Mpaka sasa CCM imelazwa chali mkoa wa Mara

Mpaka sasa CCM imelazwa chali mkoa wa Mara

otorokoko

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2012
Posts
2,437
Reaction score
154
uzinduzi wa kampeni za serikali za mitaa mkoa wa mara uliofanyika musoma mjini siku ya alhamisi ukiongozwa na mwenyekiti wa chadema mkoa wa mara(mbunge wa jimbo la musoma mjini) kamanda Vincent Nyerere akishirikiana na mbunge wa nyamagana kamanda Wenje,uzinduzi ulikuwa ni wa kipekee na wenye mapokezi makubwa kwani mpaka sasa pamoja na kwamba ccm wanatumia pesa na vitisho kwa wagombea wa upinzani lakini bado hali yao ni mbaya sana katika mkoa wa mara.Mpaka sasa ukawa ikiongozwa na kamanda Vincent Nyerere wamefanya mikutano isiyopungua mitatu kwa kila siku katika vijiji na wilaya mbalimbali za mkoa wa mara,wananchi wamesema kamwe hawatoweza kuvumilia na kukumbatia uzembe unaofanywa na serikali ya ccm na kwa pamoja watahakikisha ccm haipati kiongozi hata mtaa mmoja.Vijiji ambavyo vimeshapewa elimu ya uraia na kupiga kura ni kata ya Etaro kijiji cha rukuba,kamnyonge,kijiji cha busamba etaro,kata ya mkendo,mara sekondari,bukanga.kesho ni zamu ya wakazi wa kamnyonge kupewa elimu itafuata kibuyi,shirati,tarime,Serengeti,butiama,bunda.
 
Wale mafisadi papa yatahifadhiwa na mabwana zao sasa wale wenzangu na mimi wakina vidampa wa lumumba sijui watakimbilia nchi gani,ukawa tunasubiri kuapishwa 2015 nchi yetu
 
Mtoa hoja mkuu
huo sio ukweli
Mkoa wa Mara?????

Ccm haina pakutokea mimi ni mkazi wa musoma mjini na pia biashara zangu huwa nafanyia bunda kiujumla musoma mjini na bunda ccm haipo kabisa,na bunda wapo tayali kumng'oa wassira
 
Ccm haina pakutokea mimi ni mkazi wa musoma mjini na pia biashara zangu huwa nafanyia bunda kiujumla musoma mjini na bunda ccm haipo kabisa,na bunda wapo tayali kumng'oa wassira

Mkuu musoma mjini na BUNDA sio mkoa wa Mara rafiki bali hiyo ni sehemu tu ya mkoa wa Mara
Mie nipo Nyamongo wilaya ya Tarime
Je huku sio Mara?
Na je huku hakuna CCM kushinda?
Nadhani ulipaswa kutaja hizo sehemu ulizozitaja kuliko kusema mkoa wa Mara
Au sio mkuu?
 
Kiujumla mkoa wa mara ccm haipo tena,tarime mpaka sasa uzinduzi uliofanywa na heche juzi umewasambaratisha ccm,na siku si nyingi jembe la ukweli nyerere anakuja kusimika ushindi hapo tarime na mchezo unaisha kihivyo
 
Ccm iko taabani haina uhakika hata wa kupata mitaa asilimia 10
 
Kiujumla mkoa wa mara ccm haipo tena,tarime mpaka sasa uzinduzi uliofanywa na heche juzi umewasambaratisha ccm,na siku si nyingi jembe la ukweli nyerere anakuja kusimika ushindi hapo tarime na mchezo unaisha kihivyo

Mkuu mimi nadhani wewe ni mwenyeji wa hizo sehemu ulizozitaja
Ndiyo maana wala hata sijaguna wala kubisha!
Coz hayo ndiyo maeneo yako
Ila na mimi huku
ni mwenyeji
Na ni maeneo yangu pia
 
uzinduzi wa kampeni za serikali za mitaa mkoa wa mara uliofanyika musoma mjini siku ya alhamisi ulikuwa ni wa kipekee na wenye mapokezi makubwa kwani mpaka sasa pamoja na kwamba ccm wanatumia pesa na vitisho kwa wagombea wa upinzani lakini bado hali yao ni mbaya sana katika mkoa wa mara.
Hii ni habari njema ila umati wa watu kwenye mikutano ya kampeni sio conclusive evidence ya CCM chali mkoani Mara, determinant ni wapiga kura, na ili CCM ilale chali, hao wapiga kura wengi waipigie Chdema!. Makundi au umati wa watu kwenye kampeni sio kigezo cha ushindi!, nilihudhuria kampeni za Chadema kwenye uchaguzi mdogo majimbo ya Busanda na Biharamulo, kampeni za Chadema zilifunga funika bovu!, na CCM zilidorora hakuna mfano!, lakini kwenye matokeo, kote kuwili ni CCM ilishinda!. Hivyo mpaka sasa, inawezekana ikawa ni kweli mkoa wa Mara CCM chali, na inaweza isiwe!, tusubiri matokeo!.

Pasco.
 
Back
Top Bottom