Mpe neno moja huyu jamaa

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,640
4,426
Msichana mmoja mwanafunzi wa chuo akiwa ndani ya pantoni akivuka kutoka Magogoni kuelekea upande wa Kigamboni alimuona mwanaume Handsome akiwa ndani ya gari yake nzuri.

Bila wasiwasi yule msichana akamfuata mwanaume na kumwambia "Hey you look cute and Handsome...i like you"

Yule mwanaume akiwa na wasiwasi fulani alipandisha kioo cha gari kidogo na akamwambia yule dada "My dear, mapenzi sio kitu kizuri kwako kwa wakati huu, nakuona umetoka chuo bila shaka, wewe bado ni msichana mdogo kuwa na tabia kama hii. Tafadhali sana nenda nyumbani au sijui Hostel na usome kwa bidii, achana na mapenzi soma ili uje ufanikiwe katika maisha."

Baada ya kusema hayo Yule mwanaume akatoa note book yake akaanza kuandika huku akisema "nakuandikia hapa baadhi ya maneno ya busara na muongozo katika maisha yako. Hutakiwi kuwa cheap kiasi hiki mdogo wangu. Nakuomba sana ukasome haya kabla ya kulala."- akampa ile karatasi na akafunga kioo cha gari mpaka juu.

Yule msichana alirudi Hostel kwa aibu kubwa na usiku kabla ya kulala akafungua ile karatasi ili aisome.

Karatasi ilisomeka hivi "wewe ni kipofu? Humuoni Mke wangu yupo kwenye kiti cha abiria amekilaza amelala? Hii ni namba yangu nipigie muda wowote isipokuwa asubuhi sana na usiku. Hata hivyo na mimi nimekupenda sana. Bila shaka hautaniangusha.

*********************

Hebu mpe Neno moja tu huyu Kishoka wa wanawake mzee wa michepuko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom