GE2025 Mpina na Kalikawe ni wagombea urais kupitia Act Wazalendo

GE2025 Mpina na Kalikawe ni wagombea urais kupitia Act Wazalendo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
1754462766579.jpeg

Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza rasmi majina ya wagombea wa nafasi za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, kufuatia kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika tarehe 5 Agosti 2025 katika ukumbi wa Hakainde Hichilema.

Katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya Chama ilijadili na kupitisha mapendekezo ya wagombea watakaowakilisha Act Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majina mawili yamependekezwa kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni Aaron Kalikawe na Luhaga Mpina.

Wagombea hawa wawili watawasilishwa kwa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama kwa ajili ya kupigiwa kura na mmoja wao atachaguliwa kuwa mgombea rasmi wa urais kupitia ACT Wazalendo.

1754458289142.png

1754458427914.png
 
Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza rasmi majina ya wagombea wa nafasi za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, kufuatia kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika tarehe 5 Agosti 2025 katika ukumbi wa Hakainde Hichilema.

Katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya Chama ilijadili na kupitisha mapendekezo ya wagombea watakaowakilisha @actwazalendo_official katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majina mawili yamependekezwa kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni Aaron Kalikawe na Luhaga Mpina.

Wagombea hawa wawili watawasilishwa kwa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama kwa ajili ya kupigiwa kura na mmoja wao atachaguliwa kuwa mgombea rasmi wa urais kupitia ACT Wazalendo.
Namcheka mpina kama mazuri vile
 
Hahahah CCM wamejua kutudharau sana.
Ww Moina huna akili kabisa unatuchukuliaje na baada ya OCt ushakufa kisiasa
 
Ila vyama vya upinzani vinayumba Sana. Mtu anajiunga Leo Kisha anapewa ugombea urais. Huu ni udhaifu mkubwa Sana.
Kwa level ya siasa za Tanzania ni kawaida kwababu vyema havifuati ideology au falisafa ya chama ni njia yakupata ubinge na umaarufu wa siasa.
 
GxpWrSpX0AEK5ee.jpeg
TAARIFA KWA UMMA
Halmashauri Kuu ya ACT Wazalendo imepitisha Wagombea Urais wa Tanzania na Urais wa Zanzibar.

Urais wa Tanzania yamepitishwa majina mawili. Aaron Kalikawe na Luhaga Mpina.

Urais wa Zanzibar aliyepitishwa ni Othman Masoud Othman.
 
Kumbe hakuna mwenye akili hivi so called vyama vya upinzani! Mpina, kweli utachaguliwa kuwa Rais? Kweli?

kama siyo ujinga , basi ni propaganda za CCM kupitia ACT.....
 
Back
Top Bottom