Mpendazoe kuhusishwa na mtandao wa madawa ya kulevya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpendazoe kuhusishwa na mtandao wa madawa ya kulevya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 11, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Mpendazoe afichua njama mpya


  na Mwandishi wetu


  [​IMG] ALIYEKUWA mgombea ubunge jimbo la Segerea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Fred Mpendazoe, ameeleza kufanyiwa njama zenye lengo la kumhusisha na biashara ya madawa ya kulevya ili kudhoofisha harakati za kisiasa.
  Mpendazoe ambaye amefungua kesi mahakama kuu Dar es Salaam kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa jimbo hilo yaliyompa ushindi Makongoro Mahanga (CCM), jana aliiambia Tanzania Daima kwamba mwishoni mwa mwaka jana alipata taarifa kutoka kwa mmoja wa Wasamaria wema kwamba upo mpango wa kumpandikizia kesi ya kufanya biashara ya madawa ya kulevya ili imdhohofishe kisiasa.
  Alisema wiki moja baada ya kupewa taarifa hiyo ambayo hakuitilia maanani, aliweza kutengua mtego uliosukwa na watu wanne (majina tunayahifadhi) waliojaribu kumuomba asaidie kununua madawa ya kuhifadhia chakula huku lengo lao likiwa ni kumtegeshea madawa ya kulevya.
  Akisimulia sakata hilo Mpendazoe alisema alipigiwa simu na mtu mmoja aliyedai anafanya kazi Kigoma katika shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) na kumuomba amsaidie kununua madawa ya kuhifadhia chakula jijini Dar es Salaam.
  "Alisema malipo yote wangefanya wao lakini mimi niwasiliane kwanza na msambazaji wao aliyepo hapa Dar anionyeshe sample halafu wao watakuja kulipia madawa yote ambayo jumla yake yangegharimu milioni 150 na kwamba wangenipa kamisheni ya milioni 25. Akanipa na namba ya simu ya huyo msambazaji.
  "Msambazaji wao alisema yupo tayari kumtuma dereva wake aniletee sampuli Ubungo Plaza na sampuli moja ina thamani ya milioni tatu lakini chaajabu yeye alikuwa tayari niletewe bure wakati hata hatujaonana zaidi ya kuzungumza kwa simu tu. Huyo dereva wake alipokuja akataka tuelekee moja kwa moja kwenye gari langu ili aweke hayo madawa nikamwambia asubiri kwanza...nikampigia tena bosi wake na kumuomba aje kwanza angalau tufahamiane.
  Hakuja na dereva wake akaondoka na madawa kabla hata sijayakagua. Tangu siku hiyo nikipiga namba ya huyo muuzaji wa madawa ya vyakula haipatikani na nikipiga ya yule wa Kigoma aliyenituma nimsaidie kuyanunua nayo haipatikani...wote wanajuana" alisema Mpendazoe ambaye amewasilisha maelezo hayo kwa jeshi la polisi ili lifanye uchunguzi.
  Kabla ya sakata hilo, Mpendazoe alieleza kufanyiwa njama nyingine ya kudaiwa kutumia gari la wizi ambalo hata hivyo alithibitisha ni gari lake.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Kwenye Biblia takatifu..fisadi anatafsiriwa ni mtu yoyote yule ambaye kwa matendo na fikra zake amemchukiza mno Mwenyezi Mungu hata kufikia Mwenyezi Mungu kumlaani na hivyo kumruhusu kutenda maovu yoyote yale atakayo...........Jiulize hawa CCM hawajafikia hatua hiyo?
   
 3. k

  kada wa ccm Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ccm ccm oooh chama cha mapinduzi ccm,,,duuh pole mpendazoe ndio siasa za kitz haziko straight rafu nyingiiiiiiiiiii
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Haki ya mtu haipotei Segerea; waache CCM wakupandikizie tu mikesi ya hayo madawa ya kulevya wakati magwiji wa biashara hiyo wanao wenyewe jikoni kwao.

  Shauri yao wakifanya huo ujinga basi wasijeshangaa tutakavyoweka wazi zaidi A MOST DAMAGING LIST ya vingunge vya mihadarati Tanzania halafu tuone kama watakua na pa kujificha tena. Hivi bado wanajidanganya kwamba watu hawajui mambo yao yanayonuka??????????

  Wacha wakatumie hizo mbinu za mwaka wa 47 na wasijejutia milele hata hizi simile za kuwastahi.
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu .... hao jamaa wanaojifanya wanaotoa chance ya ku supply dawa za kuhifadhia chakula UN ni mtandao wa matapeli.... hata mimi wameshawahi kunipigia simu..... nikawapotezea...... it is a big scum.... na wayu wengi wametapeliwa kihivyo
   
 6. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wavivu wa kufikiri hao!
  wanatega mtego wa kitoto namna hiyo! Punguani kabisa hao.
   
 7. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  Huu ni mchezo wa matapeli. Sidhani kama walitaka kumbambikia madawa ya kulevya. Hat hivyo nashangaa mtu kama Mpendazoe anapigiwa simu na watu asiowajua na anakubali kuhadaika! Hebu tutafakari walau kwa dakika moja.... Kuna mtu Kigoma na anataka madawa ya kuhifadhia nafaka. Yupo tayari kukulipa wewe mtu asiyekujua sh milion 25 za kamisheni ili umnunulie hayo madawa.... mh... yeye hataki hizo fedha?
   
 8. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  .....na matapeli huwa wanajua kusoma sana watu... Walimfuata Mpendazoe kwa sababu walijua huu uchaguzi uliopita na hii kesi aliyofungua vimekomba vijisenti vyake hivyo akisikia "dili" kama hili ataingia mtegoni kwa urahisi sana...
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kama sakata la Mengi!
   
 10. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  sio siri Hapo nadhani Mpendazoe keshapigwa (Katapeliwa) na hao jamaa, hao sio jamaa wa madawa ya kulevya bali ni matapeli tu, mimi walishanipigia simu na mchezo ulikuwa ni hivyohivyo na tena kuna mzungu kabisa yupo kwenye hiyo deal
  Nasema keshatapeliwa kwa sababu ilikuwa sio raisi kwa mtu kama mpendazoe apigiwe simu na mtu asiyemjua na anaenda tu, nadhani alienda kwa sababu alikshakubali kufanya hiyo deal, si unajua tena jamaa alishakuwa serikalini kwa hiyo ni mtu wa videal deal vya hapa na pale
   
 11. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yawezekana ni matapeli au walitaka kumchomekea......Lakini Fred uliwezaje kupanga mipango hiyo mpaka kukutana na dereva wa huyo mwuza bangi? huoni ulikuwa kwenye risk exposure? sikunyingine wapotezee juu kwa juu wasije wakakuletea noma kwa style tofauti na fikra zako.
   
 12. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkubwa!kama haya yote wanafanya ili kukudhoofisha ama kukuchafua kwa sababu ya ubunge,ni dhahiri kuwa umewashika pabaya,komaa hapohapo hadi waumbuke...shiinzy!
   
 13. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  uongo wao sikubali
   
 14. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  wezi wanataka kumuharibia mbunge wetu
   
 15. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  mkwere alitangaza kwamba ana list ya wauza madawa ya kulevya ana wasubiri wale bata la krismas na new year ndo awashughulikie! As usual miaka inapita bado drug dealers wakubwa wanakula bata!
   
 16. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Wakuu,Fred naomba issue hii asiihusishe na siasa ni utapeli tu. Kwa stori aliyoieleza iko kama ya bro wangu alipolizwa dola $10,000 kama 12mil tsh mwaka jana. Biashara inatengenezwa kama halali lakini ya kamisheni,wako mpaka wizara ya kilimo,pia wanamtandao mpaka uwanja wa ndege,na mzungu yupo kabisa na sample wanazo. Yan bro alilizwa mchana kweupee! Alienda ubungo plaza,wakamfuata mzungu airport na mchezo uliishia bohari ya madawa ya kilimo ya serikali. Yan kilaini wanakula chao na cm zinazimwa,tena sio ghafla,zinapatikana mpaka siku ya pili ya kulizwa. Bro alikosa wa kumlaumu mana unakubali mwenyewe kilainii. Usicheze na kamisheni ya sh.100milioni! Pole mpendazoe lakini ni utapeli wa kawaida. Kama mpendazoe akieleza zaidi,lazma aseme ukweli alishalizwa mil 10+ . Hawazimi cm kabla hawajapata chao. Yan ni utapeli wa kimataifa!
   
Loading...