtu anachumba chake lakini hawataki kabisa kutengana wameamua kulala chumba kimoja na uwa wanatumia hiki chumba "

Alinielezea mama yao

Ilifika wakati tukaenda kukaa kwenye meza ya Chakula, yule mama ananiuliza

"Nini kinaendelea Kati yako na Calvin maana hakuwai kuwa na rafiki wa kike tangu utotoni "

Swali lilinichanganya nakunifanya nipaliwe na juice niliyokuwa nakunywa

"Oooh pole pole "


Nikajichekesha pale na kujibu

"Aaah Ni rafiki yangu, naweza Seema pia Ni kama Kaka kwangu "

"Vizuri me nafurahi nikiona wanangu wanafuraha hivyo Ni kila la kheri kwenu "

Nikaona huyu mama analeta habari sio kabisa

"Unajua Nini katika wanangu ambao Ni wachangamfu Sana Sana kuliko wote basi Ni Skyler Ni mtu mmoja mcheshi Sana Kama baba yake lakini Kuna Mambo yametokea mwezi ulioisha unamfanya awe hivyo"

"Oooh kumbe "

Niliitikia kawaida kabisa maana katika watu ambao niliwwogopa Basi ni Skyler maana tangu nimekutana nae Ni mtu wa kunipigia mikwala tu na kunitisha

"Skyler alitakiwa kuoa mwezi wa kwanza lakini siku ambayo alikuwa akimvisha Pete mchumba wake akimfumania na rafiki yake kwenye chumba Cha make up hiyo imepelekea Skyler kueachukia wanawake wote isipokuwa Mimi ambaye Ni mama yake mpe muda atakueleewa na atakuchangamkia"

" Na huyu clevo je??"

"Ahahah huyo Ni mbabe wa familia"

Alijibu mama huyo na kuanza kucheka hapo nilikubali maana clevo ni kauzu jamani mkiwa kwenye group discussion ataki ata zile story za kupoteza muda.

Wakati huo huo alikuja Skyler nilibaki nikimuangalia na kumuonea huruma Sana nilimuangalia Sana mpaka akajishtukia akawa anajiangalia vizuri mwilini mwake , mwisho akamwambia mama yake

"Mlikuwa mkiniongelea ??"

"Oooh no kwanini tukuongelee "

"Anyway mom I.........."

Aliongea kwa sauti ya chini Sana yenye uzuni nilipata wasiwasi na kutaka kujua Nini kinaendelea........

ITAENDELEA.....

FULL IPO NICHEKI

HANDSOME BOYS......


SEHEMU YA : 04

SONGA NAYO..........

"anyway mom I .........
"

Aliongea kwa sauti ya chini Sana yenye uzuni nilipata wasiwasi na kutaka kujua Nini kinaendelea, nilikaa vizuri kwa kutaka kujua hata mama yake alipata wasiwasi na kuinuka

"Shida Nini mbona Kama hauko sawa ??"

" I have to go mom naomba unisaidie nipate ndege ya asubuhi Sana "

"Ndege kwenda wapi ?? Kufanya Nini mbona unaniweka roho juu jamani...??"

"Silver amenipigia simu hapa analia Sana anasema baba amefariki "

Alizungumza hivyo na kukaa chini uku akilia sana, mwanamke Kama unavyojua alikaa chini na kuanza kulia, nilimuonea huruma Sana Skyler nilimsogelea na kumshika kwa nyuma nikimtuliza, nashukuru Mungu akuwa na hasira Zaidi alilalia bega langu na kupooza machungu yake.

Baada ya muda mama yake alianza kuangaikia tiketi mbili za ndege, niliona Ni kiasi gani walikuwa wakipendana Calvin na clevo walikuwa bize wakimsaidia mwenzao kupaki vitu , na ndipo nilipojua kuwa walizaliwa baba tofauti Calvin na clevo baba yao alikuwa nni mzungu na Skyler baba yake alikuwa Ni mkorea nilibaki njia panda nilitaka kujua ilikuwaje huyu mama akapata wanaume Hawa Tena wenye pesa sana.

Mpaka saa 6 kasoro usiku kila kitu kilikuwa kimetimia, mama alikuwa akinipigia sanasimu lakini sikuweza kuisikia kwani nikiweka kwenye pochi na ilikuwa haina sauti, niliwasaidia sana katika maandalizi ya Safari yao.

Skyler alionekana kachanganyikiwa sana alionesha jinsi gani anampenda baba yake

" Hakikisha passport yako iko karibu "

Alizungumza mama yao na kina Calvin akimkumbusha Skyler

"Yeah hope Edna ameiweka maana nilimwambia kuwa ipo kwenye droo yangu "

Hapo nikakumbuka kuwa sikuiweka, haraka nikapanda ngazi kuelekea chumbani kwao, niliikuta passport kwenye droo nilitoa na kutaka kuweka kwenye bag hapo nikapata muda wa kusoma alikuwa akiitwa SKYLEY LEE TAEQUANG nikishindwa kusoma hata Hilo jina lenyewe nikatoka nje kwa mwendo wa haraka, nikiteleza kwenye ngazi kama mzigo kila mtu alishtuka kwa kuita jina langu

"Edna....."

Skyler alikuwa wa kwanza kuinuka kitini na kuja kuniinua hapo nikaamini maneno ya mama yake, niliumia kidogo tu kwenye mguu, Calvin alikuwa akicheka tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom