Nimeachwa na mpenzi wangu, nifanye nini niimudu hali hii?

sam green

Member
Feb 21, 2020
64
125
Habari wana JF

Hapa nimebakia njia panda muda huu leo baada ya kumpigia mpenzi wangu simu! Ambaye tulipendana saaana, siku za nyuma hapo tulikosana lakini tukapatana tena maisha yakasonga leo hii nimempigia simu ananijibu majibu ya mkato sana. Nikituma sms anajibu kwa mikato nikimuulza shida nini? Anasema hakuna mpaka nilipo mbona saaana akatamuka tu neno moja " naomba uniache " Nikamuulza kivipi anasema tuu nimuache hanipendi.

Tena nashindwa kumwelewa shida nini! Hapa nilipo na hasira natamani hata nikamuue lakini siwezi! Na kumuacha nashindwaaa kabisa naombeni ushauri nifanyeje katika hili?
 

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
1,652
2,000
Pole sana dogo.

Ulikua nae huyohuyo ama ulikua na mwingine pembeni, kama ulikua na mwingine basi ongeza mapenz kwa huyu mwingine.
Kama ndo alikua yeye pekee, piga moyo konde jitahidi kutomtafuta kabisa futa namba zake, taratibu tu utamsahau.
 

sayoo

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
4,362
2,000
Habar wana jf hapa nimebakia njia panda muda huu leo baada ya kumpgia mpenz wang simu ! Ambay tulpendana saaana , siku za nyuma hapo tulikosana lakn tukapatana tena maisha yakasonga leo hii nimempgia simu ananjibu majibu ya mkato sana . nkituma sms anajibu kwa mikato nikimuulza shida nn? Anasema hakuna mpka nlpo mbna saaana akatamuka tu neno moja " naomba uniache " nikamuulza kvp anasema tuu nimuache hanipndi. Tena nashindwa kumwelewa shida nini! Hapa nilipo na hasira nataman hata nikamuue lakn siweZ! Na kumuacha nashindwaaa kabisa naomben ushaur nifanyeje katika hili
Tafuta mwingine acha ufal.a , wapo wengi wanaotafuta wenza
 

sam green

Member
Feb 21, 2020
64
125
Pole sana dogo.

Ulikua nae huyohuyo ama ulikua na mwingine pembeni, kama ulikua na mwingine basi ongeza mapenz kwa huyu mwingine.
Kama ndo alikua yeye pekee, piga moyo konde jitahidi kutomtafuta kabisa futa namba zake, taratibu tu utamsahau.
Ndio huyo huyo sinaga tabia ya kuwa na wawili nikimpta mmoja huwa nabaki hapo hapo
 

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
1,652
2,000
Ndio huyo huyo sinaga tabia ya kuwa na wawili nikimpta mmoja huwa nabaki hapo hapo
Jitafakari mkuu, labda kuna mahali ulikosea kashindwa kuvumilia ama lah kapenda kwingine. Yote kwa yote kubali yaishe kuliko kumbembeleza zaidi arudi, kwasababu atarudi kwa kukuonea huruma na sio mapenzi tena.
 

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
302
1,000
kwanza kubali kuwa si wewe wa kwanza kuachwa, Obama na umaarufu wote wa kuwa rais wa kwanza mweusi alishawahi kuachwa na mpenz wake, kila mwanaume ameshawahi pitia hayo, sasa wote tungeua ingekuaje?

jipange upya, kula vizuri fanya mazoezi rekebisha mapungufu yako kama yapo, jifunze jinsi ya kuwa mwanaume gentleman kwa kusoma nyaraka mbalimbali, tafuta marafiki wa kike piga nao stories, siku ukiamua tafuta mwanamke ambae anakuvutia sana, utampata!
.
.
Hongera sana kwa kuachwa, na pole sana kwa unavyojisikia, japo hio ni hatua ya kwanza ya uanaume, imagine uoe sasa na hio hali halafu upate kashkash za ndoa si utaua wewe! relax kijana relax!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom