Mpya! Kuuza pilau nyumba za ibada

Wewe utakuwa ni mgeni wa kuswalia misikitini, hasa misikiti ya Dar,watu wanafanya biashara zao kama kawaida na hakuna shida,kufanya biashara ndani ya msikiti ndio vibaya....japo kuwa wale masheikh wauza madawa huwa wanazitangaza dawa zao pale mimbari kwa imamu halafu pesa wanaenda kupokelea nje...utakuwa umesalia msikiti wa kwa msusa mbagala rangi tatu kuna jamaa huwa anauza pilau la take away kwa buku anakupa na kijiko cha plastiki au nasema uongo ndugu yangu?Tuliza jazba sheikh hiyo ni kawaida jamaa huwa anauwa soko la mama lishe wanaouza pilau buku jero...mimi mwenyewe nilikuwa nikitoka msikiini napitia kabox kangu naenda kupoza njaa,tuvumiliane mkuu.
Ustadh GIRITA kweli leo tuliswali pamoja Msikiti wa Kwamsusa Mbagala Rangi Tatu(mimi mgeni) kwangu mimi ni mara ya kwanza ya kuona tukio kama lile ila biashara naziona tu za kofia, kanzu, tende' madawa hata Sharbeti ya KHASUS ila Ubwawa! tena naona kuwaharibia mamantilie biashara yao, ni batili kabisa
 
Mbona tende huwa zinauzwa na dawa pia za asili huwa zinauzwa hapo? Iweje pilau ? Acha wajasiriamali wafanye biashara!
Tende ni tunda takatifu na tena imebarikiwa kulioko matunda yote' kuuzwa msikitini ruksa! Sio ubwabwa
 
Naona mapovu yameanza,kuna waliotegemea uzi utahusu makanisa
Hapa a mm alivyosema PILAU nikawaza vingine kabisa nikazama fasta kujua hilo pilau lilikuwa kwa mfumo upi DVD au kwa FLASHDISK
sasa hapo sijaona la kushangaza
na hii Inaonesha waislam ni namna gani tunapenda kutafuta RIDHIKI ya halali
Bila ujanja ujanja
Sasa kilichokushangaza nini hapo mbna kawaida hiyo
 
Mbagala kuna kuna shida gani?,huu ushamba wa mji unawasumbua sana.
Wewe Mbagala unaijua au unaisikia? Kwa taarifa yako, Mbagala usiifikiri ile ya alioiimba DIAMONDI (mbele jalala) sasa hivi kumekucha ile mbya!
 
Wewe Mbagala unaijua au unaisikia? Kwa taarifa yako, Mbagala usiifikiri ile ya alioiimba DIAMONDI (mbele jalala) sasa hivi kumekucha ile mbya!
Mimi nimemuuliza jamaa mmoja huko juu kuiponda Mbagala.
 
Back
Top Bottom