Yohana Shija Masalu
Member
- Nov 8, 2013
- 33
- 28
Pongezi na shukrani kwa serikali ya awamu ya tano kwa jitihada zake yakinifu katika kupambana na umilki na utumiaji wa madawa ya kulevya nchini mwetu Tanzania. Ni muhimu kwa kila mwananchi na raia mwenye kunia yaliyomema kuungana na serikali katika hili.
Hata hivyo, ni muhimu sasa kwa serikali, mashirika ya umma na binafsi, taasisi na asasi za kiraia, na kila mmoja wetu kupembua kiyakinifu na kiunagaubaga suluhu na njia za kweli na sahihi katika kuwasaidia wahanga wa madawa haya, kwa namna ya pekee walioathirika kwa utumiaji na kuwa sugu kwao.
Kukamata kamata na kutia gerezani ni moja na ni mwanzo wa hatua ya kusaidia. Hata hivyo, kukomea kamatakamata na kuweka watu ndani si msaada sana kwao.