Mpenzi endelea tu kununa, nimeamua kumsaidia dada yangu!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
"Nilipanga hiyo hela nimsaidie ili aongezee mtaji afungue saluni ya kike. Kabla ya kumpatia hiyo pesa ikaja taarifa ya kuuguliwa na binamu yangu. Kutokana na umuhimu wake kwangu, nikaamua pesa, nilopanga kumpa yeye ili aanzishe mradi wake wa saluni, niipeleke kwenye matibabu ya binamu yangu aliye mgonjwa sana.

Akadai eti simpendi vinginevyo ningempa yeye kwanza halafu nifanye mpango wa kutafuta nyingine ili nimtibie huyo ndugu yangu kwani yeye alikuwa wa kwanza. Hadi leo ni wiki imepita amenuna na akipigiwa simu hapokei, na wala hajakuja kumuona wifi yake mtarajiwa. Mwanzoni niliona kama ni mwanamke anayeweza kuwa mke wa maana lakini ktk hili nimeanza kuwa na wasiwasi juu ya upendo wake kwa ndugu zangu. Iweje ameshindwa kuona umuhimu wa kutibu ugonjwa ili kuepusha kifo? Je mchumba dizaini hii kweli kuishi na ndugu wa mume kweli achilia mbali kuwasaidia wakati wa shida?".

Kadhia hii imemkuta mtu wangu wa karibu na ameomba nimshauri la kufanya juu ya huyu 'kishtobe' wake alokuwa akimpa nafasi ya kuwa mkewe siku za usoni.

Jamaa ameboreka hasa kutokana na tabia iliyoonyeshwa na huyu 'kishtobe' wake. Bado anajishauri aendelee na mpango wa kumuoa au amteme jumla jumla kwa sababu ya dalili hii mbaya aloionyesha mapema?
 
hajaolewa hali hiyo,akiolewa itakuwa zaidi.wenzake kabla hawajaolewa,huwa heshima kwa mawifi na mashemeji,ili waipate hiyo ndoa.wakishaolewa mambo huwa tofauti.akili kichwani mwake
 
Katika ugonjwa ameweza kutamka hayo, je likija suala la kusomesha ama kusaidia masomo ya watoto wa ndugu?????? Sina nafasi ya kutoa maamuzi juu ya kuwa mwanamke bora au bora mwanamke tu ila hayo ninamuachia muoaji.
 
Hicho ni kipimo ambacho huyo jamaa yako anaonyeshwa mapema kabla hajasema ''I do''. Ni muhimu kuzingatia na kuchukua uamuzi sahihi.
 
hafai huyo,izo ndo dizaini zinazowaambia waume zao wachague mama au mke likijitokeza tatizo kama hili
 
Ana matatizo, maana afya ya mtu ikipotea hairudi. Hela zinatafutika, mwambie awe na ubinadamu
 
Mwambie mungu anampenda sana kumuonyeshea hayo mapema sasa kama anataka ushauri zaidi ya hapo atakua mtumwa wake na mwisho hata wazazi wake watambiwa wanachafua sofa...
 
Halafu usije ukategemea kupata chochote toka kwny hiyo saluni, sana sana atakuambia ni mali yake.
 
Huyo yaonekuna hana aibu wala subra sasa basi dalili ya mvua mawingu,
hakufai huyo leo dada kesho atakua mama naulishauhaidi kumpeleka shopping siitakua noma.
 
huyo hafai, yuko ki maslahi zaidi. piga chini, songa mbele...
 
Maanadiko yanasema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" unataka upewa maarifa gani tena zaidi ya kulitambua tatizo, juu yake sasa kufanya maamuzi.
 
hahaha kama anampenda amuoe tu at his own risk , lakini ajue there are still more to come.
 
Wanasema samaki mkunje angali mbichi, akionyesha weakness kwenye hili 'itakula kwake'-chambilecho Mrema!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom