April 13, 2020
Mbarali , Mbeya
Simulizi za BABU Jason A. Halinga mwenye Miaka 100, Watoto 78 na Wake NANE,amezaliwa Februari 23,1920 huko mkoani Mbeya na kuonesha Kadi ya Mpiga Kura cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania asimulia.
Jason A. Halinga mwenye nywele za mtindo wa rasta ndefu mpaka kupita mabegani zenye mngao wa rangi nyeusi titii huku chembe chache sana za mvi nyeupe zikijitokezo sehemu chache mno ikiwa utamuangalia kwa makini. Mzee huyu anasemea hatumii mafuta ya kupaka mwilini wala kuogea sabuni.
Babu Jason Halinga anasema u-rastamani ni jadi yao ktk ukoo wenye masharti na hata wazee wake akiwemo babu yake aliyefariki akiwa na miaka 167 walikuwa na mtindo huo wa nywele za kusuka. Enzi hizo kulikuwepo pia chifu Malema aliyewashangaza waJerumani kwa kutengeneza mvua kipindi cha kiangazi mwezi Agosti.
Siri ya umri mrefu ni kula vyakula vyenye virutubisho vya asili kama maziwa, mtama, mahindi yasiyo nyunyuziwa madawa n.k Pia matunda pori na mizizi pori ilikuwa ni sehemu ya vyakula vilivyoliwa iwe wapo safarini mwituni au majumbani. Pia mafuta kidogo ya samli na elizeti hutumia.
Babu Halinga pia anashangaa watoto wa siku hizi kuumwa kiuno wakati enzi zao ukisema kiuno chauma unaishia kucharazwa bakora. Na ilikuwa mwiko kusema maana wazee nao waseme nini kuhusu maumivu ya viungo.
Swali kubwa ni Tume ya Uchaguzi ya Taifa imewezaje kumpatia Kadi ya Mpiga Kura kama utambulisho wake kuwa ni kikongwe wa miaka 100 wakati wajihi wake, utimamu wa kumbukumbu n.k ni tofauti na mwenye kadi hiyo.
Source : MbeyaYetuOnline TV