Mpekue askari kabla hajakupekua wewe ukijiridhisha ndiyo umruhusu akupekue

Kuna taratibu nyingi zinakiukwa Wakati wa kumpekua mtuhumiwa na ukamataji wake,hii inatokana na wananchi waliowengi kutojua Sheria na askari wengi kukiuka taratibu na sheria au kijifanya Sheria na taratibu hizo haziwahusu wao.
 
Jamani sheria inasema askari akija kukupekua katika eneo lako unatakiwa kumpekua kwanza yeye ukijiridhisha ndiyo umruhusu akupekuwe maana anaweza kuleta kipandikizi.
wavuta bangi mna wasi wasi sana.
Askari haruhusiwi kukupekuwa mpaka aje na kiongozi wa mtaa pamoja na shahidi mwingine utakae pendekeza wewe.
upekuzi ni lazima ufanyike mbele ya watu hao,na kuna fomu rasmi inaandikwa kama kuna kitu kimepatikana kitaelezwa na description yake,kama umepekuliwa na hakuna kitu.Itaandikwa NIL.
Hao mashahidi wataweka sahihi zao na polisi aliekupekua pia ataweka jina na sahihi.
Kwa muktadha huo kubambikiwa ni vigumu sana,acheni kudanganyana
 
Wakija kukupekua wapangishe mstari mmoja mmoja wambie wachomoe mashati na ndimi za mifuko yao kisha wanyanyue mikono juu.

Kisha endelea na zoezi lako la upekuzi.
 
wavuta bangi mna wasi wasi sana.
Askari haruhusiwi kukupekuwa mpaka aje na kiongozi wa mtaa pamoja na shahidi mwingine utakae pendekeza wewe.
upekuzi ni lazima ufanyike mbele ya watu hao,na kuna fomu rasmi inaandikwa kama kuna kitu kimepatikana kitaelezwa na description yake,kama umepekuliwa na hakuna kitu.Itaandikwa NIL.
Hao mashahidi wataweka sahihi zao na polisi aliekupekua pia ataweka jina na sahihi.
Kwa muktadha huo kubambikiwa ni vigumu sana,acheni kudanganyana
Certificate of seizure!! Uko sahihi kabisa.
 
Back
Top Bottom