Mpenzi wangu amepewa mimba na mtu mwingine

chifusongea

Senior Member
Joined
Jan 8, 2016
Posts
164
Reaction score
154
Kwa kifupi nilikuwa na mpenzi wangu na kilikuwa mwaka wa mwisho kumaliza,tangu tuanze uhusiano ilikuwa kama miezi 8 amalize.

Sasa kosa nililofanya ni kumsubiria amalize Sshule niwe nae, laaahaula kumbe kuna mwenzangu anamla mapema, kuja kustuka mpenzi kamemaliza baada ya wiki naenda kwao nijitambulishe naulizwa wewe ndiyo uliyempa mimba? Nikauliza ya miezi mingapi?Naambiwa mitatu.

Nikajibu mbona mimi sijawahi kufanya naye tendo la ndoa maana nilikuwa namsubiria amalize shule kisha nije nijitambulishe ndiyo mambo mengine yaendelee.

Nikaulizwa kwa hiyo tukusaidieje, nikajibu naona labda mimi nilikuwa mlezi na siyo mpenzi kwake.

Msaada ni kwamba kila nikitongoza msichana naomba kufanya nae mapenzi, tatizo akikataa tu najua ndiyo wale wale navunja mahusiano na umri wa kuoa umeshafika na nahisi nikiendelea na hii tabia sitaoa.

Msaada hapo.
 
Ha ha ha ushukuru wazaz wastaarabu ingekua huku uswahilin kwetu ungetoa mpka mahari
 
Weww ni mtongozaji si mlaji!
 
Mapenzi ya mwanzo yalikoishia, ndiyo hapo mapya uanzia.
 
Ongeza juhudi za kutongoza mkuu, hata wewe iko siku utakula
 
Hiyo ndo dawa yao ww tafuna tuu lisha pumba mixer dagaa mpige sopsop week tatu kula nyama km kuku wakizungu akinona wakuoa atatokea tuu.
 
hapo pangusa vumbi endelea na msako wa kumsaka mkee...

pia epuka vibinti vidogo tafuta matured...
 
"Mkuu ulichelewa, ni sawa nakusubiria bus kumbe nauli umeacha nyumbani"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…