Mpango wa MUNGU uliuofeli kabla ya kuanza

Mpango wa MUNGU uliuofeli kabla ya kuanza

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
Hapo zamani kidogo kilikuwepo Chama cha siasa ambacho kiliwajenga waumini wake ama wafuasi kuwa Chama hicho ni cha ukombozi ambao MUNGU mwenyewe ndio msimamizi na kiongozi wa mpango huo wa kuanzishwa na kufanikiwa kwa Chama hiko cha siasa...wenyewe wakakiita "MPANGO WA MUNGU"

Kwa kawaida Mungu hajawahi kufeli, hajawahi kushindwa katika jambo lake lolote kwani yeye ni muweza wa kila jambo katika ulimwengu huu na mwingine ila kwa mara ya Kwanza katika historia ya Ulimwengu mpango wa Mungu umefeli tena umefeli kwa aibu kuu.

Kwa watu wenye akili sawasawa wametilia shaka ukweli na imani kuwa huo ulikuwa mpango wa Mungu, kwani MUNGU wanaomjua wao hajawahi kufeli katika mpango wake wowote, bali shetani huwa anafeli tena anafeli kwa aibu, Ni Shetani pekee ambae ameumbiwa kufeli katika kila mpango wake na ni wale wanaoongozwa na shetani tu ndio ambao wanajikuta wanafeli katika kila mpango wao.

Wakati CCM wakishereheka na kuimba "CCM MBELE KWA MBELE" kuna jamaa zetu wa zamani wanagawana mbao huku jahazi lao likiendelea kuzama kwa kasi ya ajabu.

Ndivyo ilivyo, Mshahara wa dhambi ni mauti na mwisho wa UBAYA ni AIBU.

Leo wanaonekana sura zao halisi, rangi zao za kweli ambazo walizificha kwenye ngozi ya kondoo..hawa ni mbwa mwitu wawindaji, wasaka tonge na wabinafsi.

Kila la heri kwa wale ndugu zangu wa MPANGO WA MUNGU!
 
Umeshinda viti maalumu na magamba yenu?

Ameshinda viti maalum huyu naona hatutalala hivi utaratibu upoje kwa magamba huyu kwa kushinda kula za maoni ndio tayari ana tiketi ya ubunge? Mnisaidie ufafanuzi wadau
 
Pesa alizotumia kwenye kampeni Imekula kwake maana viti maalumu inatokana na idadi ya wabunge wa majimbo jambo amblo ccm safari hii hawafiki 100
Ameshinda viti maalum huyu naona hatutalala hivi utaratibu upoje kwa magamba huyu kwa kushinda kula za maoni ndio tayari ana tiketi ya ubunge? Mnisaidie ufafanuzi wadau
 
Shoza

Mwache Mungu na usimtumie kwa mizaa kabisa. Kusema kuwa jambo fulani ni mpango wa Mungu ni wewe mwenyewe ulivyokuwa na imani na unavyojiamini. Nitakupa mfano mmoja na kama ukiuelewa tubu haraka kabla ya kupatwa na dhuruba ya ya unaye mkejeli!

Stefano alipopigwa mawe na kuuwawa na wayaudi huku kijana mdogo aitwaye Sauli aliyechonganisaha akiwa pembeni akifurahia , watu wengi walisema kuwa Mungu amefeli au hana nguvu tena au hayuko. lakini Mungu atabakia kuwa Mungu tu hata akidhihakiwa na akina Shozi atabaki kuwa Mungu, na mipango yake itabaki kuwa juu sana ukilinganisha na ya kwetu na akili zake ni kama mbingu na ardhi ukifanannisha naza kwetu. Yuko wapi saul leo na ni nani aliyeihubiri injiri kumpita yeye, si mitume wala watu waliofundishwa na Yesu. Ukisoma ujumbe huu tubu kwani ni (Rhema kwako)kwa ajiri yako.

Mungu anaweza kuinua mawe yamtumikie sembuse fisadi?
 
Juliana Shonza

Pole sana , mwisho wa ubaya aibu kweli maana now unaogopa jinsi CDM inavyongara
 
Last edited by a moderator:
Naendelea kumshukuru MUNGU kwa kuniongoza mapema na kutokuwa sehemu ya AIBU.
 
uliana Shonza

Juliana niliyewahi kumjua siye huyo, siasa zimekufanya umekuwa wa ajabu kabisa, Juliana umekuwa mwongo unaandika vitu vya ajabu! siasa ni mwana halamu.

Hivi huwa unapata muda na kuyakumbuka maisha yako kabla ya siasa?
 
Last edited by a moderator:
Naendelea kumshukuru MUNGU kwa kuniongoza mapema na kutokuwa sehemu ya AIBU.

Hee! Yaani hujui kuwa sasa ndio uko kwenye aibu? Sidhani kama MUNGU ndiyo alikuongoza kwenda huko, huyo lazima atakuwa ni shetani aliyekudanganya kuwa yeye ni mungu.
Pili nasikia umepita kura za maoni ndani ya ccm, sasa hilo la kuingia Bungeni ujue linategemea CCM itapata kura ngapi kwenye majimbo ya uchaguzi. Kwa picha niionayo sasa hivi kupata hata majimbo 30 ni shughuli pevu. Jiandae kisaikolojia.
 
Pole sana binti wa lumumba.jiandae kuitwa mpinzani baada ya october
 
Kwa hali ilipofikia hata kwa kuwanga kutembea utupu ilimradi magamba yaondoke
 
mtajipakata mwakaa huu acha kelele tulia uone mlishaambiwa ukichezea koki kifuatacho nikulowa sasa unamlalamikia nani humu, tulia cdm ifanye kazi
 
Back
Top Bottom