Mpango wa Trump na Marekani ni kuidondosha EU, sio Urusi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,247
Reaction score
16,169
Adui namba moja wa uchumi wa Marekana ni Ulaya iliyoungana na sarafu ya euro. Marekani inakasirishwa na upanuzi wa umoja wa ulaya kuelekea Mashariki. Upanuzi huu wa ulaya unaibana Marekani kwa upande mmoja na China kwa upande mwingine na baadae BRICS kwa upande uleee.

Uingereza kujitoa kwenye umoja wa ulaya ilikuwa moja ya mikakati hiyo. Vita ya Ukraine ni mpango mwingine wa kuisambaratisha EU kiuchumi hasa baada ya kaka mkuu wao Ujerumani kuanguka kiuchumi baada ya kukata upatikanaji wa gesi rahisi kutoka Urusi.

Baada ya ulaya kususia gesi na mafuta ya Urusi, hii imeinufaisha India na China ambazo sasa zinafaidika na rasilimali za Urusi hivyo kuchechemua uchumi wao kwa gharama nafuu. Hii inaitisha Marekani vibaya sana kiasi kwamba inaona ni ujinga mkubwa kuzikosa rasilimali rahisi za Urusi kwasababu ya kijinga ya vita ya Ukraine ambayo imeshindikana kuishinda Urusi inayotegemea ushirika wake na China na India. Kumbuka lengo kuu la vita ya Ukraine ilikuwa kuzipora rasulimali za Urusi na Ukraine lakini lengo hilo linaonekana kama vile liko mbali sana na uhalisia.

Marekani wamebadili gia angani na kuachana na vita ya Ukraine na kuamua kuisogelea Urusi kibiashara badala ya kivita. Ukweli hata huu mkutano wa Trump na Putin huko Alaska haukuwa kwaajili ya Ukraine, bali kwaajili ya kuombana radhi na kuendelea na uhusiano wa kibiashara kati ya Urusi na Marekani. Kama ukimsikia Rais Putin na Makamu wake JD Vance utagundua sasa hivi wanauacha mzigo wa Ukraine kwa umoja wa ulaya pekee ili wazidi kufilisika na hatimaye kuwa dhaifu kiuchumi kiasi cha kuhitaji kuitegemea tena marekani. Ndiyo maana unaona hata baada ya mazungumzo na Trump lakini Putin anaendelea kuitwanga Ukraine bila Trump kusema lolote.

Marekani wamegundua kuwa hawawezi kuishinda Urusi inayoungwa mkono na China, ndiyo maana sasa hivi inataka kurudisha Marekani viwanda vyake vyote kutoka Asia. Iko karibu hata Taiwan itakuwa haina umuhimu tena kwa Marekani.

Vita ya Ukraine imekwisha.
 
Unajua nini viwanda haviwezi kurudi marekani kama atakavyo Trump labda kama huo Urais Trump hataki kuendelea kuushikilia kwa muda mrefu.

Waliomuweka Trump madarakani ndio hao hao wenye viwanda vya mabilioni ya fedha na faida Asia ambayo hayo mabilioni hawawezi kuyapata marekani.

Pili marekani haiwezi kuitupa EU marekani kuiacha ulaya ni wanasema utakuwa ni msumari wa mwisho katika kaburi la utawala wa magharibi hapa duniani.

Ulaya imeeiunga marekani kwenye ushenzi mwingi sana ni Rais mpumbavu pekee atakaye kubali kujenga urafiki na Urusi na kumtenga rafiki na mshirika wa karibu kabisa ulaya.

Kiuhalisia marekani na urusi hawatakuwa na urafiki wowote zaidi ya kunafikiana na kuviziana kinyume kabisa na urafiki wa ulaya na marekani.

Marekani anacho taka kufanya kwa Urusi ni hatari zaidi ndio hicho hicho unacho fikiri anataka kufanya kwa EU lengo la marekani ni kumvuta karibu Urusi na kumtenga mbali na China ili aweze kumuangusha.

Hii michezo marekani haliwahi kujaribu kuifanya huko miaka ya 70s wakati ulipo tokea mpasuko wa mashariki kati ya China na Usovieti
 
Kaka gharama ya kuilinda Taiwan sasa hivi ni kubwa sana. Ushirika wa Urusi, China na NKorea na sasa Iran hatari sana kusema wataendelea kulinda mitaji ya Marekani huko Asia. Ulaya inavyozidi kujitanua ndivyo inavyozidi kuwa na nguvu moja dhidi ya marekani. wanaweza hata kuiwekea vikwazo Marekani kibiashara. Trump analalamika kuwa Ulaya inanunua kidogo sana kutoka marekani na inauza sana Marekani, kitu ambacho hawakipendi kabisa.
 
Marekani imewalazimisha Ulaya kutenga 5% ya bajeti zao badala ya 2% kugharamia ulinzi wao kupitia NATO. marekani wanalazimisha hivyo wakijua kwamba fedha hizo zitatumika kununua silaha bora kutoka Marekani ili kujilinda dhidi ya tishio kutoka Urusi. Marekani anatamani Urusi iongeze mashambulizi yake Ukraine ili Ulaya ijione iko hatarini bila kununua silaha za Marekani. Ndiyo maana Trump hafichi kuwa wao watauza silaha kwenye mgogoro wa Ukraine.
 
Nani kampa marekani jukumu la kuilinda Taiwan ? Trump ni mbwatukaji tu
 
Marekani imewalazimisha Ulaya kutenga 5% ya bajeti zao badala ya 2% kugharamia ulinzi wao kupitia NATO. marekani wanalazimisha hivyo wakijua kwamba fedha hizo zitatumika kununua silaha bora kutoka Marekani ili kujilinda dhidi ya tishio kutoka Urusi. Marekani anatamani Urusi iongeze mashambulizi yake Ukraine ili Ulaya ijione iko hatarini bila kununua silaha za Marekani. Ndiyo maana Trump hafichi kuwa wao watauza silaha kwenye mgogoro wa Ukraine.
Lazima mchango wao uongezeke kwa ajili ya usalama wao wenyewe na pia ulaya nayo ina viwanda vingi tu vya silaha budget hawaongezi kwa ajili ya marekani bali kwa ajili ya usalama wao wenyewe.
 
Adui namba moja wa uchumi wa Marekana ni Ulaya iliyoungana na sarafu ya euro. Marekani inakasirishwa na upanuzi wa umoja wa ulaya kuelekea Mashariki. Upanuzi huu wa ulaya unaibana Marekani kwa upande mmoja na China kwa upande mwingine na baadae BRICS kwa upande uleee.

Uingereza kujitoa kwenye umoja wa ulaya ilikuwa moja ya mikakati hiyo. Vita ya Ukraine ni mpango mwingine wa kuisambaratisha EU kiuchumi hasa baada ya kaka mkuu wao Ujerumani kuanguka kiuchumi baada ya kukata upatikanaji wa gesi rahisi kutoka Urusi.

Baada ya ulaya kususia gesi na mafuta ya Urusi, hii imeinufaisha India na China ambazo sasa zinafaidika na rasilimali za Urusi hivyo kuchechemua uchumi wao kwa gharama nafuu. Hii inaitisha Marekani vibaya sana kiasi kwamba inaona ni ujinga mkubwa kuzikosa rasilimali rahisi za Urusi kwasababu ya kijinga ya vita ya Ukraine ambayo imeshindikana kuishinda Urusi inayotegemea ushirika wake na China na India. Kumbuka lengo kuu la vita ya Ukraine ilikuwa kuzipora rasulimali za Urusi na Ukraine lakini lengo hilo linaonekana kama vile liko mbali sana na uhalisia.

Marekani wamebadili gia angani na kuachana na vita ya Ukraine na kuamua kuisogelea Urusi kibiashara badala ya kivita. Ukweli hata huu mkutano wa Trump na Putin huko Alaska haukuwa kwaajili ya Ukraine, bali kwaajili ya kuombana radhi na kuendelea na uhusiano wa kibiashara kati ya Urusi na Marekani. Kama ukimsikia Rais Putin na Makamu wake JD Vance utagundua sasa hivi wanauacha mzigo wa Ukraine kwa umoja wa ulaya pekee ili wazidi kufilisika na hatimaye kuwa dhaifu kiuchumi kiasi cha kuhitaji kuitegemea tena marekani. Ndiyo maana unaona hata baada ya mazungumzo na Trump lakini Putin anaendelea kuitwanga Ukraine bila Trump kusema lolote.

Marekani wamegundua kuwa hawawezi kuishinda Urusi inayoungwa mkono na China, ndiyo maana sasa hivi inataka kurudisha Marekani viwanda vyake vyote kutoka Asia. Iko karibu hata Taiwan itakuwa haina umuhimu tena kwa Marekani.

Vita ya Ukraine imekwisha.
Mh,hili gogoro ukiangalia Kwa karibu unagundua NATO inakoelekea Haitokuwa na tofauti na jumuiya ya Afrika Mashariki,Urusi ukiichunguza anahakikisha Kuwa Dollar si chochote zaidi ya Kuwa ni karatasi lililoaminiwa,

Swali langu kwako, Urusi yupo tiari kuhakikisha USA anabaki Kuwa juu?
 
Marekani imewalazimisha Ulaya kutenga 5% ya bajeti zao badala ya 2% kugharamia ulinzi wao kupitia NATO. marekani wanalazimisha hivyo wakijua kwamba fedha hizo zitatumika kununua silaha bora kutoka Marekani ili kujilinda dhidi ya tishio kutoka Urusi. Marekani anatamani Urusi iongeze mashambulizi yake Ukraine ili Ulaya ijione iko hatarini bila kununua silaha za Marekani. Ndiyo maana Trump hafichi kuwa wao watauza silaha kwenye mgogoro wa Ukraine.
Noma sana 🔥🤣 so wame jiingiza wenyewe tunduni !?
 
China, India, N.korea, Iran, Russia. Bado South Africa, Brazil kujoin firmly
 
Trump anatamani ajiunge na China na Urusi kuitenga Ulaya. Jumuiya ya Ulaya ndiye adui yake namba Moja kiuchumi duniani. Marekani walihakikisha kuwa Ulaya hawapati mafuta na gesi ya bei rahisi kutoka Urusi inayowapa jeuri. Magari ya Ulaya yanauzwa Marekani lakini Mahari ya Marekani hayauzwi Ulaya, hayako Ulaya. Magari ya ujerumani ni mengi sana Marekani.
 
Back
Top Bottom