Mpaka wa Belgium na Netherlands

Sijawahi pia kwa gari au miguu hivi mipaka yetu imechorwa?

Sidhani kama imechorwa, nimepita namanga kuelekea Nairobi ingawa ndio mpaka lakini huoni michoro yoyote, pia nilipita Uganda kuja tz hamna ila nilichoona ni mstari wa equator tu ndio umenivutia sana
 
Sidhani kama imechorwa, nimepita namanga kuelekea Nairobi ingawa ndio mpaka lakini huoni michoro yoyote, pia nilipita Uganda kuja tz hamna ila nilichoona ni mstari wa equator tu ndio umenivutia sana

Ila nadhani kwenye mipaka yetu ukipita huko porini unaingia tu nchi nyingine,maana mtaani kwetu kuna mzee mmoja mkenya Hana hata document lakini anaishi na familia yake na kashakuwa Kama mbongo
 
Ila nadhani kwenye mipaka yetu ukipita huko porini unaingia tu nchi nyingine,maana mtaani kwetu kuna mzee mmoja mkenya Hana hata document lakini anaishi na familia yake na kashakuwa Kama mbongo

Ni kweli, mpakani huwezi Ku control maana mjomba anaishi Kenya na ndugu zake wako jirani sana ambayo inakuwa tz kwa mfano
 
Mkuu,
Thanks nilikuwa sijui ndo maana nikawa najiuliza kwamba mgahawani ingekuwaje ukihama kiti unakuwa nchi nyingine,halafu hii ya mpaka kupita katikati ya nyumba ni makusudi au?au ardhi hamna

Swali zuri, ukweli ni kuwa hata sisi kama tukiwa na miji mingi ikapita mipaka yote matokeo yatakuwa hivyo hivyo, wao nchi zao sio ndogo kihivyo ila wamejenga sana mpaka wamefikiana kwenye mipaka.
Nafikiri ni hivyo
 
Ni kama ilivyo kwa mpaka wa rombo kwa taveta ....naomba moto kenya nakuja kupikia tanzania
 
Hahhaa mkuu umenifikirisha sikuwaza hilo,kweli visa ya hapo sasa inakwaje kuvuka upande wa pili

Mkuu sehemu za mpakani muingiliano wao ni kama watu wanaoishi nyumba moja yaani huhitaji visa kuingia upande mmoja unless unapoingia ndani zaidi ndo masuala ya visa yanapokuja
 
Mkuu sehemu za mpakani muingiliano wao ni kama watu wanaoishi nyumba moja yaani huhitaji visa kuingia upande mmoja unless unapoingia ndani zaidi ndo masuala ya visa yanapokuja

Kwahiyo ina maana sisi na nchi jirani huo mwongiliano ni wa kawaida,aiseee ndo maana watu wa mipakani majina yao yanafanana na ya nchi zingine
 
Swali zuri, ukweli ni kuwa hata sisi kama tukiwa na miji mingi ikapita mipaka yote matokeo yatakuwa hivyo hivyo, wao nchi zao sio ndogo kihivyo ila wamejenga sana mpaka wamefikiana kwenye mipaka.
Nafikiri ni hivyo
Wakuu; Ukubwa miji yao Siyo sababu ya kuingiliana kihivyo !! Wao wameshibana na kukubaliana kuwa sote tuishi na tunahitaji kuishi maisha bora !!! Sasa mfumo huo umeridhia pande zote. ( akili pevu na upendo bila ubinafsi) !!!
NB:- ukitazama nchi za ulaya ni nduchu na finyufinyu !! Hawana ardhi kubwa na maeneo makubwa kama nchi za ulimwengu wetu !!
Viol huo mfano wao ni funzo kwetu na wa kuigwa haswa!!
 
Last edited by a moderator:


huu mpaka kati Germany, Nertheland na Belgium unanikumbusha mbali sana! hapo kwenye mduara ndipo zinakutana nchi zote tatu, iliwahi kupiganwa vita ya muda mrefu kugombea hicho kieneo. mwisho wakakubaliana iwe free area kwa watu wote. pakazungushiwa duara na bendera za nchi zote zikachomekwa. Hayo maeneo Niliwahi kuonja shubiri ya Kaubaguzi kwa kukataliwa kuuziwa chipsi na mpika chipsi mmoja kwa upande wa Ujerumani,ninahisi alikuwa Mjerumani ukizingatia jamaa huwa ni wabaguzi,kwa Nertheland na Belgium wao hawana ubaguzi kihivyo
 
Rombo na Kenya hamna kitu kama hii kweli?
 
Hahhaa mkuu umenifikirisha sikuwaza hilo,kweli visa ya hapo sasa inakwaje kuvuka upande wa pili

Wanatumia viza moja inayoitwa Schengen visa..inatumika kwa nchi zaidi ya 20 bila shaka.
 
Ila nadhani kwenye mipaka yetu ukipita huko porini unaingia tu nchi nyingine,maana mtaani kwetu kuna mzee mmoja mkenya Hana hata document lakini anaishi na familia yake na kashakuwa Kama mbongo

Wasiwasi wangu ni kwa Magamba kusajili watu kama hawa kwenye daftari la kupiga kura ili waongeze kura zao!
 
Kuna nchi za EU Schengen haitumiki, kama UK, Bulgaria, Romania, Cyprus na Croatia.

Ni sawa na East African visa, hatuitambui nyumbani kwetu maana hatutaki kuchanganyana madesa hapa.
 
Ila nadhani kwenye mipaka yetu ukipita huko porini unaingia tu nchi nyingine,maana mtaani kwetu kuna mzee mmoja mkenya Hana hata document lakini anaishi na familia yake na kashakuwa Kama mbongo

Uko sahihi mkuu.
 
Very interesting post.Mods keeps this in sticky pls!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…