Paw
Content Manager
- Nov 14, 2010
- 2,109
- 1,360
Umepevuka na kuwanda kaka
Midundo pu! pu! pu! pasichoka
Mawazo yangu umeyapakata
Hisia za mahaba kufichuka
Utungu wa simanzi unakumbuka?
Mchana damu wasukuma
Usiku hukuacha kuvuma
Mara nyingi nilikwama
Maradhi na hatari lawama
Uongo pia nilisema
Mikono uliijaza nguvu
Damu ilifika bila povu,
Miguu uliipa ukakamavu
Akili haikuwa chakavu
Mirija hadi kwenye kidevu
Haukuacha wako unyenyekevu
Leo umetweta tweta
Hospitalini nilikuvuta
Nimekuletea utata
Nilalapo bado naota
Maisha haya yana vita?
Nyie miguu nawalaumu
Tena mkapate hukumu
Mlimpeleka kwa kaumu
Penzini kwa vidumu
Hamkujali mkamdhulumu
Nimekuomba nakuomba sana
Usichoke kunipa amana
Thamani kama yako hamna
Tiririka mpendwa bila namna
Samahani mara nilizokukana
Loh hatimaye safari itaisha
Najua hili linakutisha
Ukisimama basi nimeisha
Hodi na kwaheri zakinaisha
Urefu wa njia utakwisha
Nakupenda moyo wangu
Wakuu ni wiki sasa tangu nimeambiwa nina tatizo linalohusiana na maradhi ya moyo.
nimeweka hii tenzi kuubembeleza Moyo usiache na kunipa kampani maana nauona una hofu kweli.....
Midundo pu! pu! pu! pasichoka
Mawazo yangu umeyapakata
Hisia za mahaba kufichuka
Utungu wa simanzi unakumbuka?
Mchana damu wasukuma
Usiku hukuacha kuvuma
Mara nyingi nilikwama
Maradhi na hatari lawama
Uongo pia nilisema
Mikono uliijaza nguvu
Damu ilifika bila povu,
Miguu uliipa ukakamavu
Akili haikuwa chakavu
Mirija hadi kwenye kidevu
Haukuacha wako unyenyekevu
Leo umetweta tweta
Hospitalini nilikuvuta
Nimekuletea utata
Nilalapo bado naota
Maisha haya yana vita?
Nyie miguu nawalaumu
Tena mkapate hukumu
Mlimpeleka kwa kaumu
Penzini kwa vidumu
Hamkujali mkamdhulumu
Nimekuomba nakuomba sana
Usichoke kunipa amana
Thamani kama yako hamna
Tiririka mpendwa bila namna
Samahani mara nilizokukana
Loh hatimaye safari itaisha
Najua hili linakutisha
Ukisimama basi nimeisha
Hodi na kwaheri zakinaisha
Urefu wa njia utakwisha
Nakupenda moyo wangu
Wakuu ni wiki sasa tangu nimeambiwa nina tatizo linalohusiana na maradhi ya moyo.
nimeweka hii tenzi kuubembeleza Moyo usiache na kunipa kampani maana nauona una hofu kweli.....