Mpatuka
JF-Expert Member
- Nov 15, 2015
- 1,711
- 2,494
Mimi ni kijana, mwenye kila sababu ya kuwa na mke kwa umri wangu, lakini kutokana na changamoto za kimaisha nimejikuta nachelewa mpaka muda huu nipo kwenye mahusiano tu. Nimepitia mahusino kadha wa kadha lakini kwa huyu binti niliyenaye sasa nahisi tunaweza kufikia lengo hasa lakuwa mwili mmoja, kilichonifanya kuanzisha uzi huu na kuhitaji maoni toka kwa wadau kwenye jukwaa hili ni mazingira ya mimi na huyu bibie.
Huyu binti yupo wizarani mkoa x kama data clerk na mm nipo mkoa x kama researcher. Anadai ananipenda sana nami niwe muwazi nampenda pia tena sana, changamoto ni yeye anadai kutokana na ugumu wa maisha hasa kwenye nyumba za kupanga amepata kijana mmoja anadai wachukue nyumba nzima waishi pamoja.
Huyo kijana kipindi cha nyuma alishawahi kumtaka kimapenzi na mimi nilishirikishwa na mpenzi wangu na sms nikaoneshwa. Baada ya kupokea taarifa hizo nikakataa kabisa kuwa mpango huo siyo salama kwa mapenzi yetu, lakini jambo la kushangaza huyu mpenzi wangu amesisitiza kuwa anajielewa na wala hakuna shida yoyote ile.
Nilipoonesha msimamo wangu kuwa sitaki hilo litokee ameninunia na amani hakuna mpaka muda huu. Hivyo basi naombeni ushauri wenu wadau nifanye uamuzi gani katika hili.