Hapo zamani kidogo kilikuwepo Chama cha siasa ambacho kiliwajenga waumini wake ama wafuasi kuwa Chama hicho ni cha ukombozi ambao MUNGU mwenyewe ndio msimamizi na kiongozi wa mpango huo wa kuanzishwa na kufanikiwa kwa Chama hiko cha siasa...wenyewe wakakiita "MPANGO WA MUNGU"
Kwa kawaida Mungu hajawahi kufeli, hajawahi kushindwa katika jambo lake lolote kwani yeye ni muweza wa kila jambo katika ulimwengu huu na mwingine ila kwa mara ya Kwanza katika historia ya Ulimwengu mpango wa Mungu umefeli tena umefeli kwa aibu kuu.
Kwa watu wenye akili sawasawa wametilia shaka ukweli na imani kuwa huo ulikuwa mpango wa Mungu, kwani MUNGU wanaomjua wao hajawahi kufeli katika mpango wake wowote, bali shetani huwa anafeli tena anafeli kwa aibu, Ni Shetani pekee ambae ameumbiwa kufeli katika kila mpango wake na ni wale wanaoongozwa na shetani tu ndio ambao wanajikuta wanafeli katika kila mpango wao.
Wakati CCM wakishereheka na kuimba "CCM MBELE KWA MBELE" kuna jamaa zetu wa zamani wanagawana mbao huku jahazi lao likiendelea kuzama kwa kasi ya ajabu.
Ndivyo ilivyo, Mshahara wa dhambi ni mauti na mwisho wa UBAYA ni AIBU.
Leo wanaonekana sura zao halisi, rangi zao za kweli ambazo walizificha kwenye ngozi ya kondoo..hawa ni mbwa mwitu wawindaji, wasaka tonge na wabinafsi.
Kila la heri kwa wale ndugu zangu wa MPANGO WA MUNGU!