Mpango wa kuvuruga GNU wafichuliwa

Mpango wa kuvuruga GNU wafichuliwa

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
858
Reaction score
131
[h=1]Mpango wa kuvuruga GNU wafichuliwa[/h]Written by Mrfroasty (Ufundi) // 04/11/2012 // Habari // 9 Comments

3247324290_10e9e2ddaf_b.jpg


Salma Said, Zanzibar
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad jana amedai kuwepo kwa mpango maalumu unaofanywa na baadhi ya watu wenye lengo la kuvuruga serikali ya umoja wa kitaifa (GNU) visiwani Zanzibar.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kibanda Maiti na kuhudhuriwa na maelefu ya watu Maalim Seif amesema mbinu za watu hao zimeshatambuliwa na kamwe wazanzibari hawatakubali kurejeshwa walipotoka kwa kuvurugiwa kwa serikali yao.
Akiwahutubia wafuasi wa chama hicho alisema mpango huo hauwezi kuwa na mafanikio kwa kuwa serikali ya umoja wa kitaifa imepewa baraza zote na wazanzibari wenyewe kwa kuichagua kwa kura nyingi za maoni na pia serikali hiyo ipo kikatiba hivyo haiwezi kuvunjika.
“GNU is there to stay,….na mimi ndio makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, mpango wao hautafanikiwa tumeshawagundua” alisema Maalim Seif huku akishangiriwa na wafuasi wake. Na kuongeza kwamba.
“Wale wenye ndoto kuwa serikali ya umoja wa kitaifa itavunjika yagujuuu hatutoki hatutoki na ili serikali ya umoja wa kitaifa itoke basi kuitishwe kura ya maoni” alisema Maalim ambaye ni makamo wa kwanza wa rais Zanzibar.
Maalim Seif alisema vitendo vinavyofanywa hivi sasa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na vikosi vya SMZ dhidi ya raia wasio na hatia ni miongoni mwa mipango ya kuwavunja moyo wananchi ili wachukie serikali yao.
Maalim Seif alisema kwa kuwa yeye ni kiongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa hangependa kumsema rais wake hadharani lakini kwa kuwa amefanya jitihada za kuwasiliana na kiongozi wake na kumueleza juu ya vitendo wanavyofanyiwa raia lakini jambo la kusikitisha Dk Shein hajachukua hatua yoyote dhidi ya kusimamisha vitendo hivyo vinavyoendelea ambapo hadi sasa wananchi wanaendelea kupigwa na kufuatwa majumbani kwa kisingizio cha kutafutwa wahalifu.
“Leo naongea kwa masikitiko makubwaaaa nina huzuni kubwa kwa mambo yanayofanyika hapa nchini kwetu na niseme ni mambo ya kishenzi kabisa wanaofanyiwa raia” alisema Maalim Seif.
Katibu Mkuu huyo alisema hapendi kuisema serikali na Rais wa Zanzibar hadharani, lakini analazimika kusema”Rais wangu Dk Shein unatungusha kwa kuwa wewe ndiye mwenye jukumu kubwa zaidi la kulinda amani ya Zanzibar.”
Hata hivyo katika kumkumbusha Dk Shein ahadi yake aliyoitoa siku ambayo anatangazwa mshindi na tume ya uchaguzi miaka miwili iliyopita Maalim Seif alisema “Dk Shein alichukua ahadi kwa wazanzibari wote kwamba atawalinda rai wote bila ya ubaguzi na akachukua hadi kwa Mwenyeenzi Mungu kwamba atailinda Zanzibar basi namuomba Rais wangu mpenzi akumbuke ahadi yeke”.
Katibu Mkuu huyo alimshutumu Rais Kikwete na Dk Shein na watendaji wake huku akieleza masikitiko yake ya kufanya kikao kikubwa Dodoma kinachohusu masuala ya nchi bila ya kumshirikisha yeye kwa kisingizio cha kipengele cha katiba kutomtambua.
“Inasikitisha kuona masuala mazito yanazungumzwa katika kikao ambacho kimewashirikisha viongozi wote isipokuwa mimi eti kisingizio katiba inamtambua waziri kiongozi … haikutaja makamo wa kwanza”
Alisema lengo la kikao hicho ni kuzungumzia vurugu zimetokea Zanzibar katika kipindi cha miezi miwili iliyopita ambapo polisi walilaumiwa kuwa hawakuchukua hatua za kukabiliana na vurugu zilizotokea.
“Viongozi wa ngazi ya juu wa serikali ya umoja wa kitaifa wote walikuwepo kasoro mimi, walishirikishwa kuandaa mpango huo, lakini kila likuepukalo lina kheri nalo na mimi bora nilipokuwa sikuwepo kwa sababu hata siku moja nisingebariki suala hilo.” alisisitiza Maalim Seif.
“Sasa haya yanayofanyika ndio matokeo ya kikao hicho kwa sababu polisi wanalaumiwa hawajachukua hatua sasa hivi ndio hao wanachukua hatua lakini wanafanya udhalilishaji mkubwa sana wa ukiukwaji wa haki za binaadamu, wanawapiga watu ndani ya majumba yao, watu wanahama majumba yao kutokana na unyama wanaofanyiwa mtu anapigwa mbele ya watoto wake mbele ya mkewe na kudhalilishwa jee rais haya hayaoni?” alihoji Maalim Seif.
Akivitaja vikundi ambavyo vinafakazi na polisi, na kutekeleza mpango wa kuvuruga serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuwadhalilisha wananchi ni pamoja na kikosi cha Janjaweed ambacho ni tawi la CCM, Ubayaubaya, kimyakimya, na mbwa mwitu na mbwa mkali ambao wote ni vikundi vilivyopewa mafunzo na sasa kuwafunza watoto wadogo kufanya uharamia.
Akizungumzia athari zilizopatikana baada ya jeshi la polisi kuzima vurugu zilizotokea Oktoba 17 Zanzibar, mwaka huu alisema kumetokea madhara ya kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa Zanzibar kutokana na vyombo vya dola kutumia nguvu ya ziada kudhibiti vurugu hizo.
Aidha alisema hatua za kurejesha amani wakati wa vurugu hizo hazikuwa muafaka, kutokana na nguvu iliyotumika ilikuwa kubwa kupita kiasi na hatua hizo ziliwadhalilisha wananchi wasiokuwa na hatia na mali zao kuhujumiwa, huku wengine wakipoteza maisha.
“Tunalaani mauaji yaloofanywa kwa polisi lakini pia tunalaani udhalilishaji unaofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia na hatuungi mkono kabisa unyanyasaji wanaofanyiwa wananchi hasa katika maeneo maalumu ambao ynajulikana ni maeneo ya wafuasi wa CUF kwa nini iwe hivi” alihoji Maalim Seif.
Maalim Seif alisema serikali na vyombo vya dola vitekeleze jukumu la kulinda haki za raia kwa kuwasaka waliohusika na tukio hilo bila kuwadhalilisha wananchi wasiokuwa na hatia.
Alisema hakutarajia vitendo vya aina hiyo kutendeka wakati huu ambapo mfumo wa serikali ya Zanzibar unaendeshwa kwa kuzingatia maridhiano ya kisiasa baina ya CUF na CCM ambayo lengo lake ni kumaliza uhasama na chuki na kujenga amani pamoja na kuheshimu utawala wa demokrasia.
Katika mkutano huo, Maalim Seif pia alisema mbali ya lengo la kuivuruga serikali ya umoja wa kitaifa lakini wahafidhina wanafanya juu shini ili kuuharibu mshikamano wa wazanzibari ambao kwa kiasi fulani ulikuwa umeonesha nia njema.
Akizungumzia lengo la tatu la wahafidhina hao alisema ni kuogopa mchakato wa katiba ambao unaonesha dhahiri kwamba wazanzibari wanapigania mamlaka kamili ya Zanzibar na kutaka Muungano wa Mkataba jambo ambalo ni mwiba kwa baadhi wana CCM na wahafidhina.
Katika hatua nyengine Maalim Seif aliitupia lawama Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kushindwa kuheshimu mawazo ya wananchi juu ya aina ya Muungano wanaotaka na kusema kwamba tume hiyo imekuwa ikiwalazimisha wananchi waseme kile ambacho wao wanakiamini.
Maalim Seif alimshauri Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Joseph Warioba ahakikishe tume yake inaheshimu mawazo tofauti ya makundi yote, yakiwemo yanayotaka mabadiliko katika mfumo wa sasa wa Muungano kwa kuwa tayari tume imeanza kuonyesha upendeleo kwa baadhi ya makundi fulani.
Awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho. Salim Bimani alisema wazanzibari wamechoshwa na vitendo wanavyofanyiwa kwa kudhalilishwa na kupigwa bila ya hatia huku wneye kufanyiwa vitendo hivyo ni kutoka CUF.
Bimani alisema ni jambo la kusikitisha kuona hakuna hatua zinazochukuliwa licha ya vitendo hivyo kuripotiwa na kuonekana hadharani na kuwataka wananchi wasikubali kurejeshwa walipotoka huku akiwasisitiza kujitokeza kwa wingi katika tume ya mabadiliko ya katiba ili kutoa maoni yao ili kubadili mfumo wa serikali.
“Wananchi msikubali kuchokozeka, nendeni mkatoe maoni kwani hii ni fursa pekee ya kupata katiba tuitakayo” alisisitiza Bimani.
Akisoma risala ya mikoa mitano ya Zanzibar, Khalifa Abdallah Ali alisema imani waliokuwa nayo wazanzibari kwa rais wao Dk Shein imeanza kuondoka na hivyo kumuomba kuchukua hatua ya kusitisha zoezi linaloendelea la vikosi vyake kupita majumbani na kuwapiga wafuasi wa CUF kwa kisingizio cha kuwatafuta wahalifu.
‘Tunamuomba rais wetu Dk Shein imani tuliompa alipokuwa anaingia madarakani ni kubwa na sasa tunamwambia imani hiyo imeanza kutoweka miongoni mwetu na tunamuomba ahadi aliyochukua ya kuhakikisha usalama wa raia wote anautekeleza bila ya ubaguzi kwani hilo ni jukumu lake kama kiongozi wa nchi’ alisema Khalifa.
 
Ndoa tamu bana,achia Miguu mkwaju waja, CUF ilamke vinginevyo inapoteza Imani ya washabiki wake Pemba na unguja
 
Zanzibar hakuna GNU bali the Government of CCM and Seif (GCS). Gnu haiwezi kuhusisha watu wawili watatu bali nusu kwa nusu. Seif ameishiwa kama kawaida yake baada ya wana uamsho wake kustukiwa. Shame on you Seif!
 
Kuna mtu anakumbuka kauli ya Maalim Seif baada ya kuchomwa vibanda vya wafanyabishara wa Tanzania bara (huko Zanzibar) na pia uchomaji wa makanisa?
 
Haya UAMSHO hawatajwi au ndo mtoto.Wa CUF au CUF yenyewe?
Dr Sheni yupo sahihi Sheria ichukue. Mkondo huyo Farid CUF imwekee dhamana tujuwe wazi
 
CUF ni "Chama Tawala" kishiriki, pia ni "Chama Kikuu Cha Upinzani Zanzibar!" Very interesting indeed!
 
CUF semeni ukweli kama mnavyoujua lakini muelewe kuwa dkt Shein amezidiwa na washenzi wenye kupenda machafuko sio Zanzibr tu bali kote duniani.Hata atakapojitahidi kutoa amri kwenye vikosi vyake ataambulia patupu.
Hivyo katika hali iliyopo CUF mtajeni sana Mungu (Allah) katika mikutano yenu bila hofu yoyote.Mshuhudisheni Mungu kwamba mumeona na mumesema.
Kama ambavyo hawana haya kwenda kinyume na katiba na protocol zao wanapotaka kuleta fitna nchini na nyinyi msione haya kumweka mbele Mungu kwenye mikutano yenu.Kumbukeni Huyu ndiye mjuzi wa yote,Mkali wa kuadhibu na asiyeshindwa na hila za Kikwete,Shein wala Warioba na ndiye anayeweza kuwadhibiti Pinda na mtandao wake.
Allah ndiye anayeunda vimbunga na kuvituma kwa nchi nzima pindi uovu ukinyamaziwa,hivyo Yeye tu ndiye wa kuogopwa.
Pamoja na umuhimu wa kujitokeza kutoa maoni kama sehemu ya ushahidi wa kueleza mnachotaka lakini ukweli kulingana na hali ya nchi ilivyo hakuna kitakachopatika chenye kheri kwa Zanzibar wala waislamu wa Tanzania katika mchakato huo.Watu wenye nia mbaya wanakusudia kuwamaliza watu wenye nia njema kwa kuwavunja moyo kiwango cha juu kupitia katiba ijayo.Kumbukeni Allah ndiye Mkuu kuliko njama zao.
 
Maalim Seif lazima akubali kuwa katiba ya JMT inamtambua Waziri kiongozi.
Hakuna short cut ya kumwingiza makamu wa kwanza wa rais, huo ni ukweli mchungu na ni lazima maalim aumeze kama ulivyo.Umakamu wake mwisho ni bahari kuu kama si chumbe.

Ili kujenga hoja yake ametafuta namna ya kuingiza neno Dodoma ili ionekane bara hawataki GNU.
Ukweli ni kuwa hilo halimshughulishi Mtanzania bara yeyote kwasababu halina tija kwakwe.

Maalim Seif anashindwa kuelewa au amegoma kuelewa kuwa vikundi vya Janjaweed, Ubayaubaya, kimyakimya, na mbwa mwitu na mbwa mkali ni vya Wazanzibar wenyewe. Anapaswa aongee na viundi hivyo siyo kutafuta kisingizio cha Dodoma.

Dodoma ni makao makuu ya CCM, akina Sheni na wenzake walikwenda kama wana CCM,yeye angealikwaje?
Asingeweza kualikwa kama makamu wa kwanza wa rais maana mwisho wa himaya yake ni Chumbe.
Hawezi kualikwa kama mwana CCM kwasababu yeye ni mwana ndoa tu haingiliani na ukoo wa kiumeni(CCM).
Mwambieni Seif hizo ndio adha za ndoa, avumilie tu !
 
Seif anawachezea tu Wazanzibari kama kweli anaona serikali inawatendea vibaya wananchi wake alitakiwa ajiuzulu siyo abakie kwenye serikali hiyo hiyo. "Ooh hii nyumba inavuja sana, misingi yake mibovu na tena ina panya na chawa"... sasa hama basi!!!
 
Seif anawachezea tu Wazanzibari kama kweli anaona serikali inawatendea vibaya wananchi wake alitakiwa ajiuzulu siyo abakie kwenye serikali hiyo hiyo. "Ooh hii nyumba inavuja sana, misingi yake mibovu na tena ina panya na chawa"... sasa hama basi!!!
Hiyo akili yako nayo ina walakini.Yaani nyumba ikivuja au ikiingia panya unahama!.Hutaki kuezeka wala kutafuta dawa ya panya.
 
Zanzibar ni nchi huru ina haki kamili ya kufuata mambo yake yenyewe kwa mujibu wa KATIBA yake.

Shein anatumiwa na jirani zenu ili kuleta mfumo usio sahihi kwa Znz.
 
Dawa ya Panya ni kuhama (kujiuzulu) ebo hata hili linakushinda kulielewa !.

Hiyo akili yako nayo ina walakini.Yaani nyumba ikivuja au ikiingia panya unahama!.Hutaki kuezeka wala kutafuta dawa ya panya.
 
Hivi kile kiti chenu UN bado kipo ?.

Zanzibar ni nchi huru ina haki kamili ya kufuata mambo yake yenyewe kwa mujibu wa KATIBA yake.

Shein anatumiwa na jirani zenu ili kuleta mfumo usio sahihi kwa Znz.
 
Zanzibar ni nchi huru ina haki kamili ya kufuata mambo yake yenyewe kwa mujibu wa KATIBA yake.

Shein anatumiwa na jirani zenu ili kuleta mfumo usio sahihi kwa Znz.
:majani7::majani7:
 
CUF na nyimbo yao ya nitoke vp... wameishiwa nawatafuta pa kutokea.
 
Haya UAMSHO hawatajwi au ndo mtoto.Wa CUF au CUF yenyewe?
Dr Sheni yupo sahihi Sheria ichukue. Mkondo huyo Farid CUF imwekee dhamana tujuwe wazi


Ni sawa na Chadema na Ukristo.

Sasa anachofanya Shein ni kutaka kuleta mfumo unaoongoza bara na kuupeleka Znz. kitu ambacho UAMSHO kinapinga kwa nguvu zote.

Kwani kila nchi wana mila, desturi na sirka zao.
 
seif sharif ndiye mwanasiasa aliyebaki hapa tanzania baada ya Nyerere, anazijua siasa, si mwoga, mkweli, jasiri mpenda haki.
 
Hiyo akili yako nayo ina walakini.Yaani nyumba ikivuja au ikiingia panya unahama!.Hutaki kuezeka wala kutafuta dawa ya panya.
Nyumba ya kupanga inapokuwa na matatizo tajwa suluhisho lake ni kuhama,waweza kuvumilia tu iwapo nyumba hiyo ni yako kama Dr Shain!
 
Back
Top Bottom