Mpenzi kukupa majukumu ya mke ni sawa?

Principle girl

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
1,107
1,094
Habarini waungwana,

Hivi mpenzi ambaye hata kwenye uchumba hamjafikia bado kukupa majukumu ya mke yani ukienda umfulie, umpikie, umsafishie na nyumba hivi ni sahihi kwa mwanamke kufanya hayo

Maana kuna jirani yangu hapa yeye yupo na msichana ni wapenzi tu lakini kambebesha majukumu hayo na mbaya zaid binti wa watu atafua jion wanakuja kulalia wengine na saa nyingine huyo kijana atampigia simu kwa kufoka yaani kana kwamba ni lazima,

Eti waungwana ni sahihi kuyafanya hayo kwa mpenzi
 
Nakushauri umueleze binti wa watu ukweli kuendelea kukaa kimya sio sawa afu pili kupewa majukumu hayo ni nyie wenyewe mnajirahisisha kwani papuchi inafaa apewe nani?si mume?ukinipa nashindwaje kukupa majukumu hayo wakati papuchi naifaidi daily?
 
Hoyo binti wa watu imejirahisisha sana ndiomaana anatumika kama dada wa kazi.
 
Mbona wanaume tunagewa majukumu ya mume, baba, rafiki, fundi ujenzi, fundi seremala, mcheza x, mhasibu, mshauri hadi majukumu ya kikaka lakini hatuulizi kama ni sawa?
Sasa kumfulia mtu uliyempa majukumu yote hayo sioni tatizo.
 
Habarini waungwana,hivi mpenzi ambaye hata kwenye uchumba hamjafikia bado kukupa majukumu ya mke yani ukienda umfulie umpikie umsafishie na nyumba hivi ni sahihi kwa mwanamke kufanya hayo maana kuna jirani yangu hapa yeye yupo na msichana ni wapenzi tu lakini kambebesha majukumu hayo na mbaya zaid binti wa watu atafua jion wanakuja kulalia wengine na saa nyingine huyo kijana atampigia simu kwa kufoka yani kana kwamba ni lazima,eti waungwana ni sahihi kuyafanya hayo kwa mpenzi
 

Attachments

  • IMG_20170423_205524.jpg
    IMG_20170423_205524.jpg
    43.8 KB · Views: 40
Mambo mengi tunafanyiana kabla ya ndoa sio majukumu yetu.

»Kufanya ngono, sio majukumu yetu, hadi pale sheikh, askofu, padre, mchungaji au serikali itakapohalalisha.

»Mdada kufanya house chores kwa mpenzi wake sio sahihi kabla hawajaoana.

» Kupeana matunzo ya kifedha sio sahihi hadi muoane, wazazi wanafanya nini hadi umtunze binti yao kabla hujamuoa.

»Kusomesha mchumba sio jukumu lako.

...na mengine mengi tu.
 
Mkuu hata sisi watu wa soka tunajua kuwa mchezaji kabla hatujamsajili na kumpa ulaji lazima afanye trials ili kujiridhisha na kiwango chake.

Sasa wewe unadhani nani anataka kuuziwa mbuzi kwenye gunia?
 
Sidhani kama kuna ubaya ikiwa unayemfanyia ana muelekeo wa kufika mbali zaidi mpaka kuoana.
Ikiwa mtu haeleweki ya nini kujihangaisha mwisho wa siku anakuja kuoa mwingine.

Nadhani ni sisi wanawake kujitahidi kuwasoma japo ni ngumu kabla ya kuanza kumfanyia yote hayo ikiwa hana mwelekeo bora afanye mwenyewe aisee.

Japo kuwa sio sawa ila kwa maisha tunayoishi ni ngumu.
 
Mara nyingine hayo majukumu hata hajapewa ila katika kujishikiza na kulinda himaya analazimisha kuyafanya hasa kama ni wale ambao ni ving'ang'anizi. Unaweza kuta jamaa kapewa majukumu ya zaidi hata ya baba, kwahiyo hayo ya usaidizi wa nyumbani sio tatizo kama mwenyewe anaridhia...maana nijuavyo wengi hutaka wao wenyewe ndio hujisiki wamemiliki himaya.
 
Mambo mengi tunafanyiana kabla ya ndoa sio majukumu yetu.

»Kufanya ngono, sio majukumu yetu, hadi pale sheikh, askofu, padre, mchungaji au serikali itakapohalalisha.

»Mdada kufanya house chores kwa mpenzi wake sio sahihi kabla hawajaoana.

» Kupeana matunzo ya kifedha sio sahihi hadi muoane, wazazi wanafanya nini hadi umtunze binti yao kabla hujamuoa.

»Kusomesha mchumba sio jukumu lako.

...na mengine mengi tu.
Kama jamiii kuna sehemu ipo shida saana kuanzia kwenye makuzi yetu.

Elimu inayotolewa Ni ya darasani tuu elimu ya mahusiano plus sijui jando hamna.

Vijana wa nafanya vile wanavyoona wao sio kwa misingi au maadili yetu sio kwa sababu wanapenda Ila hawana elimu.

Wanaangamia kwa kukosa maarifa.

Unamfulia, unampikia , daaahhh rahisi kukuchoka na kwenda kuoa kwingine
 
Back
Top Bottom