SoC04 Mpango mkakati Uboreshaji na urahisishaji shughuli na muingiliano maeneo ya biashara katikati ya miji na majiji

Tanzania Tuitakayo competition threads

Jerry Farms

Member
Jul 18, 2022
63
43
Tanzania imekua ikishuhudia mabadiriko mbalimbali ya kimaendeleo, kufuatia mabadiriko haya vijiji vimekua toka ukijiji hadi mitaa, miji hadi manispaa, manispaa hadi majiji nakadharika.

Kufuatia ukuaji huu wa maeneo kasi ya uingilianaji wa shughuli za binadamu ni suala lisiloepukika hivyo kujitokeza kwa changamoto mbalimbali. Andiko hilo litajikita kutazama changamoto mbili zitokanazo na ongezeko la muingiliano huu: Ugeni na masumbufu yake na Ukosefu wa maeneo ya kupumzika yenye miundombinu rafiki katika maeneo ya kibiashara katikati ya miji ma majiji.

Fumba macho na uvute picha wewe ni mgeni katika mkoa XXY upo katikati ya mji na unauhitaji wa bidhaa ABCD. Je utachukua hatua ipi? Katika mizunguko yako Je, umewahi kukumbana na adha ya kupotea pindi uendapo mahali mfano katika soko ama katikati ya mji? Fikiria wewe ni mgeni upo katikati ya Kariakoo na una fikra ya "nikiuliza nielekezwe mahali nimeibiwa" Je, utaweza kweli kuzunguka soko zima kufanya manunuzi?
Picha ya kipande cha eneo la mji wa kibiashara Kariakoo, Dar es Salaam.​
IMG_20240513_200933.jpg

Chanzo: Google Earth​

Tufanye umezunguka ukapata bidhaa! pindi unapochoka kuzunguka kufanya manunuzi Je, umewahi kufikiria ni wapi ukae na kupumzika? Je na wewe ni muhanga wa kuingia maeneo ya kibiashara na kuagiza "soda" angalau upate eneo la kuvuta pumzi ma kupungwa upepo pale unapokua umechoshwa na mizunguko katika mji/soko?
Kufuatia changamoto hizi mbili yaani; changamoto ya ukosefu wa maeneo ya kupumzika yenye miundombinu wezeshi na adha ya kupotea kwa wageni katika maeneo ya kibiashara. Serikali haina budi kuja na mpango mkakati kutatua changamoto hizi.​

Changamoto ya Ugeni wa mahali na kupotea ("ushamba" wa mji)
Hii ni changamoto ambayo imekua ikiwakumba wageni na wasio wageni katika miji na maeneo ya kibiashara mfano maeneo ya masoko makubwa na vituo vya biashara.Kufuatia adha hii baadhi ya wahanga licha ya kupatwa na usumbufu baadhi yao wanaishia kulaghaiwa na kutapeliwa hivyo kuchukia sehemu husika na kutangaza sifa mbaya ya eneo husika. Hii ina athari kwa uchumi hivyo serikali haina budi kuja na suluhusho, moja wapo ya suluhisho hili ni Uanzishwaji wa mfumo wa kidigitali wa kuongoza watu wenye Programu ya ramani za kidigitali kuongoza watu katika maeneo ya miji na maeneo katikati ya miji/majiji ambayo ni vitovu vya kibiashara na shughuli zinginezo.
Mfumo wa kidigitali wa kuongoza watu katika maeneo ya miji na majiji.
Mfumo huu utakua na vipengele vifuatavyo ili kurahishisha safari;
•Ramani za kikanda za kidigitali zinazooneaha huduma, mgawanyo wa eneo na bidhaa.
•Jinsi ya kufika katika eneo husika( mgawanyo wa barabara).
•Gharama za usafiri na njia za usafiri( magari ya umma, huduma za taksi, bajaji, bodaboda nakadhalika. Gharama zitakua zimedadavuliwa kumrahisishia mgeni kufanya machaguo ya usafiri.
•Sehemu ya kuingiza namba ya utambulisho ya mtoa huduma.
•Sehemu ya machaguo ya lugha na maulizo.
•Sehemu ya kujaza taarifa binafsi za mgeni.
•Huduma za dharula.
•Mengineyo
Programu za ramani za kidigitali za kuongoza wageni katika maeneo ya ki-kanda yenye shughuli za biashara na huduma zinginezo.
Hii ni programu yenye ramani ya kidigitali inayoonesha eneo la kimkakati lilivyopangwa kikanda kulingana na huduma na bidhaa zitolewazo mfano ukanda wa maduka ya nguo, pembejeo za kilimo, vifaa vya ujenzi, vifaa vya kielektroniki na nyinginezo. Ramani hizi pia zitaonesha mpangilio wa barabara na alama zingine tambuliwa katika eneo. Programu hii itakua ikitumika kupitia simu janja.

Ramani ya karatasi ngumu zinazoonesha kipande cha eneo husika mgeni anakusudia kwenda. Ramani hizi zitawarahisishia safari wale wasio kua na simu janja.
Uandaaji wa ramani na mfumo wa utambuzi wa eneo.
-Idara ya mipango miji kupitia wataalamu wake wapite katika maeneo yote ya kimkakati na kuchukua alama za utambuzi wa mahali(coordinates) na kuandaa mchoro.
-Wafanye utambuzi wa shughuli/bidhaa zipatikanazo kwa wingi katika eneo.
-Waandae michoro ya ramani za kikanda (ramani zinazooneaha mgawanyo wa huduma na bidhaa katika eneo).
-Wagawe namba za utambuzi kwa wamiliki wa maeneo tambuliwa.
Namba hizi zitakuwa zikitumiwa kurahisisha mawasiliano baina ya mhitaji huduma na mtoa huduma/bidhaa. Mfano mhitaji huduma akishapatiwa ramani ya kidigitali katika simu yake ataingiza namba ya utambuzi ya mtoa huduma na kuoneshwa mahali mhusika alipo katika ramani.
Kuwezesha hili vituo maalumu viwekwe katika malango ya miji na katika vituo vya maegesho ya magari na taratibu zifuatazo zifuatwe kurahisisha muingiliano wa watu.

• Punde mgeni(mpya) anapofika katika eneo la mji la kibiashara atajisajiri na kuelezea anahitaji nini na nini katika eneo la soko.
• Ataingiziwa mfumo wa programu katika simu na kuelekezwa matumizi.
• Kwa wenyeji, pindi watakapofika katika eneo pangwa watafungua mfumo na kuitisha bidhaa ama huduma waitakayo.
• Mfumo wa ramani utafunguka na kumuonesha mgawanyo mzima wa eneo na maeneo bidhaa/huduma zipo.
Picha ya mchoro bunifu kuonesha mfano wa mgawanyo wa huduma na upatikanaji wa bidhaa katika eneo.
IMG_20240513_173521.jpg
Chanzo, picha bunifu ya mwandishi
• Mgeni atatia alama katika mfumo/ramani mahali alipo na kuanza mizunguko yake. Mfano atakwenda mpaka mahali penye nguzo yenye jina la barabara na kutia alama/kujaza taarifa kwenye programu na kuanza mizunguko.

Kila atakapokua akinunua mzigo mkubwa( kwa wateja wakubwa) atakua akijaza taarifa katika mfumo kwa kumbukumbu ya eneo( maana ni vigumu kununua mzigo na kubeba papo hapo), hivyo mwisho wa manunuzi ataitisha mfumo na kuanza kukusanya mizigo yake kwa urahisi. Kuwepo vituo vya maafisa waratibu wa safari ndani ya eneo la kibiashara. Hawa jukumu lao ni kuongoza mfumo, kutoa usaidizi kwa kuwaelekeza wageni/ watu waliopotea na mengineyo.
Angalizo:
Kuepuka changamoto ya lugha mfumo uwe na machaguo ya lugha: Kifaransa, Kiingereza, Kiswahili na lugha zinginezo za mataifa mbalimbali. Kwa wageni watakao kua na changamoto ya uelewa wa matumizi ya mfumo, maafisa waongozaji watakua na majukumu ya kutoa usaidizi. Maafisa hawa watakua na sifa zifuatazo:
-Ujuzi wa eneo la kibiashara( mgawanyo wa huduma na maeneo bidhaa mbalimbali zinapatikana katiaka soko/eneo).
-Wenye mafunzo ya Ukarimu na jinsi ya kuhudumia wageni.
-Wajuzi wa lugha mbalimbali za kitaifa na kimataifa.​
-Waaminifu.

Taarifa juu ya uwepo wa mfumo wa kuongozea wageni katikati ya miji/jiji na katika maeneo ya kibiashara.
Uwepo wa mfumo pekee pasi na watumiaji ni hasara! Taarifa kwa umma haina budi kutolewa ili kuwezesha umma kufaidi matunda ya mfumo huu. Hivyo taarifa zitolewe kupitia:
-Vyombo vya habari( redio,runinga na mitandao ya kijamii)
-Matangazo katika vituo vya magari
-Vipeperushi kwa wageni katika usafiri wa umma(daladala,mabasi,ndege,treni,meli na vivuko).
-Maelezo ubavuni mwa magari yenye safari kuelekea katikati ya mji.
- Njia zinginezo zitakazopendekezwa

Waongozaji wa mfumo
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kupitia wataalamu wa TEHAMA, mipango miji, idara za ulinzi na usalama na maafisa biashara watasimamia zoezi zima.

Faida za mfumo wa ramani za ki-kanda katika maeneo ya kibiashara katikati ya miji na majiji.
•Kuongoza wageni ndani ya mji kwa kuonesha mpangilio wa barabara, maeneo ya bidhaa na huduma na mengineyo.
•Kutambulisha mahali huduma na bidhaa zinapatikana mfano kupitia mfumo eneo la soko litachambuliwa na kuonesha upatikanaji wa bidhaa kimafungu( eneo lenye bidhaa za kilimo, nguo, vyakula na migahawa).
•Kuokoa muda
•Usasa wa mji/eneo la kibiashara na kuvutia wateja zaidi.
•Kuboresha usalama(visa vya wizi na kutapeliwa vitapungua)
•Huduma za kidharula
Mfumo utakua na sehemu ya maulizo( uoneshe mahali karibu na eneo alipo mgeni anaweza pata usaidizi kwa haraka pindi atakapokuwa na uhitaji).
•Kuongeza hamasa ya utalii wa ndani na pato la taifa kwa ujumla.
•Kuwajengea amani wanunuzi wapya pindi waingiapo maeneo ya biashara hivyo kuvuta wateja na kuongeza pato.

Changamoto ya ukosekanaji wa maeneo ya kupumzika yenye miundombinu wezeshi katika maeneo ya kibiashara.​
Ili kutatua changamoto hii serikali kupitia idara za upangaji na mazingira haina budi kufanya yafuatayo:
-Kufanya utambuzi, utafiti na kukusanya taarifa juu ya maeneo yenye uhitaji wa maeneo ya kupumzikia na miundombinu itakayohitajika.
-Kuandaa ramani za mipango miji katika maeneo ya kimkakati na kufanya ubunifu wa mpangilio wa maeneo ya kupumzikia/ jinsi ya uwekaji wa mijundombinu ya kupumzikia.
-Kutenga maeneo pembezoni mwa barabara za watembea kwa miguu katika eneo la kibiashara/katikati ya mji na kuweka miundombinu.
-Kuweka maeneo ya kupumzikia sambamba na maeneo ya kibiashara yenye viti( mabenchi) ya kukalia na kupumzika punde baada ya mizunguko.
-Maeneo ya kupumzikia yaambatanishwe na biashara ya vinywaji na burudani za hapa na pale kumpunguzia uchovu mtu aliepumzika.
Maeneo yahakikishiwe usalama kwa kufungwa kamera za ulinzi vilevile maeneo yawe na nyenzo rafiki kwa mapumziko mfano vivuli kukinga jua na mvua.

Faida za maeneo ya kupumzika katika maeneo ya kibiashara katikati ya miji/ manispaa/jiji.
•Kuchochea mzunguko wa kibiashara.
•Mvuto wa eneo la kibiashara na kuongeza uwekezaji.
•Kupunguza adha kwa wanunuzi na watu wengine wenye shughuli katika mji.
•Kuboresha mazingira na muonekano wa eneo hivyo utambulisho wa kipekee wa eneo kutokana na ubunifu utakao kua umewekwa katika eneo la kupumzikia.

HITIMISHO
Uchumi ni suala nyeti katika taifa lolote, serikali haina budi kuja na mipango mikakati ya kuweka mazingira bora yatakayochochea ukuaji wa uchumi wa taifa na watu wake. Kuingizwa mipango iliyojadiliwa katika andiko hili serikali inaweza kuanza na utekelezaji awamu kwa awamu kwa kuangalia maeneo ya jiji, miji,manispaa na senta za biashara zenye ukuaji wa kasi na kuanza nayo. Hii ndio Tanzania tuotakayo, Tanzania ikumbatiayo teknolojia na yenye kukubali mabadiriko.​
 
Kufuatia changamoto hizi mbili yaani; changamoto ya ukosefu wa maeneo ya kupumzika yenye miundombinu wezeshi na adha ya kupotea kwa wageni katika maeneo ya kibiashara. Serikali haina budi kuja na mpango mkakati kutatua changamoto hizi.​
Changamoto ya Ugeni wa mahali na kupotea ("ushamba" wa mji)
Hii ni changamoto ambayo imekua ikiwakumba wageni na wasio wageni​
Yas, nasubiria hilo suluhisho kwa watu ambao kuyaelewa mazingira dira hasisomagi kabisa 'geographically challenged'. Mi niko kundi la wasio wageni lakini bado wanapoteaga 😁😁


Usasa wa mji/eneo la kibiashara na kuvutia wateja zaidi.
Nmeusoma na kuuelewa, na kuonelea kuwa hata kabla haujawa nchi nzima: mamlaka za miji zinaweza kuweka kwenye mipango yake na kuanza kuutumia. Itapendeza kusikia 'Ebhana ulishafika mji xyz!, yaani kule huwezi potea kila kitu ukisearch tu unaelekezwa hadi ramani ya kufika'

Uchumi ni suala nyeti katika taifa lolote, serikali haina budi kuja na mipango mikakati ya kuweka mazingira bora yatakayochochea ukuaji wa uchumi wa taifa na watu wake. Kuingizwa mipango iliyojadiliwa katika andiko hili serikali inaweza kuanza na utekelezaji awamu kwa awamu kwa kuangalia maeneo ya jiji, miji,manispaa na senta za biashara zenye ukuaji wa kasi na kuanza nayo. Hii ndio Tanzania tuotakayo, Tanzania ikumbatiay
Ahsante sana
 
Yas, nasubiria hilo suluhisho kwa watu ambao kuyaelewa mazingira dira hasisomagi kabisa 'geographically challenged'. Mi niko kundi la wasio wageni lakini bado wanapoteaga 😁😁



Nmeusoma na kuuelewa, na kuonelea kuwa hata kabla haujawa nchi nzima: mamlaka za miji zinaweza kuweka kwenye mipango yake na kuanza kuutumia. Itapendeza kusikia 'Ebhana ulishafika mji xyz!, yaani kule huwezi potea kila kitu ukisearch tu unaelekezwa hadi ramani ya kufika'


Ahsante sana
Hahahaa....mwenyeji anayepoteaga. Ni hatari saana! Ila mjini ni mjini tu! Kuna watu husema Kariakoo haizoeleki😁😁😁
 
Upekee wa miji! Inavutia saana, yaan unaenda mahali unajiamini kabisa
Yas, nasubiria hilo suluhisho kwa watu ambao kuyaelewa mazingira dira hasisomagi kabisa 'geographically challenged'. Mi niko kundi la wasio wageni lakini bado wanapoteaga 😁😁



Nmeusoma na kuuelewa, na kuonelea kuwa hata kabla haujawa nchi nzima: mamlaka za miji zinaweza kuweka kwenye mipango yake na kuanza kuutumia. Itapendeza kusikia 'Ebhana ulishafika mji xyz!, yaani kule huwezi potea kila kitu ukisearch tu unaelekezwa hadi ramani ya kufika'
 
Back
Top Bottom