Mpango wa siri wa kujenga taifa la wajinga

Mgaya

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
519
2
Hii picha ni ushahidi wa zile habari zinazosemwa mtaani kuwa serikali ya ccm ina mpango wa kuua elimu ya watanzania ili kujenga taifa la watu wajinga wasioweza kuuliza chochote kuhusu mali zao zinazoibwa na kuuzwa kwa wageni kila mwaka.

http://bp1.blogger.com/_HO8ijU76ZcQ/R-TcyCxD0uI/AAAAAAAAPWQ/t15kDjwbqxI/s1600-h/SHULE+2.JPG

picha kwa hisani ya michuzi

Jiulize swali kuwa pesa kiasi gani zinapotezwa kwa makusudi ili zisitumike kujenga shule na kuwapatia watoto kama hawa madawati ya kusomea?
 
Mwana JF mwenye ujuzi wa kuweka picha naomba anisaidie kuweka hiyo picha!
 
SHULE%2B2.jpg
sijaelewa umekusudia kuua kivipi?

hawa wanafunzi wanafanya mitihani. na rangi ya njano level nyengine na hao wengine.

kurahisisha usimamizi wamewekwa pamoja, tatizo liko wapi?

kwani form four na form six si inakaribiana na hivyo wengi kwenye hall?
 
View attachment 1323

Mtu Wa Pwani,

Hawa watoto WAMEKETI CHINI!!! Ni vigumu kwa hawa watoto kuweza kujifunza vizuri na kuelewa kama hali ya mazingira ya kusomea hayaridhishi. Wamebanana na wameketi chini. Nilipokuwa nasoma (nilianza darasa la kwanza mwaka 1961) hadi mpaka leo, sikuwahi kusoma nikiwa nimeketi chini. Kwa maoni yangu, taifa la Tanganyika, na baadae Tanzania la wakati ule, lilifanya juu chini kufanya mazingira yetu ya kusomea yawe bora kwa kiasi kilichoweza. Nilisoma sekondari, high school mpaka chuo kikuu katika mazingira yaliyoniruhusu kutumia kipaji changu cha kuelimika vizuri. Serikali ilikuwa na MOYO na NIA ya kutoa wasomi na wataalamu wazuri. Hebu angalia, wataalamu hao wapo sasa nchini na wengine wametapakaa ulimwenguni kote!

Kiwango cha sasa cha elimu nchini ni duni sana. Tatizo linaanzia kwa kuwepo na waalimu ambao hawana utaalam wa kutosha, na kwa ajili hiyo, wanafunzi nao hawaelimishwi vizuri. Mazingira ya elimu ni ya hali ya chini kwa sababu elimu haikupewa kiupa umbele kinachostahili! Mambo mengine ambayo sio muhimu kwa taifa yamepewa kiupaumbele. Hakuna haja ya kutoa mifano ila kashfa za BOT, Richmond n.k. ni tawsira nzuri ya kufanya malinganisho.

Siri mojawapo ya nchi kuendelea ni kuusomesha vizuri umma wake. Nchi nyingi zilizoendelea zimekazania sana elimu, hasa elimu kwa vijana wake!
 
hii ingechukuliwa ni juhudi za makusudi za ccm kuimarisha elimu ningekubaliana na nynyi.

ccm inasisitiza kila aliefikia umri wa kwenda shule aende, tunajua uchumi wetu hawezi kukidhi nahatijio ya elimu bora kwa waanafunzi wote lkn sio haki kuwanyima wengine elimu ili wachache wakae kwenye viti na wapewe madaftari na vidawati vya wino kama zamani.

tunajua kuna mapungufu na mapungufu hayo ni challenge kwa taifa na ccm ambayo inaongoza taifa.

jitihada zinafanya kuwataka wazee na wananchi wa kawaida wachangie elimu, ingawa wako wengine kwa utashi wa kisiasa wanawachochea wananchi wasichangie.

tushirikiane ufisadi wa fedha za umma ukome na fedha hizo zisaidie elimu na afya na mambo mengine.

tujue ufisadi haufanywi na viongozi au wanachama wa ccm kwa maslahi ya watu binafsi peke yao.

watanzania karibu sote ni mafisadi na tunatakiwa tuache tabia hii

yeyote anaeshindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo hata awe mkilima ni fisadi awe mwalimu ni fisadi awe muuza maandazi ni fisadi.

tujue jukumu la kujenga nchi si la ccm peke yake na wala ccm haina hati miliki ya taifa hili, hili ni taifa letu sote

tuwe tayari kila saa kujiuliza tumeifanyia nn tanzania na sio wameifanyia nn tanzania.

mie nnnaamini tatizo la kuwa nyuma kwa tanzania hakusababishwi na ccm wala chadema bali watanzani wenyew walioluwapo popote pale iwe kwenye vyama au marekani au ingerza au popote.

wangapi wanasaidia nchi zao na kuleta maendeleo ya nchi zao huku wakiwa mahasimu na serikali za nchi zao.

tanzania iko juu kuliko ccm au vyama vyengine watoto wetu amba ndio warithi wa taifa letu hatuna budi wa kuwasaidia kwa hali na mali

pia tukubali hali ya tanzania ya kipindi tulichosoma sisi sio ya leo kwa kila hali, kuna mabadiliko ya akiuchumi kisiasa na kijamii. kabla hujaamua kubwabwaja zingatia sana haya.

natumia nafasi hii kuwalaani wale wote wenye kula michango ya wananchi na pesa za serikali zilizoelekezwa kuinua elimu
 
...Kwa kuongezea hapo kuna ongezeko kubwa la watanzania kulinganisha na miundo mbinu....
 
attachment.php

Inatia aibu lakini kuna viongozi ambao kila mwezi safari za Ulaya na Marekani haziishi kwa kufanya shopping ya nguvu, wakitumia pesa ya walipa kodi.
 
Vipi kama fedha zinazorudishwa za EPA zikipelekwa Wizara ya Elimu? tatizo si litakuwa limepungua sana!! sasa Wabunge wanasema ziende TANESCO ili walipwe RICHMOND, IPTL, SONGAS, at El.. Wananchi hawataweza kuchangia kiasi cha kutosha. tunaoishi vijijini ndiyo tunajua adha zinazowapata wasioweza kuchangia.
 
I still stand by my argument. Tanzania government priorities are misplaced as far as education is concerned. The government sets policies and citizens apply/follow them.

By the way kusema mtu anabwabwaja anapotoa maoni yake, wakati hakumtusi mtu, huo sio uungwana.
 
attachment.php

Inatia aibu lakini kuna viongozi ambao kila mwezi safari za Ulaya na Marekani haziishi kwa kufanya shopping ya nguvu, wakitumia pesa ya walipa kodi.

Nakutumia rasilimali za taifa kwa mambo yao ya kipuuzi na kibinafsi mfano magari ya serikali, kutumia ndege za jeshi kwenye utalii, Kwenda kusalimu mjomba na ndege ya serikali etc etc wanamahesabu wanadai pesa za EPA peke yake bila kuhusisha za Rich Monduli zilikuwa zinatosha kujenga shule za msingi zaidi ya 1000, na madawati na vitendea kazi murua. Bila kusahau kulipa waaalimu vizuri.. sasa tunaishia huku kwa akina kayumba
 
...Kwa kuongezea hapo kuna ongezeko kubwa la watanzania kulinganisha na miundo mbinu....

...Vile vile pamoja na ongezeko la Watanzania,kumekuwa na ongezeko kubwa sana la fedha amabazo zinachotwa kwa matumizi ya watu bibafsi...
 
Nakutumia rasilimali za taifa kwa mambo yao ya kipuuzi na kibinafsi mfano magari ya serikali, kutumia ndege za jeshi kwenye utalii, Kwenda kusalimu mjomba na ndege ya serikali etc etc wanamahesabu wanadai pesa za EPA peke yake bila kuhusisha za Rich Monduli zilikuwa zinatosha kujenga shule zaidi ya 1000, na madawati na vitendea kazi murua. Bila kusahau kulipa waaalimu vizuri.. sasa tunaishia huku kwa akina kayumba

Hawa wanafunzi wako Mkoa wa Kagera ama wapi ?
 
Kulingana na blog ya Michuzi hii shule ya msingi ya amani iliyoko kigogo, wilaya ya ilala, Dar es salaam. Shule hii ina wanafunzi 2989, madarasa 17 na madawati 287 tu.
 
Siwezi kuamini kwamba JK anaona shule hii iko Dar na bado akawa anasema sera ya CCM ya Elimu inatekelezeka .This is madness and a big Mess
 
Vipi kama fedha zinazorudishwa za EPA zikipelekwa Wizara ya Elimu? tatizo si litakuwa limepungua sana!! sasa Wabunge wanasema ziende TANESCO ili walipwe RICHMOND, IPTL, SONGAS, at El.. Wananchi hawataweza kuchangia kiasi cha kutosha. tunaoishi vijijini ndiyo tunajua adha zinazowapata wasioweza kuchangia.

sasa pesa hizi kila pahala zinatakiwa zipelekwe
 
sidhani kama ni kazi ya serikali kujenga na kugharimia shule. Watu wamekuwa wavivu na kutegemea kila kitu kutoka serikalini. Kwa nini hao wazazi hapo wasinunue madawati kwa ajili ya watoto hao badala ya kusubiria serikali iwafanyie.

Ama kweli Mkapa alikuwa right kuwa watanzania ni wavivu. Kila kitu kulaumu serikali na ccm hata kwenye shule?
 
sidhani kama ni kazi ya serikali kujenga na kugharimia shule. Watu wamekuwa wavivu na kutegemea kila kitu kutoka serikalini. Kwa nini hao wazazi hapo wasinunue madawati kwa ajili ya watoto hao badala ya kusubiria serikali iwafanyie. Ama kweli Mkapa alikuwa right kuwa watanzania ni wavivu. Kila kitu kulaumu serikali na ccm hata kwenye shule?

Napenda kutokubaliana wa wewe angalia shillingi pande zote, wananchi wanajitahidi kujenga mashule kwa nguvu zao kujitolea na michango isokuwa mwisho, nakumbuka serikali hukusanya hata kodi ya kuku achilia vichwa vya ng'ombe kwenye zizi...sasa serikali inatakiwa kuhahakikisha inatoa mazingira mazuri kama kupleka waaalimu na kuwalipa vizuri, kama wananchi wamejenga shule basi madawati serikali ipeleke ..sasa unafikiri kodi yako na yangu zinafanya nini? Hebu fikiria kidogo usiwe mvivu
 
sidhani kama ni kazi ya serikali kujenga na kugharimia shule. Watu wamekuwa wavivu na kutegemea kila kitu kutoka serikalini. Kwa nini hao wazazi hapo wasinunue madawati kwa ajili ya watoto hao badala ya kusubiria serikali iwafanyie.

Ama kweli Mkapa alikuwa right kuwa watanzania ni wavivu. Kila kitu kulaumu serikali na ccm hata kwenye shule?

Kama hujui kuwa moja kati ya matumizi ya pesa za serikali ni kugharimia elimu basi umepotea njia. Wananchi wamechangishwa maelfu ya pesa tena kwa lazima huko vijijini kujenga shule na kugharimia kila kitu, kwani matumizi ya kodi za serikali ni nini? Ndio maana pesa zinaliwa maana Kikwete na wenzake kazi yao kusafiri tu na kutumia magari ghali wakati watoto wao wakikaa kwenye vumbi ili kusoma.

Huu si uvivu na huyo Mkapa asubirie tu siku yake mahakamani na jehanam siku ya siku ikifika ajibu mashtaka yote ya kuiba mapesa ya watanzania.
 
mie hujiuliza kulikoni kupinga na kushutumu kila kitu, hata kwa hoja nyaufu kisai hiki.

hivi nani asiejua kuwa jitihada zinafanyika kunyanyua elimu tanzania?

hivi kuonesha darasa moja la skuli kukaa chini ndio kigezo cha kuandaa wajinga?

tupeni takwimu tulikuwa na shule ngapi na walimu wangapi na sasa tuko wapi?

maendeleo si jambo la siku moja, hiki ni kipindi cha mpito tumo kwenda na jitihada zipo, ila wako wahuni na wababaishaji wengi ktk watanzania ambao ni watendaji bila ya kujali vyama vyao au itikadi zao ambao hurejesha nyuma jitihada hizo kwa matashi yao

mbona nchi za wenzetu yako madaarasa wanasoma chini ya miti tena kwenye vumbi, hao angalau wako kwenye jengo na wamekaa juu ya sakafu ya saruji.

bado sijashawishika kama kuna lengo la kuua elimu, ni kweli sijaridhika na hali hii na nnaamini mm ni mmoja ambae nnaamini msaada wangu unahitajika kusaidia elimu na mengine badala kudoea kutafuta udhaifu ili nichonge kwa saaana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom