Mpaka kieleweke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpaka kieleweke

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Graph Theory, Jul 29, 2012.

 1. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Siku moja nikiwa ndo kwanza nimetoka kazini, nilipofika nyumbani sikumkuta mke wangu wala watoto wangu. Lakini chini ya mti wa mchungwa kulikuwa na beseni ambalo ndani yake palikuwa pamejaa maji na katika kutazama kwangu ndani ya hilo baseni, nikaona kulikuwa na mjusi. Nilipowaza sana kwa namna gani amefika ndani ya lile beseni, niliona hakuna uwezekano wa kuwa amefika mle kwa kuapnda kutokea chini, na nilipokuwa bado nawaza namna ambayo alifika ndani ya lile beseni, ndipo nilipotazama kwa upande wa juu wa beseni kulikuwa na matawi ya mti wa mchungwa, ndipo nilipogundua kuwa yule mjusi alianguka ndani ya lile beseni wakati alipokuwa katika harakati zake za kucheza. Na katika kutazama sana, niligundua ya kwamba, yule mjusi alikuwa wa kike, kumbe inawezekana kabisa ya kuwa alikuwa na mme wake wakiwa wanacheza ndipo alipoteleza na kuangukia ndani ya beseni. Na kipindi nilipomkuta yule mjusi, alikuwa amevimba tumbo kutokana na kumeza maji mengi sana hivyo alishindwa hata kutembea, nami nikaanza kuwaza namna ya kumtoa ndani ya lile beseni maana hakuwa na msaada baada ya mmewe kumkimbia, ndipo katika kuwaza namna ya kumtoa kwenye maji, nikafikiria niyamwage yale maji, lakini nikaona ya kuwa haitakua njia nzuri ya kumtoa. Ndipo nikiwa katika kuwaza nikapata wazo, nikatafuta mti ambao niliamua kuuingiza ule mti ndani ya beseni na katika hali ya utulivu kabisa ili yule mjusi asijue kama kuna kitu kipya ndani ya himaya yake, nilifumba macho yangu lakini kumbe ule mti ulisababisha mawimbi ambayo yalimsitua yule mjusi hivyo akaanza kutafuta chanzo cha mawimbi yale. Nikamuona akaanza kujivuta kwa shida kuelekea kwenye ule mti, n alipoufikia, nikamuona akianza kutupa mguu wake mmoja katika ule mti, baadaye akatupa na mguu wa pili baada ya hapo nikaona akaanza kujivuta kiwiliwili chake ili kiwe katika ule mti na alipofanikiwa akaanza kujivuta taratibu katika mti ule na hatimaye akawa amefanikiwa kujitoa ndani ya beseni na hatimaye akaangukia chini. Na alipofanikiwa kuanguka chini, taratibu akaanza kuangaza huku na kule ili kumtafuta aliyemuokoa, hatimaye akawa amekutanisha nami macho yake na aliponiona akajivuta karibu yangu na hatimaye akainua miguu yake ya mbele kama shukrani kwangu.
  Kesho yake nikiwa nimeshasahau juu ya yule mjusi, nilifika nyumbani na nilipofungua tu mlango nikashangaa kumkuta mjusi ili hali si kawaida kukuta mjusi katika nyumba yangu, nami nilipomuona, nikamtazama sana ndipo nikamkumbuka kuwa ndiye yule mjusi wa jana yake naye alipogundua kuwa nimemkumbuka, alisogea karibu yangu na akainua miguu yake ya mbele kisha akacheka sana, na baada ya kucheka akakimbilia hadi chumbani kwangu na baadaye alipokuja mke wangu nilimuambia ya kwamba tumepata mgeni kwa hiyo akimuona mjusi ndani ya nyumba yetu asimuue.
  Ndipo baada ya muda nilihamishwa kikazi, siku nahamisha mizigo yangu, nikiwa najiandaa kuiweka ndani ya gari, nilishangaa nilipomuona mjusi akikimbia kuelekea vyombo vyangu.
   
 2. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Alipovifia vile vyombo alipanda juu yake kisha akainua miguu yake ya mbele na akalia na hapo ndipo ikawa mwisho wa kuonana na rafiki yangu kipenzi ambaye alipokuwa amekibiwa na mme wake, alinipata mimi naye akaamua kuyakabidhi maisha yake kwangu.
  Binadamu kama ilivyokuwa kwa mjusi huyu, tulikuwa tumezama ndani ya tope zito la dhambi, na haikuwepo njia ya sisi wenyewe kujiokoa na wala hakuwepo kiumbe ambaye angeweza kutuokoa. Lakini ndipo Yesu kristo akaamua hivi, aliamua kujishusha na kutwaa umbo la mwanadamu kusudi atutoe dhambini. Katika kitabu cha Wafilipi 2:5-8 tunasoma Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya kristo Yesu; Ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho; Bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; Tena alipoonekana ana umbo kama la mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti,naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo kipindi tukiwa dhambini tena tukiwa hatuna tumaini la kuokoka toka dhambini Yesu kristo aliamua kutwaa namna ya mtumwa kusudi atuokoe toka dhambini. Katika kitabu kile cha Mathayo 26:28 tunasoma Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. Kumbe Yesu alimwaga damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi ya kuasi kwa mwanadamu pale edeni. Kama mjusi kiumbe mdogo kabisa alikumbuka hisani niliyomtendea kwa kumwokoa toka kwenye majii, habari gani kwangu na kwako, je hisani hii aliyoitenda Bwana Yesu kwa ajili yetu, je upo tayari kuifurahia na pia kumpenda mwokozi wa maisha yako? Je upo tayari kuambatana naye?. Katika Warumi 5:8 tunasoma Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi. Kumbe Yesu alikufa kwa ajili yetu kipindi tulipokuwa dhambini, bali sasa kwa kuiamini damu yake kwamba inatakasa na kuondoa dhambi, tunapita toka mautini na kuingia nuruni.
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Mmmm...!
   
Loading...