Leo nikiwa natokea Dodoma naelekea Tabora, nilipofika maeneo ya Four ways nikasimama ili nipate vichwa vya kupiga navyo story njiani
Mara katokea mpiga Debe na kuanza kumzuia kijana mmoja asipande gari yangu licha ya anapokwenda ndio njia ninayopita.
"Wewe kwanini upite shortcut kuja Kwa dereva, sasa hupandi hii gari napakia hawa wawili" alisikika mpiga Debe huyo.
Kuepuka mkosi safarini imenibidi niwabebe hawa wawili nimuache yule kijana lakini mke wangu ananilaumu Sana kuwapa umiliki wa gari wapiga debe.
Mke wangu ananilaumu njia nzima mpaka sina Amani ya moyo.
Nimenuniwa na ndoa yangu ipo hatarini