Mpenzi ana mahusiano na Mtu mwingine

Mpenzi ana mahusiano na Mtu mwingine

kintu

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
542
Reaction score
136
Wana JF,katika kipindi cha hivi karibuni nimegundua mpenzi wangu ana mahusiano na mtu mwingine japo wako mbali mmoja yupo Dar na Mwingine Arusha,hawa watu wanafamihamina kwa muda mrefu ,sina huakika kama wamewahi kuwa wapenzi ,ila nikwamba walipotezana na wamekuja kukutana Facebook,ndo message za dear,sweet,bby,umekula nini dear,n.k zimeanza.

Nilianza kuhisi kitu ,maana mwenzangu mwanzo alikuwa hana wasiwasi anapokuwa fb,lakina sasa amekuwa akikakaa na cmu yake muda wote,na ukiingia chumbani au sebuleni anapokuwa anachat anashutuka na kufunga page ,mara ata ongea hivi mala vile au ajifanye alikuwa anacheza game n.k.

Baada ya kuona hivyo niliamua kufuatilia na nilibaatika kuingia kwenye chat zake ndo nikaona hizo chat ,na kuanzia hapo nimekuwa nazifuatilia kila wanapo chat,Sijamwambia chochote na nilitaka nipate details za kutosha maana hisia siyo nzuri hasa ikitokea kuwa hazina ukweli wowote.

Ningependa kupata ushauri wenu..
1.Je nisahii kufutila chat za mpenzi wako unapoona mambo yake yana utata..na ukagundua ni kweli ?
2.Je nimwambie au nisubiri wandelee na mipango yao ya kupanda Fast Jet wakati ukiwadia ndo niwakamate maana kwa sasa wako mabali?
3.Je mpenzi wangu hakijua nimeweza kutrace chat zake itakuwaje japo ndo nimeshajua ukweli,Je atajitete kuwa wanachat tu na hakuna kitu kinaweza kutokea kwa kuwa woko mabli?

Naomba Ushauri wenu kwa kuzingatia tunafamilia ya mtoto mmoja.
 
ah kumbe mpenzi na ulishazaa nae kweli wee wakajanga....ah sasa hapo nikukubali tuu mweza sio mwaminifu na mkae uvumilie mlee mtoto
 
Kama mna mtoto muonye mpange maisha ya baadae ya huyo mtoto.
 
Sasa kwa nini uwendelee kuwa na mtu anayekupa waswasi kila leo na kukukosesha Amani? Kwanini usichukue uamuzi mgumu? Ni wazi huyoo si muaminifu wala usiimize kichwa kufanya upelelezi.
 
Ni mpenzi wako, nini mwisho wa hayo mapenzi yenu kaka, maana kwangu mimi nashindwa kutoa ushauri kwa sababu sijui hujasema nini mpango wa baadaye juu ya mapenzi yenu hayo.

Funguka zaidi ili watu wakushauri ipasavyo.
 
Kwanza hapa sijajua hata niki comment nitakuwa namsaidia mtu wa aina gani, kwanza wewe ni dada au kaka??unaweza kurahisha zaidi then tuendelee??Nadhani number 1 umeshafanya tayari so sidhani kama kuna haja ya ushauri na zaidi mkalishe chini ongea nae tu kiutu uzima why ukae na kitu moyoni unaumia tu, mwambie ukweli kama yeye ana akiri za kutosha atajuwa anafanya vibaya na atabadilika
 
Wana JF,katika kipindi cha hivi karibuni nimegundua mpenzi wangu ana mahusiano na mtu mwingine japo wako mbali mmoja yupo Dar na Mwingine Arusha,hawa watu wanafamihamina kwa muda mrefu ,sina huakika kama wamewahi kuwa wapenzi ,ila nikwamba walipotezana na wamekuja kukutana Facebook,ndo message za dear,sweet,bby,umekula nini dear,n.k zimeanza. Nilianza kuhisi kitu ,maana mwenzangu mwanzo alikuwa hana wasiwasi anapokuwa fb,lakina sasa amekuwa akikakaa na cmu yake muda wote,na ukiingia chumbani au sebuleni anapokuwa anachat anashutuka na kufunga page ,mara ata ongea hivi mala vile au ajifanye alikuwa anacheza game n.k. Baada ya kuona hivyo niliamua kufuatilia na nilibaatika kuingia kwenye chat zake ndo nikaona hizo chat ,na kuanzia hapo nimekuwa nazifuatilia kila wanapo chat,Sijamwambia chochote na nilitaka nipate details za kutosha maana hisia siyo nzuri hasa ikitokea kuwa hazina ukweli wowote. Ningependa kupata ushauri wenu.. 1.Je nisahii kufutila chat za mpenzi wako unapoona mambo yake yana utata..na ukagundua ni kweli ? 2.Je nimwambie au nisubiri wandelee na mipango yao ya kupanda Fast Jet wakati ukiwadia ndo niwakamate maana kwa sasa wako mabali? 3.Je mpenzi wangu hakijua nimeweza kutrace chat zake itakuwaje japo ndo nimeshajua ukweli,Je atajitete kuwa wanachat tu na hakuna kitu kinaweza kutokea kwa kuwa woko mabli? Naomba Ushauri wenu kwa kuzingatia tunafamilia ya mtoto mmoja.
Taarifa umeipata mwenyewe wala hujaambiwa na mtu mwingine sasa unasubiri nini? fanya maamuzi magumu uokoe nafsi yako isiteseke bure.
 
...mkuu kwakuwa wewe ndo unammiliki huyo mwadada kwa sasa na kwa utaratibu wa kawaida wa mapenzi,wewe ndo unahatimiliki ya kuitwa
dear,sweet,baby,dear,honey n.k...lakin kwakuwa umeisha gundua kuwa kunamtu mwingine naye anaitwa hayo majina,nakushauri uanzetaratibu nyingine za kutafuta mpenzi mwaminifu kabla haujapatwa na ugonjwa wa moyo...
 
Yaani hakuna kitu kinauma kama unaishi na mtu wakati unaelewa kabisa anakusaliti..! Una moyo mgumu sana..!
 
Penda unapopendwa...hayo ndio mapenzi!!
 
kuendelea kuwaacha ni kuzidi kuwafanya wawe karibu zaidi, chukua hatua mara moja kwa kukaa na kuongea naye. safari ya mapenzi ina changamoto nyingi kikubwa ni namna gani unazikabili.
 
Ni mpenzi wako, nini mwisho wa hayo mapenzi yenu kaka, maana kwangu mimi nashindwa kutoa ushauri kwa sababu sijui hujasema nini mpango wa baadaye juu ya mapenzi yenu hayo.

Funguka zaidi ili watu wakushauri ipasavyo.

Lyagwa sikupenda kufunguka sana ili nisijemwaga kila kitu kabla ya kupata ushauri na kufanya maamuzi sahihi. Kwa ufupi tunaishi pamoja .
Its looks a very happy family by the way...
 
mkuu kintu, mbona kama demu mwenyewe unamuogopa? watu wengine mna uvumilivu. mi ningekua nshamakiza mchezo mapema. huyo sio mwanamke ni kikwekwelekwe. haya ndo madhara ha kumchunguza mpenzio. ni kujipa presha. mia
 
Last edited by a moderator:
Lyagwa sikupenda kufunguka sana ili nisijemwaga kila kitu kabla ya kupata ushauri na kufanya maamuzi sahihi. Kwa ufupi tunaishi pamoja .
Its looks a very happy family by the way...

Kama mnaishi pamoja kama familia as you said, let say for two years or more then she is your wife as per Tanzania regulations nadhani sheria ya ndoa ya 2004. Hii inamaanisha kuwa japokuwa hamjafunga ndoa thus why unamuita mpenzi lakini already kila mmoja wenu ana haki juu ya mwingine.

Katika mkutadha huo basi una kila sababu sasa ya kufuatilia hayo mawasiliano ya huyu mpenzi wako kwa karibu ili kuyavunja na kulejesha amani ya moyo wako kwake ama pia aweze kufanya maamuzi sahihi mapema kama ni kuachana iwe mapema msije potezeana muda bure kumbe mwenzako ana lake jambo.

Mwisho kabisa uamuzi unao wewe mwenyewe na hii pia inategemea ni kwa kiwango gani unampenda huyu mpenzi wako hadi kwa wakati huu unaoleta thread yako hapa kwenye jukwaa la mmu.

Nakutakia uamuzi sahihi mkuu, mapenzi ni maisha na maisha ni mapenzi




 
Back
Top Bottom