Mpendazoe: Nihukumiwe kwa dhamira yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpendazoe: Nihukumiwe kwa dhamira yangu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Aug 18, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,192
  Trophy Points: 280
  JULAI 14 mwaka huu aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kishapu na msemaji mkuu wa kilichokuwa Chama cha Jamii (CCJ), Fred Mpendazoe, alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Mbali na kujiunga na chama hicho, mbunge huyo aliyejipatia umaarufu kama mmoja wa makamanda waliokuwa wakipinga ufisadi bungeni, pia alitangaza dhamira yake ya kugombea ubunge katika Jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam.

  Tayari Mpendazoe amepitishwa kuwa mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA baada ya kushinda rufaa yake ya kupinga matokeo ya kura ya maoni yaliyokuwa yamempa ushindi mwanasiasa chipukizi, Rachel Mashishanga.

  Hata hivyo, katika harakati zake hizo, Mpendazoe amekuwa akiandamwa na maswali makubwa mawili ya msingi yanayoonekana kudadisi utashi, uadilifu na msimamo wake wa kisiasa hasa akiwa katika chama chake kipya – CHADEMA.

  Kwanza, kwanini alipotoka CCM alikwenda kwanza CCJ badala ya kujiunga moja kwa moja na CHADEMA?

  Pili, baada ya kujiunga na CHADEMA kwanini aliamua kugombea ubunge Segerea badala ya kuendelea na Jimbo la Kishapu?

  Nikitilia maanani kiu ya baadhi ya wafuatiliaji wa mambo ya siasa kutaka kupata majibu yake juu ya maswali hayo, nilimtafuta mwanasiasa huyo mwishoni mwa wiki na kufanya naye mahojiano maalumu. Mwanasiasa huyo alitoa maelezo au majibu yafuatayo kuhusiana na maswali hayo:

  “Acha nikupe ufafanuzi wa kutosha, juu ya maoni mbalimbali yanayohusu sababu zilizonifanya nihame CCM na kwenda CCJ na baadaye kuhamia CHADEMA. Baadhi ya watu wanatoa hukumu ya jumla badala ya kuangalia dhamira ya mtu. Kwanza, naomba nitoe mfano uliotolewa na mwandishi Majid Mjengwa kama moja ya maandiko yake, ambao naamini utawasaidia Watanzania kukielewa kile ninachotaka wakielewe.

  Katika kitabu cha ‘The Moral of the Story’, magazeti ya Marekani yaliripoti tukio la ajali ya moto katika eneo la ‘Pacific Northwest’.

  Familia moja iliyokuwa ikiishi eneo hilo ilikwenda likizo fupi. Waliacha funguo za nyumba kwa jirani ili amwagilie maua yao. Jumapili moja saa kadhaa kabla ya familia kurudi, baridi iliongezeka sana. Jirani akaona ni vema awaandalie jirani zake makazi mazuri yenye joto.

  Hivyo, bwana yule aliingia nyumba ya jirani na kuwasha moto wa kuni kwenye tanuri. Kumbe upepo wa mchana uliopita dirishani ulisababisha moto kusamba ndani na kuunguza na kuteketeza nyumba. Wenye nyumba waliporudi waliyakuta majivu ya nyumba yao, kila kitu kimeteketea. Jirani huyu alikumbwa na huzuni kubwa kutokana na magazeti kuandika kuwa yeye ndiye aliyesababisha moto ule kwa makusudi.

  Jirani aliyewasha moto alilazimishwa kujibu maswali yaliyohusiana na hatima ama matokeo ya kitendo alichokifanya. Hakuna aliyefanya kazi kuuliza ni kwa nini aliwasha moto ule ili afahamu dhamira ya tendo lile.

  Funzo hapa ni kuwa, wanadamu tunapaswa kuwahukumu binadamu wenzetu kutokana na dhamira zao na si kwa matokeo ya matendo yao tu.

  Jirani aliyewasha moto kwa dhamira njema alipata misukosuko kutokana na nyumba kuungua. Wangezingatia dhamira yake huenda wangemsifu kwa alichokifanya. Licha ya kufikwa na bahati mbaya kwa nyumba kuungua lakini ni ukweli usiopingika kuwa dhamira yake ya kuwaandalia joto jirani zake waliokuwa warudi siku hiyo kutoka likizo, ilikuwa dhamira njema sana. Sasa nifafanue nini ilikuwa dhamira yangu juu ya maswali hayo uliyoniuliza.
  Nilihamia CCJ tarehe 30 Machi 2010 na sababu za msingi zilizonifanya nihamie CCJ bado ni hai na bado ninaamini nilifanya maamuzi sahihi na sijajutia maamuzi hayo. Mageuzi ya kidemokrasia, kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa faida ya kizazi cha sasa na ya vizazi vijavyo yatapatikana hatua kwa hatua.


  Hatua ya kwanza ni kuwa na Bunge lenye wabunge wengi wa upinzani ambao watatetea mageuzi hayo kwani ni dhahiri sasa uongozi uliopo wa CCM hauwezi kuongoza mageuzi hayo. Hii ndiyo ilikuwa sababu yangu ya kuhamia CCJ.

  CCJ haikupata usajili wa kudumu si kwa sababu haikuwa na wanachama bali ni tatizo la mfumo wa utawala tulionao. Tukumbuke Msajili wa Vyama vya Siasa nchini huteuliwa na kuapishwa na Rais wa chama tawala. Ni dhahiri utendaji kazi wake na maamuzi yake lazima yazingatie masilahi ya aliyemteua. Watanzania watakumbuka CCJ iliomba usajili wa muda tarehe 19, Januari 2010 na ilipata usajili huo tarehe 2, Machi 2010 na ni baada ya mvutano mkubwa.

  CCJ ilikubalika kwa Watanzania nchi nzima na ilipata wanachama wengi na si kweli kwamba haikuwa na wanachama kama Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ilivyodai. Aliyekuwa Katibu wa CCJ na Katibu Mwenezi wake ndio waliokuwa wanatafuta wanachama na ndio walioshughulikia usajili wa CCJ.

  Msajili wa Vyama vya Siasa kaifuta CCJ na kusajili CCK kwa maombi ya siku mbili tu na cha kushangaza Katibu wa CCK ni yule yule aliyekuwa CCJ na Mwenyekiti wa CCK ni yule aliyekuwa Katibu Mwenezi na Katiba ya CCK ni ile ile ya CCJ isipokuwa penye herufi J imewekwa K. Hii ndiyo kazi nzuri ya Msajili wa Vyama vya Siasa? Tunahitaji Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa iwe huru na itende haki.

  Ni bayana CCJ imehujumiwa kwa maslahi ya watu wachache na kwa faida ya chama kinachoogopa upinzani wa kweli. Tulitaka CCJ iwe na nguvu ili ishirikiane na vyama vingine vyenye nguvu hasa CHADEMA na kuhakikisha kwa pamoja tunapata wabunge na madiwani wengi pamoja na rais kwa masilahi ya Tanzania.

  Tangu awali CCJ ilikuwa na lengo la kuungana na CHADEMA, kuwa na alliance (umoja) ili kuimarisha upinzani kama ingepata usajili wa kudumu. Na kuwa na utaratibu wa wana CCJ kugombea kupitia CHADEMA kama usajili wa kudumu usipopatikana. Inasikitisha sana kama mtu anaona kwamba uchu wa madaraka ndio uliosababisha maamuzi hayo.

  Tukumbuke Watanzania wamekata tamaa kwa sababu ya matatizo mbali mbali yanayowakabili wananchi yakiwemo maamuzi kadhaa yenye utata.

  Watanzania wakumbuke maamuzi ya Mahakama ya Rufaa juu ya suala la mgombea binafsi. Tatizo ninaloliona ni lile lile la mfumo. Jaji wa Mahakama ya Rufaa huteuliwa na kuapishwa na rais. Hapa lazima pawe na mgongano wa masilahi wakati wa kufanya maamuzi. Ipo haja ya kuwa na katiba mpya itakayoondoa mfumo wa kulindana uliopo, la sivyo mageuzi ya kweli ya kidemokrasia na kiuchumi ni vigumu kupatikana.

  Wenzetu Kenya hivi karibuni waliona upungufu wa katiba yao ya zamani na kupiga kura nyingi za kuunga mkono katiba mpya. Kwa yeyote anayeijua katiba ya zamani ya nchi hiyo na hii ya kwetu, atakubaliana nami kuwa kwa kiasi kikubwa upungufu wake ulikuwa unafanana na huu wa katiba yetu ya sasa.

  Lakini wenzetu tayari wamepiga hatua kubwa mbele, zaidi ya kutuzidi kiuchumi sasa wamekuwa wa kwanza kuibadilisha katiba, tusipoibadili hii ya kwetu ili kuondoa mgongano mkubwa wa kimasilahi uliopo ni dhahiri kuwa tutaendelea kukwama katika shughuli za kimaendeleo maana uwajibikaji wa utawala kwa umma wa Watanzania utaendelea kuwa kikwazo.

  Ndiyo maana hata mgombea wetu wa urais, Dk. Wilbrod Slaa amelipa kipaumbele suala la kubadili katiba ya nchi hii pindi akiingia ikulu - ambapo ataianza kazi hiyo baada ya siku tisini tu tangu siku atakayoingia madarakani.

  Tunashuhudia uozo wa maadili unavyogharimu maisha ya Watanzania kila kukicha. Nilidhani waliojitoa mhanga kuanzisha CCJ wangeonekana ni mashujaa na wazalendo badala yake wanabezwa na baadhi ya Watanzania.
  Ninaamini siku si nyingi Watanzania wote wataelewa kwamba chama hicho kilikuwa na wanachama wengi nchi nzima lakini kilifutwa kwa sababu za mfumo wa kulindana tulionao. Walioanzisha CCJ wasihukumiwe kwamba hawakuwa makini, tazameni dhamira yao.


  Mageuzi ya kidemokrasia, kiuchumi, kijamii na kisiasa Tanzania hayatapatikana bila gharama. Kutakuwepo na mapambano makali kati ya utawala wa sasa unaokandamiza Watanzania wengi wanyonge na wale watakaojitolea mhanga kutetea masilahi ya wengi.

  Tuelewe, katika mapambano yoyote, wapambanaji wale walioko msitari wa mbele wana majukumu magumu na wanajeruhiwa sana kuliko wengine wote, aidha, unyama mwingi watakaofanyiwa na dhihaka watakazopata si kwa bahati mbaya.

  Na pia tuelewe kwamba ukiwa hapa duniani uwe tayari kufanya mambo yasiyo na faida kwako wewe binafsi tu, bali uwe tayari kufanya mambo yenye faida kwa jamii kwa sasa au baadaye, ingawa watu wa namna hiyo ni wachache sana lakini ndio wanaoweza kuleta mabadiliko kwenye jamii au taifa. Hivyo basi, waliothubutu kuanzisha CCJ naomba waheshimuni hata kama chama hakikupata usajili wa kudumu, walikuwa na nia njema.

  Dhamira yangu ya kutoka CCM kwenda CCJ ni ilele iliyonifanya nitoke CCJ kwenda CHADEMA na ni dhamira ile ile ambayo ilinifanya nikubali kugombea Segerea.

  Najua ninachokitaka, sitachoka kukitafuta wala sitakata tamaa, pia najua gharama yake ni kubwa. Mzee Mandela pia amesema ninukuu: “Popote pale hakuna njia rahisi ya ukombozi, na wengi wetu itabidi tupite tena na tena kwenye bonde la kivuli cha mauti kabla ya kufikia kilele cha mafanikio.”

  Kuleta mageuzi ya kidemokrasia, kiuchumi, kijamii na kisiasa Tanzania ndiyo lengo kuu linalonisukuma kuwa na dhamira niliyonayo.
   
 2. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mimi huyu jamaa simkubali kabisa, kwa sababu yupo kama "Rolling stone" hawezi kutulia
  Sasa ameenda huko, kuna matatizo yake pia na asipokwenda vema nako atahama na atachanganyikiwa kabisa.
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Aug 18, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  nilihisi mapema, rangi zako zinaanza kujionyesha. maneno yako, akili zako hazitofautiani na yule mjamaa-Jeykey.
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,192
  Trophy Points: 280
  Ukiona mtu yeyote mwenye mwelekeo wa udini jua hakuna kitu ndani, angalia avatar yake.
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Aug 18, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  nimekusoma, nimekuelewa.
   
 6. w

  wasp JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii virus nyingine ya sisiem. CHADEMA watchout. He may be another type of mzee wa Kiraracha but from Kishapu this time around.
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,192
  Trophy Points: 280
  Nafikiri tumpe muda najua Chadema wako makini watampima kwa matendo yake.
   
 8. H

  Haika JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  watu wote ambao wanajaribu kuhangaikiamajambo magumu kama haya lazima waonekane kama vichaa.
  Waliokaa kimya unaweza ukadhani ndio wenye akili, kumbe ndio wajinga au vichaa zaidi.

  hii vita ni ngumu jamani,
  inahusisha wabinafsi, wenye moyo wa kujitolea, tofauti ni asilimia ya ubinafsi na kujitolea, wote tuko in between.
  Uvunjaji wa sheria ndo hautakiwi
   
 9. minda

  minda JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  huyu jamaa ana dhamira nzuri tu kwa watanzania. tusubiri tuone.
   
 10. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu hana shaka ni jirani na Makongoro na hawaongei miaka mingi tu! angekuwa kwenye System wangekuwa mashoga
   
 11. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu unajua,wapo wengi tuu kama huyu wa chini hapa
  Shalom [​IMG]
  JF Premium Member


  [​IMG]
   
 12. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,503
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Nyie ndiyo mnaochanganaya watu hasa katika kipindi kama hiki cha uchaguzi. Kama wewe siyo chama tawala, ningeshauri bora ukae kimya, au usuggest solutions, kuliko kutoa comments ambazo ziko hewani!
   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Jamani hivi nyinyi huu udini utawaisha lini?
  Whay don't we discuss a lot of things we have at hand? Kueni na acheni udini. Avatar ni atar tu!!
   
 14. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Avatar si kitu, haiwezi m-define mtu. Kinachotusaidia ni uelewa na maandiko yake. JeyKey hana tofauti na Malaria Sugu, ukiwaangalia vizuri hata maandika yanafanana!!!

  Wote ni wadini kwa maana hiyo, wanakandamiza kwa kujitambulisha kwa avatar!!!

  Udini ni adui katika jamii yetu tuuache....
   
 15. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu ni mkubwa kama huyu bwana amekubaliwa kugombea segerea. Mimi ni mpiga kura ktk jimbo hili na mwana CCM ninaye chukia ufisadi. Naahidi mbele ya Mungu na mbele ya wanajamvi wote kuwa siku nitakapokutana na Bwana Mpendazoe nitamkabidhi kadi ya CCM na kumhakikishia kura yangu.
  Binafsi sijawahi kumuona wala hatufahamiani hata kidogo, lakini alipodiriki kujitoa CCM na kuacha marupurupu yake yote ya Ubunge alinikuna sana hata kuanza kumuona kama Shujaa wa jamii yetu iliyonyaswa na kugandamizwa na mafisadi wakisaidiwa na watawala wetu.
  Niko tayari sasa kuhamia CHADEMA na kumsaidia Mpendazoe
   
Loading...