Mpendwa wangu moyo

Paw

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
2,113
2,000
Umepevuka na kuwanda kaka
Midundo pu! pu! pu! pasichoka
Mawazo yangu umeyapakata
Hisia za mahaba kufichuka
Utungu wa simanzi unakumbuka?

Mchana damu wasukuma
Usiku hukuacha kuvuma
Mara nyingi nilikwama
Maradhi na hatari lawama
Uongo pia nilisema

Mikono uliijaza nguvu
Damu ilifika bila povu,
Miguu uliipa ukakamavu
Akili haikuwa chakavu
Mirija hadi kwenye kidevu
Haukuacha wako unyenyekevu

Leo umetweta tweta
Hospitalini nilikuvuta
Nimekuletea utata
Nilalapo bado naota
Maisha haya yana vita?

Nyie miguu nawalaumu
Tena mkapate hukumu
Mlimpeleka kwa kaumu
Penzini kwa vidumu
Hamkujali mkamdhulumu

Nimekuomba nakuomba sana
Usichoke kunipa amana
Thamani kama yako hamna
Tiririka mpendwa bila namna
Samahani mara nilizokukana

Loh hatimaye safari itaisha
Najua hili linakutisha
Ukisimama basi nimeisha
Hodi na kwaheri zakinaisha
Urefu wa njia utakwishaNakupenda moyo wangu

Wakuu ni wiki sasa tangu nimeambiwa nina tatizo linalohusiana na maradhi ya moyo.
nimeweka hii tenzi kuubembeleza Moyo usiache na kunipa kampani maana nauona una hofu kweli..... 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,749
2,000
Sasa l'aziz inabidi uniandikie nijibu mapigo hapa ya huu utenzi . Ila mie nipo hapa, huo moyo tutaufunga papi na nitaubeba mgongoni hadi tuzeeke pamoja. Huyu Excel muache asubirie mkono udondoke. BADILI TABIA, hii kapo yetu imeishinda ya zarimondi
 
Last edited by a moderator:

Excel

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
18,807

Paw anahitaji morning jogging everyday...
Mbadilishie mfumo mzima wa 'malisho' yake ya kila siku..
Acha kumpa stress..:glasses-nerdy:
Then....:mimba:...on time! okay?
 
Last edited by a moderator:

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,035
1,500
Umeufanya nini moyo wa mwenzio?

Usinambie ushakuwa mkaanga sumu za mioyo?

Pole sana Paw, nitakuombea upone, ila nawe usiache kufuata ushauri wa madaktari.

Sasa l'aziz inabidi uniandikie nijibu mapigo hapa ya huu utenzi . Ila mie nipo hapa, huo moyo tutaufunga papi na nitaubeba mgongoni hadi tuzeeke pamoja. Huyu Excel muache asubirie mkono udondoke. BADILI TABIA, hii kapo yetu imeishinda ya zarimondi
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,749
2,000
Dr kasema morning glory mara mbili kutwa, na asilale njaa.
Sasa hii ya jogging wewe ndio umeongezea bwana.

Nampenda mno hadi anapata stress, ngoja nikuchukue mchepuko ili nipunguze mahaba basi
Paw anahitaji morning jogging everyday...
Mbadilishie mfumo mzima wa 'malisho' yake ya kila siku..
Acha kumpa stress..:glasses-nerdy:
Then....:mimba:...on time! okay?
hahaha hamna bwana, anapendwa sana huyu hadi moyo unagoma.
Umeufanya nini moyo wa mwenzio?

Usinambie ushakuwa mkaanga sumu za mioyo?

Pole sana Paw, nitakuombea upone, ila nawe usiache kufuata ushauri wa madaktari.
 
  • Thanks
Reactions: Paw

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
8,596
2,000
Moyo tulia usinipe udhia
Kiungo muhimu hakina karaha

Taratibu usinipe simanzi
Moyo poa kwa mengi unijali
 
  • Thanks
Reactions: Paw

Excel

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
18,807
2,000
Paw unaendeleaje mkuu?

Jaribu kuwa unakimbia sana as morning exercises.. Na hivyo dala dala hazifanyi kazi, it will be a nice jogging with ur baby, King'asti!!!:sad:
 
Last edited by a moderator:

Paw

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
2,113
2,000
Paw unaendeleaje mkuu?

Jaribu kuwa unakimbia sana as morning exercises.. Na hivyo dala dala hazifanyi kazi, it will be a nice jogging with ur baby, King'asti!!!:sad:
Soma hapa mkuu, Dokta ameshauri na jitihada zipo

Dr kasema morning glory mara mbili kutwa....
Wakuu naendelea vyema na huyu moyo.

Tiba inaendelea vyema nazingatia ushauri wa wataalam naamini second test itatoa majibu mazuri.
Ila mazoezi nimekatazwa kwani moyo umeonekana umeongezeka ukubwa na hivyo sintofahamu zote zimeletwa na such probe
 
Top Bottom