Mpasuko CCM: Watofautiana juu ya Serikali mbili

Mpasuko CCM: Watofautiana juu ya Serikali mbili

Geeky

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
307
Reaction score
181
Dodoma. Baadhi ya wabunge wa CCM ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamepinga msimamo wa chama hicho unaowataka kutetea muundo wa Serikali mbili katika mijadala ya Bunge hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, wamesema hawaoni mantiki ya msimamo huo, kwa kuwa Katiba inayotengenezwa ni ya wananchi.

Habari kutoka katika kikao cha ndani cha CCM kilichofanyika juzi kati ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya na wabunge wa CCM, baadhi ya wabunge waliweka wazi msimamo wao wa kutaka Serikali tatu.

"Wapo wengi hawakubaliani na msimamo wa CCM wa kutaka watetee Serikali mbili na wanashikilia msimamo wa Serikali tatu, ambao ndiyo msimamo wa wananchi wao," alisema mmoja wa wabunge aliyekaririwa kutoka katika kikao hicho.

Habari zilizovuja kutoka katika kikao hicho, miongoni mwa walioeleza msomamo huo ni Alphaxard Kangi Lugola wa Mwibara, ni miongoni mwa waliokuwa na msimamo mkali kuhusu jambo hilo.

Lugola alipohojiwa jana, alishikilia msimamo wake wa kutaka Serikali tatu akisema anafanya hivyo ili kulinda masilahi ya wananchi anaowawakilisha.

"Mimi kama Kangi Lugola kama mjumbe ninayesimamia walionituma, nataka Serikali tatu… Hapa kuna mambo mawili, msimamo wa chama na msimamo wa mimi kama mwakilishi," alisema.

Lugola aliongeza, "Msimamo huu nitautoa pia kwenye Bunge la Katiba na nitajenga hoja halafu Bunge kama chombo kitaweka mizania, ni muundo upi wa Serikali upite."

Inadaiwa Christopher Ole Sendeka wa Simanjiro alikwenda mbali zaidi na kumweleza Rais Kikwete kwamba hakuna dhambi kubwa aliyotenda kama kuruhusu Zanzibar kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa mujibu wa habari hizo, Sendeka alisema matatizo yote yanayoibuka sasa kuhusu muundo wa Serikali, yanatokana na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ambayo yalivunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 ndiyo yaliyosababisha Zanzibar kutambuliwa kama nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuruhusu Rais wa Zanzibar kuwa na uwezo wa kuigawa mipaka ya Zanzibar, jukumu ambalo ni la Rais wa Muungano.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo jana, Sendeka, alikataa kueleza lolote akisema kikao hicho kilikuwa ni cha faragha.

Mbunge mmoja kutoka Kanda ya Ziwa ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe, aliliambia gazeti hili kuwa kwa uchache, theluthi mbili ya wabunge wa CCM wanataka Serikali tatu.

"Subirini muone moto utakaowaka bungeni siku tutakapofika kwenye hicho kipengele cha Muungano, nadhani halitatosha, tumeamua kusimama na wananchi siyo msimamo wa CCM," alidokeza.

Mjumbe huyo alisema yeye ataeleza wazi kuwa haungi mkono muundo wa Serikali ya CCM unaotaka Serikali mbili na kwamba yuko tayari kukabiliana na adhabu yoyote kama CCM itaona amefanya makosa.

Mbunge wa Beatrice Shelukindo wa Kilindi ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo, alisema awali alikuwa muumini wa Serikali tatu lakini baada ya kuelimishwa, amebadili msimamo huo.

"Ni kweli wapo wana CCM wanataka Serikali tatu, hata mimi nilikuwa huko lakini baada ya kuelimishwa nakubali muundo wa Serikali mbili pale tu kero za Muungano zitakapotatuliwa," alisema.

Alitoa mfano wa mbunge kutoka Zanzibar kuwekwa katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) wakati mambo yanayofanywa na kamati hiyo kwa asilimia 100 yanahusu upande wa Bara pekee.

Mbunge mwingine kutoka Kanda ya Ziwa ambaye naye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema ni usaliti kwa CCM kuwachagulia Watanzania aina ya Muungano baada ya kutoa maoni yao kuhusu jambo hilo.

"Mimi binafsi nataka Serikali mbili lakini siungi mkono kitendo cha chama changu kuweka msimamo wa pamoja na kutaka uwe ndiyo msimamo wa taifa kwani Katiba ni mali ya wananchi," alisema na kuongeza:

Mgawanyiko huo wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, umekuja siku moja baada ya CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kutangaza msimamo wa CCM kama taasisi kuwa ni muundo wa Serikali mbili na imewataka wajumbe wake kusimamia msimamo huo wakati wa mijadala bungeni.

Hata hivyo, Zainab Kawawa alitaka wajumbe wa Bunge la Katiba watakaokwenda kinyume na msimamo wa chama, wanyang'anywe kadi

source : mwananchi.co.tz
 
ukweli huu uajulikana wakati wa mjadala bungeni, hatuna sababu ya kuukubali uzushi wako huu. baadhi ya wabunge, hawana majina?
 
CCM wasiwatishe wanachama wao bure , hawana uwezo wa kuminya demokrasia kiasi hicho, mimi najiuliza inakuwaje mbuge uliyeaminiwa na watu kuwa muwakilishi wao unakubari kuwa bendera fuata upepo ? yaani CCM inataka kuwambia wabunge wao kuwa hawana uwezo wa kufikiri na kuamua wanachokiamini mpaka walazimishwe. Huu utamaduni ukiendelea kuwa hivyo itafika wakati sasa mbuge asiwe na uwezo wa kufanya lolote mpaka asubiri muongozo wa chama. Ikumbukwe kuwa nyinyi sio wa bunge wa ccm hicho ni chama tu mlichopitia bali nyinyi ni wabunge wa wale waliowatuma. Fanyeni kile wanachokitarajia waliowatuma
 
Naona CHADEMA mmejipanga kushinda hoja ya serikali tatu kwa namna yoyote ile, CCM wako smart sana, hawawezi kuja na msimamo ambao wengine hawakubaliani nao. Halafu serikali tatu hapingwi na wana-CCM pekee, juzi nimemsikia Cardinary PENGO akisema serikali tatu, hakuna muungano, na makundi mbalimbali pia hawaungani na hoja hii ya CHADEMA.
 
siyo swala la mbunge mkuu, CCM wana wasomi wazuri sana, wanajua athari za serikali tatu kama ambavyo makundi mengine wakiwemo wanazuoni wanaungana na CCM kuilaani hoja ya serikali tatu kwa vile haina mashiko katika mstakabali wa umoja, undugu ulioasisiwa na viongozi watangulizi wa taifa hili teule la Mungu. Inawezekana kabisa Mwandishi wa habari aliwahoji wana-CCM wafu kama akina MBOWE na weingine waliokumbatia kadi za CCM huku wakiwa upinzani.
 
Source ikiwa Mwananchi au Tanzania Daima bsi tena.
 
ukweli huu uajulikana wakati wa mjadala bungeni, hatuna sababu ya kuukubali uzushi wako huu. baadhi ya wabunge, hawana majina?

mleta mada mwenyewe kaiweka na kusema mkuu, ni wazi ni uzushi tu na wala hakuna mbunge wa CCM anaweza kuwa kinyume na hoja ya serikali mbili, serikali mbili ndiyo muhimili wa Muungano kama kweli tunahitaji kuendelea kujiita watanzania.
 
Naona CHADEMA mmejipanga kushinda hoja ya serikali tatu kwa namna yoyote ile, CCM wako smart sana, hawawezi kuja na msimamo ambao wengine hawakubaliani nao. Halafu serikali tatu hapingwi na wana-CCM pekee, juzi nimemsikia Cardinary PENGO akisema serikali tatu, hakuna muungano, na makundi mbalimbali pia hawaungani na hoja hii ya CHADEMA.

Tlishawazoea hawa.
 
Mimi ni mwana-CHADEMA, lakini napenda serikali moja (nina hoja zake, wala si gharama za kuendesha kama wengine wanavyodai), ikishindikana moja basi walau zibaki mbili halafu Katiba ya Zanzibar ikarekebishwe
 
siyo swala la mbunge mkuu, CCM wana wasomi wazuri sana, wanajua athari za serikali tatu kama ambavyo makundi mengine wakiwemo wanazuoni wanaungana na CCM kuilaani hoja ya serikali tatu kwa vile haina mashiko katika mstakabali wa umoja, undugu ulioasisiwa na viongozi watangulizi wa taifa hili teule la Mungu. Inawezekana kabisa Mwandishi wa habari aliwahoji wana-CCM wafu kama akina MBOWE na weingine waliokumbatia kadi za CCM huku wakiwa upinzani.

Hahaha haahaa et wasomi wazuri
 
Mimi binafsi nilipenda tuwe na serikali moja lakini Zanzibar tayari wamerekebisha Katiba yao na kujitangazia kuwa Nchi yenye serikali yake, rais wake na mamlaka yake, sasa inakuwaje Tanganyika isiwepo pia?
 
Naona CHADEMA mmejipanga kushinda hoja ya serikali tatu kwa namna yoyote ile, CCM wako smart sana, hawawezi kuja na msimamo ambao wengine hawakubaliani nao. Halafu serikali tatu hapingwi na wana-CCM pekee, juzi nimemsikia Cardinary PENGO akisema serikali tatu, hakuna muungano, na makundi mbalimbali pia hawaungani na hoja hii ya CHADEMA.

Ni vema tukawa tunajadili hili jambo bila kuingiza ITIKADI. Hili swala la serikali 3 siyo la CHADEMA, bali zaidi ya 61% ya waliotoa maoni. Inamaana hayo maoni yalitolewa kwa kufata ITIKADI? Na je, hawa wabunge wengine wa CCM wanaounga mkono serikali 3 kinyume na azimio la chama chao ni CHADEMA hao? Ni vema tukatumia hoja kujadili hili bila kujali ni msimamo wa chama gani. KATIBA tunayoipigania siyo ya chama chochote, bali ni ya wananchi wote wa TANZANIA.
 
Hata hivyo, Zainab Kawawa alitaka wajumbe wa Bunge la Katiba watakaokwenda kinyume na msimamo wa chama, wanyang’anywe kadi

source : mwananchi.co.tz
Nimeipenda hii!!
 
Serikali tatu haiepukiki ,maana ndio msimamo wa wananchi asilimia 64 , hivyo wanapotaka tuunge mkono asilimia 24 ya maoni wajenge hoja zao sio kuweka msimamo bila hoja za msingi.
 
Ni jizi pekee anayeweza kusema kuwa kutakuwa na serikali mbili na kero za muungano zikaisha. Hilo liko wazi kabisa na serikali moja kwa wazanzibar ni sawa na kuchoma kisu kikali wanadai watakuwa wamemezwa. Dawa ni kufufua serikali ya Tanganyika na kuunda shirikisho na si muungano. Nawasilisha.
 
maoni ndio mpasuko, matatizo ya waandishi vilaza
 
Sisi wananchi tulishapendekeza maoni yetu vyama vilishapeleka maoni yao then rasim ikatoka na mapendekezo ya wananchi leo yabadilishwe kwa sababu tuu ccm hawayakubali ni kweli?
 
Mbunge yeyote anayetetea serikali mbili hapaswi kurudi bungeni mwaka 2015! Mbunge wa ukweli atasimamia mawazo ya wananchi ambayo ni serikali tatu!
 
Back
Top Bottom