Mpenzi wa kweli ni yupi???

Gwamahala

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
3,925
2,324
Wakubwa shikamooni,wadogo habari zenu. Wadau mi niko hapa kutafuta ukweli juu ya tabia za mpenzi aliye na mapenzi ya kweli.
 
hili swali gumu sana, watu hawafanani bana, nikikuambia tabia za mpenzi wangu haziwezi kufanana na za mwanamke mwingine. Nway
 
Wakubwa shikamooni,wadogo habari zenu. Wadau mi niko hapa kutafuta ukweli juu ya tabia za mpenzi aliye na mapenzi ya kweli.

Kwangu mpenzi wa kweli ni yule ambaye atakuwa na wewe mwanzo mpaka mwisho katika kipindi cha shida. Wakati wa raha rangi za watu huwa hazijulikani.

Kwa hiyo kujua walau kwa uhakika wa kuridhisha kama mpenzi wako ana mapenzi ya kweli au la ni pale shida fulani itakapojitokeza na kukaa kwa muda mrefu au mrefu kiasi. Hapo ndipo utajua nani ni nani. Bila ya hivyo ni ngumu kujua.
 
atakujali, atakuheshimu, atakutii, hatakuficha ficha mambo yake.
ONYO :
kuna mbwa mwitu waliojivika vazi la mwana kondoo!!
 
:bowl::bowl::bowl::A S-confused1::A S-confused1: ngoja nika ikariri dictionary......
 
Marahaba! Mpenzi wa kweli ni yule anayekupenda wewe na watu wako wa karibu, anayekujali wakati wote, muwazi, asiyemfikiria mwingine zaidi yako, anayejiheshimu na kukuheshimu, anayeheshimu interests zako, ambaye yupo tayari yeye asile ila wewe ushibe.

Nb:Mpenzi wa kweli ni wewe mwenyewe. Kabla hujampenda mwingine jipende wewe kwanza.
 
Back
Top Bottom