Mpenzi wangu ana singlet isiyo yangu

Mpenzi wangu ana singlet isiyo yangu

Mayunga6

Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
94
Reaction score
15
Yapata miezi minne (4) tangu nimejuana na mpenzi wangu,na mapenzi yemetukolea kweli kweli. Yeye ana makazi yake nami yangu. Huwa tunatembeleana week ends,ikiwa ni pamoja na kulala kabi. Kila tuwapo pamoja, mpenzi wangu hupenda kuvaa nguo zangu akidai anapenda harufu ya perfume yangu n.k. Week end iliyopita nililala kwake, niliamka mapema ili niwahi kupita nyumbani kwangu kuchukua baadhi ya vitu kwenda navyo ofisini,hivyo nikamuaga akiwa kitandani amelala. Nilipofika ofisini akaniambia kuwa nilikurupuka na kuacha 'singlet' yangu,sikumbishia kwani kweli niliondoka kwa haraka sana. Ikawa kila siku ananiambia kuwa huwa anaivaa ile singlet niliyoisahau na kunikumbuka sana. Jana nilimtembelea kwake kumjulia hali,nae kwa kunioneshea anachoniambiaga kila siku akaivaa tena ile singlet.Nilipoitazama vizuri nikagundua kumbe haikuwa ya kwangu.Nikimuuliza ananuna na kung'ang'ania kuwa ni ya kwangu wakati haifanani na singlet zangu, na harufu ya perfume si ya perfume n itumiayo. Hataki kukiri,na analazimisha niikubali...plz wana JF nahitaji ushauri wenu.
 
this is funyy
Ni kwamba mdada ana vidume viwili na vyote ninavaa singlet na kutumia perfume zinazofanana ...
duh lol
 
Kuna kijeba kina lala kati kati ya wiki wewe ni wa week ends kimbembe huyo mme mwenzio kama nae anademu anaye fua.
 
Hahahaaaaaaaaaaaaa! Kachanganya madawa !! Mulika Mwizi Meeeen!!!!! Unabugi Men!!!!
 
hahaha sasa ndio umejua kuwa wanawake wakoje..mwanamke wa dunia ya sasa kugegedqa na njemba mmoja ni ndoto...hawa wanapenda sana kutaste dushelele tofauti tofauti.....wamege na kusepa kaka
 
Utakuwa umesahau tu bro ni yako...na pengine perfume imepoteza nguvu na imenukia kivingine..amini tu ni yako!!
manake kama wewe mwenyewe unasema sio yako..sijui kama sisi tutasemaje?
Kaka hiyo anayodai ni yangu hata hainitoshi (over-size) na materials yake ni nylon, zangu ni cotton
 
kubali tu yako yaishe na uandelee kufanya close followup kwake, ila uichukue hiyo ukaichome asiendelee kuivaa
 
duh la leo kali, inamaana kama mwenzako ndo aliisahau ijumaa jioni yeye hakuiona mpaka ulipondoka?
swali la kizushi huyo mpenzio kabila gani?
 
this is funyy
Ni kwamba mdada ana vidume viwili na vyote ninavaa singlet na kutumia perfume zinazofanana ...
duh lol

jamani hivi zile research zisizokuwa na source zilisema idadi ya wanawake ndio kubwa kuliko ya wanaume au viseversa
 
Hahahahaahhaaaaaaaaa! huyo kapika KISHUMBA kamlisha mpemba hapo chacha!!!!! mm simooooooo!!
 
Yapata miezi minne (4) tangu nimejuana na mpenzi wangu,na mapenzi yemetukolea kweli kweli. Yeye ana makazi yake nami yangu. Huwa tunatembeleana week ends,ikiwa ni pamoja na kulala kabi. Kila tuwapo pamoja, mpenzi wangu hupenda kuvaa nguo zangu akidai anapenda harufu ya perfume yangu n.k. Week end iliyopita nililala kwake, niliamka mapema ili niwahi kupita nyumbani kwangu kuchukua baadhi ya vitu kwenda navyo ofisini,hivyo nikamuaga akiwa kitandani amelala. Nilipofika ofisini akaniambia kuwa nilikurupuka na kuacha 'singlet' yangu,sikumbishia kwani kweli niliondoka kwa haraka sana. Ikawa kila siku ananiambia kuwa huwa anaivaa ile singlet niliyoisahau na kunikumbuka sana. Jana nilimtembelea kwake kumjulia hali,nae kwa kunioneshea anachoniambiaga kila siku akaivaa tena ile singlet.Nilipoitazama vizuri nikagundua kumbe haikuwa ya kwangu.Nikimuuliza ananuna na kung'ang'ania kuwa ni ya kwangu wakati haifanani na singlet zangu, na harufu ya perfume si ya perfume n itumiayo. Hataki kukiri,na analazimisha niikubali...plz wana JF nahitaji ushauri wenu.





Ina maana humuamini mpenzi wako na laazizi wako? Kma unahisi hiyo nguo sio ya kwako then mulika mwizi na ujiulize mko wangapi??????
 
kwa uhakika wa asilimia tisini,mimi kama mwizi wa mapenzi mstaafu,nakuthibitishia unaibiwa(au wewe ndo unamuibia mtu...lol!usichukulie poa uwezo wa mwanamke kukushika masikio chalii yangu)!usijitengenezee majibu tofauti kichwani wala ndugu...unaibiwa na huyo dada kachanganya madawa tu.jasho utalijua tu!..uliza tu mzee.''TUKO WANGAPI''?
 
duh la leo kali, inamaana kama mwenzako ndo aliisahau ijumaa jioni yeye hakuiona mpaka ulipondoka?
swali la kizushi huyo mpenzio kabila gani?
Labda nae anadhani yuko peke yake kama mimi:redfaces:
 
Back
Top Bottom