Mpenzi wangu hapokei simu wala kujibu sms zangu, Nifanye nini?

ps2 2014

Senior Member
Dec 23, 2014
108
120
Nina mpenzi ambaye naona kuna tatizo japo yeye hayuko wazi kunieleza ukweli.

Tatizo kubwa ni mawasiliano,ni kwamba mm siku zote namtafuta yeye,mara moja moja anapokea simu,mara nyingi hapokei,nikituma msg hajibu,inaweza pita miezi bila yeye kunipigia au kutuma sms hata kubip tu.

nikimuuliza kwa nn unafanya hivyo,anasema hajui sababu na anasema atajirekebisha lakini hakuna mabadiliko,nikaona ninamlazimisha mapenzi nikatoa wazo basi tuachane,maana si vizuri kumlazimisha kunipenda,yeye akasema nimsamehe atabadirika tu.

wakuu tabia haijabadirika mpaka sasa,na mawasiliano ktk mapenzi ni muhimu sana,nahisi hanipendi lakini hataki kuniambia tu,mm sijui nifanye nini?,nafsi inakuwa ngumu kubwaga manyanga kwa sababu ya sintofahamu ya msimamo wake kwangu,angeniambia tu kwamba hanihitaji,mm ningekung'uta mavumbi na kuendelea.

Mm ni mwanaume

msaada tafadhali,nifanye nn?
 
Yamekukuta kama yangu. Ila mimi ni 'ke. Inauma sana mtu asipokuwa muwazi. Napitia wakati mgumu sana asee. Ila nimeamua kupiga moyo konde, nisonge mbele. Huyo hakupendi braza. Yuko mwenzako anayependwa zaidi.
Ni kweli,nimemuuliza sana kwamba anataka tuachane,amekuwa akisema hapana,nikimuuliza kama ananipenda anasema ndiyo,lakini no mawasiliano,nikimuuliza kama kitu namkosea anasema hapana,nikimuuliza unaridhika na mahusiano yasiyokuwa na mawasiliano anasema hapana,kiufupi ananichanganya.nikimwambia nieleze ukweli ulio moyoni mwako,anasema huo ndio ukweli....nashukuru kwa ushauri wako na pole kwa yaliyokukuta.
 
Asante.
 
Inawezekana kuna mambo wewe mwenyewe ndio unamkwaza/ ulimkwaza na akaumia sana juu yako lakini pia kuna kumbukumbu nzuri sana ambayo mliwahi kushare pamoja.

Huyo mwanamke anakupenda na anatamani sana kuishi na wewe bila kukupoteza ila kuna tabia/ mambo unayoyafanya ambayo yanamuumiza moyo wake bila ya kukwambia inawezekana kutokana na upole wake/ mazingira/ historia yake au vile unavyoishi nae.

Kuwa biz na mambo yake sio mara zote amepata mwanaume mwingine inawezekana anaamini kukaa kimya na kukubali matokeo ndio njia sahihi kwa upande wake.

Kuishi katika mahusiano kunahitaji sana uvumilivu, mvumilie kwani kutafuta mwingine inawezekana ikawa pigo kubwa zaidi kwako.

Jenga tabia ya kumsaidia katika matatizo yake na kumpelekea zawadi
 
Nina mpenzi ambaye naona kuna tatizo japo yeye hayuko wazi kunieleza ukweli.

Tatizo kubwa ni mawasiliano,ni kwamba mm siku zote namtafuta yeye,mara moja moja anapokea simu,mara nyingi hapokei,nikituma msg hajibu,inaweza pita miezi bila yeye kunipigia au kutuma sms hata kubip tu.

nikimuuliza kwa nn unafanya hivyo,anasema hajui sababu na anasema atajirekebisha lakini hakuna mabadiliko,nikaona ninamlazimisha mapenzi nikatoa wazo basi tuachane,maana si vizuri kumlazimisha kunipenda,yeye akasema nimsamehe atabadirika tu.

wakuu tabia haijabadirika mpaka sasa,na mawasiliano ktk mapenzi ni muhimu sana,nahisi hanipendi lakini hataki kuniambia tu,mm sijui nifanye nini?,nafsi inakuwa ngumu kubwaga manyanga kwa sababu ya sintofahamu ya msimamo wake kwangu,angeniambia tu kwamba hanihitaji,mm ningekung'uta mavumbi na kuendelea.

Mm ni mwanaume

msaada tafadhali,nifanye nn?
Fanya vitu vingne
 
Back
Top Bottom